DUH !!!!!!!!! HAPA TUMEKWISHA
Nashindwa kupata jibu nani anazungumza kwa niaba ya nani, kwani wote waliotangulia kila mmoja anatoa kauli tofauti kama vile ndio kwanza jambo hili limifika mezani kwake. Naanza kwa kuzungumzia kauli ya waziri mwenye amana, mh Ngeleja ambaye alisikika akisema Dowans ni lazima ilipwe, kauli yake hii ilipingwa vikali na baadhi ya mawaziri wenye uchungu na kodi za watanzania akiwemo Mh. Sita pamoja na naibu waziri Mh.Mwakyembe ambao naweza kuwaita kwamba ni wawakilishi wa wananchi na sio wawakilishi wa matakwa yao binafsi. Baada ya hapo mawaziri wengine wengi waliwashambulia Sitta na Mwakyembe wakidai kwamba hawakuwa na haki ya kuzungumzia swala la Dowans eti kwa kuwa sio wizara yao.Leo hii tena Mh. Waziri Mkuu ndugu Mizengwe Pindwa naye kaja na jipya eti swala la kuilipa au kutoilipa Dowans halitapelekwa bungeni kwa kuwa ni swala la kisheria. Kinacho nichanganya hapa ni kwamba je huko mahakama kuu ni nani atakayekuwa mshtakiwa na ni nani mlalamikaji? Mahakama kuu walishasema kwamba hakuna kesi yoyote kuhusu Dowans iliyokwisha andikishwa na kwa taratibu za mahakama ni lazima kuwepo pande mbili, mdai na mdaiwa, mdai ni Dowans tunamfahamu je mdaiwa ni yupi wakati serikali ilisha ridhia kulipa deni? mbona hapa ni sawa na kesi ya nyani kuharibu mazao halafu jaji awe ni tumbili, kweli hapa haki itatendeka kweli !!!!!!!!! Hii ni danganya toto, serikali ituweke wazi kwa hili tumechoka kudanganywa kila kukicha. Kwanza hebu tujiulize, je serikali yetu haina madeni mengine kuancha hili la Dowans? na hayo madeni yana muda gani mpaka leo serikali haijalipa? Kwanini deni hili liwe livaliwe njuga na kila kiongozi wa nchi? Hapa panma utata mkubwa sana. Naamini kuna madeni mengi ya nyuma tangu enzi za Mwalimu Nyerere lakini mpaka sasa hivi hatujalipa. Achilia mbali madeni mengine ambayo mpaka sasa sasa hivi wananchi wazawa na walala hoi wa Tanzania waliokuwa wafanyakazi wa Shirikisho la Afrika Mashariki wazee wetu ambao hawana uwezo wa kujikimu kwa njia yoyote ile wanaishia kupigwa virungu na kumwagiwa maji ya kuwasha na jeshi la kuwalinda viongozi waserikali na kuwanyanyasa pamoja na kuwauwa wananchi. Je malimbikizo ya likizo za waalimu sio deni kwa serikali, mbona haya yote hayashikiwi bango na viongozi wa serikali? Inapotokea ni madai ya wananchi walala hoi serikali inasema kwamba hakuna pesa ila kwa hili la Dowans pesa zipo !!!!!!! Sisi wananchi watanzania tunazikataa kauli hizi za viongozi walafi wanaotaka kutubebesha mzigo huu mkubwa kwa masilahi yao wenyewe. Kwa kauli hii ya Mh. Pinda inaonyesha kwamba serikali yetu yote ni ya kisanii. Nilitegea kwamba mtoto wa mkulima ( Pinda ) angekuwa pamoja na wananchi wa Tanzania ktk kupinga hili. Sasa napata jibu kwamba huyu alikuwa mtoto wa mkulima kwa kipindi hicho lakini sio sasa. Sasa hivi ni sawa na tone la mafuta lililomwagwa baharini. Inawezekani kauli hii haikutoka kwa utashi wake mwenyewe bali ni kwa shinikizo la viongozi mapapa wa ufisadi. Ila kama ni kwa matakwa yake basi tunaweza kumuweka kwenye kundi la akina .............. tutaanza kuingiwa na uoga kwamba ni hata yeye pia sio mwenzetu (mlala hoi)
Hebu turudi nyuma kidogo, nakumbuka wakati Mh. Pinda anateuliwa kuwa waziri mkuu alianza kwa kasi ya hali juu kwa kuhoji ulali wa serikali masikini kama ya Tanzania kununua magari ya kifarahi na ya bei ya juu kwa ajili ya wabunge na mawaziri (Land Cruiser VX) kasi hii ilitugusa wengi na kuamini kwamba huyu PM atakaye tufaa. Baada ya uchaguzi tumemsikia tena eti ndugu yetu huyu amelikataa gari lake jipya eti kwa kigezo cha kwamba magari hayo ni ya bei kubwa na kwamba hata gari lake la awali bado linamfaa kutumia. Jamani, hebu nisaidiani hapa kwani nahisi kwamba uelewa wangu ni mdogo. Hapa nafananisha na baba aliyenunua chakuala halafu kimeshapikwa eti anagoma kula kwa kuwa ni cha gharama !!!!!!!!!! hivi hili linakuingia akilini kweli? Yeye kama mtendaji mkuu wa serikali alitakiwa kuzuia manunuzi ya haya magari na sio kukataa la kwake ambalo tayari limeshanunuliwa !!!!!!!!! Watanzania tunapatwa na wasiwasi kwa hili, haya ni mazingaumbu, mtoto wa mkulima Pinda amesha tutosa hivyo tunamuomba Mh. Sita pamaoja na Mwakyembe wasimame imara kuhakikisha kwamba Dowans halipwi kitu. Msiogope kutishiwa na viongozi mafisadi wanaojali maslai binafsi kuliko ya wananchi wao. Msifungwe midomo katika kuwatetea wananchi ambao ndio wamewapeleka bungeni kuwawakilisha, tunaamini kwamba kwamba mlicho kizungumza hamkuzungumza kama mawaziri au wana CCM bali mmezungumza kama wawakilishi wa wananchi wa Tanzania walio wapa kura zao. Sisi tutakuwa nyumba yenu, hata kama ni kwa maandamano ya nchi nzima kuhakikisha kwamba kodi na jasho la watanzania halipotelei mikononi wa hawa Dowans. Na hata kama ni lazima tuko tayari kuandamana tukiwa uchi wa mnyama kama vile walivyo ahidi baadhi ya wasanii katika kipindi cha jana Jumanne katika kindindi cha "Wanawake Live" cha chanel 5.
Jamani watanzania amkeni kutetea kodi zetu zisitumike vibaya.