Pinda atufunda nini kufanya tunapochukua likizo

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,884
6,885
pakua+(1).jpg

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa mapumzikoni kijijni kwake Kibaoni - Mpanda

Kubadilisha mazingira na kuongea na hawa malaika kwa kweli ni burudani tosha kuondoa virus ndani ya system ya ubongo na hivyo kurudi kazini na fresh mind.
 
hapo ni mpanda kijinini kwake....hao watoto ni wajukuu zake na huko yanki hapo ni mtot wake..........tatizo ni kwamba huyu hana msaada katika nchi hii...
 
hapo ni mpanda kijinini kwake....hao watoto ni wajukuu zake na huko yanki hapo ni mtot wake..........tatizo ni kwamba huyu hana msaada katika nchi hii...

Huyu bwana alikuwa mtu mzuri sana, niliwahi kusafiri naye kwa mara ya kwanza wakati akitoka kugombea ubunge kwa mara ya kwanza toka Mpanda, Tabora nikaungana naye kwenye mabehewa ya abiria daraja apili, hakuwa na makuu na kuonekana wa kawaida tu. Halafu yuko very social. Sasa ndani ya CCM hata uweje itashindikana, unalazimika kuwa popo vinginevyo utajiweka katika kundi fulani. Upopo wa Pinda ni bora kubaki neutral kuliko kujifanya mjuaji na kubaki kufedheheka, afadhali abaki kulaumiwa tu.
 
nimeipenda hii picha see.......
anaonekana kutulia kabisa.......yupo na wajukuu zake.
 
mtoto wa mkulima.alafu hao wajukuu hawajui kama babu yao ni waziri mkuu.wao wanajua babu tu safi sana
 
hawa watakuwa ni wajukuu zake anawahadhia hadidhi za uongo eti uchumi wa Tanzania umekuwa halafu eti serikali imelitambua suala ruhanjo kwa hiyo watalifanyia kazi sasa sijui hawa watoto wanaelewa
 
Huyu jamaa yani asingekua muoga ndio alifaa kuwa mrithi wa jakaya lakini tatizo lake uoga maskini!
 
Huyu jamaa yani asingekua muoga ndio alifaa kuwa mrithi wa jakaya lakini tatizo lake uoga maskini!

HAFAI, HAFAI kabisa huyu ni mnafiki sana!! Anajifanya maskini kumbe tajiri wa kutupa; ameficha mali zake kwa SUMRY!
 
HAFAI, HAFAI kabisa huyu ni mnafiki sana!! Anajifanya maskini kumbe tajiri wa kutupa; ameficha mali zake kwa SUMRY!

Hayo maneno cku hz ctzki hata kuyasikia. Umbea mtupu. Nakumbuka kipindikile Mwl Nyerere anapanda ndege kwenda kwenye matibabu, kunamtu aliniambia kwamba Jamaa ana visima vya mafuta huko uarabuni ndo anaenda kuvitembelea anasingizia matibabu!!?? Akarudi kwenye Jeneza. Hivyo visima viko wapi? Kweli visinge fahamika mpaka leo???? Umbea mtupu.
 
Jamani hata tabasamu?
Aonyeshe kufurahia basi kuwa na hao wajukuu zake.
 
Anatufundisha kuwa tunapopata likizo turudi kijijini kupumzika tukiwa na familia zetu
 
Jamani hata tabasamu?
Aonyeshe kufurahia basi kuwa na hao wajukuu zake.

Atatabasamu ataweza? Hapo anawaza jinsi CDM inavyozidi kuwashika pabaya...na jinsi wenzake wanavyohaha kutafuta hati fungani pale magogoni ili kuinusuru nchi!!!
 
Atatabasamu ataweza? Hapo anawaza jinsi CDM inavyozidi kuwashika pabaya...na jinsi wenzake wanavyohaha kutafuta hati fungani pale magogoni ili kuinusuru nchi!!!

Ukweli unabaki kama ulivyo, anaonekana kutulia vizuri sana katika likizo yake kule kijijini. Hata mimi nifikapo kijijini nilikozaliwa huwa najisikia kama nazaliwa upya. Sijajua wenzangu waliozaliwa mijini. Na kabisa hao malaika waliomzunguka ni faraja tosha.
 
Hawa watoto wanaangalia nini hapo?!?Kweli ukiwa mzee aibu inaisha mbele ya wajukuu zako!!
 
Atatabasamu ataweza? Hapo anawaza jinsi CDM inavyozidi kuwashika pabaya...na jinsi wenzake wanavyohaha kutafuta hati fungani pale magogoni ili kuinusuru nchi!!!

Yani haonekani kufurahia kabisa. . . kweli ufisadi kazi.
 
Back
Top Bottom