pinda apokewa na mabango yanayoishutumu CHADEMA

Mujumba

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
853
Reaction score
306
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amepokewa wilayani Missenyi kwa mabango yanayokemea kauli za CHADEMA zinazoashiria uvunjivu wa amani.Katika hali inayoonyesha kukerwa na siasa za namna hiyo, wananchi hao jana walibeba mabango yanayosomeka 'maandamano, vurugu, jeshi haviwezi kuongoza nchi, hiyo si demokrasia' na ëTendwa chukua hatua dhidi ya CHADEMA sasa'.

Hata hivyo, mabango mengine yalikuwa yakitoa pongeza na kumkaribisha Pinda wilayani humo, ambayo yalisomeka: ëHongera Rais Jakaya Kikwete kwa ushindi katika uchaguzi mkuu' na 'Karibu Missenyi mtoto wa mkulima Mizengo Pinda'.Waziri Mkuu alipokewa kwa mabango hayo katika uwanja wa Mashujaa, Gunazi, ambako aliyasoma baadhi kabla ya kuanza kuhutubia wananchi.

“Tangu nimeanza ziara mkoani Kagera sijakutana na hali hii," alisema Pinda baada ya kusoma mabango hayo yaliyokuwa yamebebwa na wananchi wa rika tofauti.

Awali, akiwa katika wilaya za Karagwe na Ngara, Pinda aliwataka wananchi kukataa kitu chochote kinachoweza kuwaondoa katika amani waliyoizoea.

Waziri Mkuu Pinda alitoa kauli hiyo baada ya baadhi ya wananchi waishio mipakani kutoa kilio chao kuwa, viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakipita na kuwatisha, wakitaka wawaunge mkono kuiondoa serikali madarakani watakapoamua kuingia msituni kutumia nguvu ya umma.

Pinda aliwataka wananchi kutokubali jambo lolote linaloweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi, hivyo wapuuze wanaoneza chuki.

IUkimuona mtu anahamasisha watu kufanya maandamano na kuwashawishi kutumia mapanga ili wapate serikali huyo ni mtu aliyekosa kazi ya kufanya, msimsikilize wala kumpa nafasi. Wasiwanyime usingizi, fanyeni kazi ili kujiletea maendeleo, alisema.
 
si ndo yanayosemwa na CCM, kama kweli yalikuwepo yaliandaliwa na CCM, unataka CCM wawapongeze Chadema, waambie wamechelewa na huyo Pinda wao aliepinda akili.
 
na yale ya CHADEMA si huwa yanaandaliwa na chadema au na TLP,CUF au CCM? try to be realistic man
 
kashaka jinalako linaonyesha ulivyo mshamba nyie ndiyo mnaburuzwa mpaka mwisho wa dunia, CCM wote mmepinda kama pinda(PM)
 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amepokewa wilayani Missenyi kwa mabango yanayokemea kauli za CHADEMA zinazoashiria uvunjivu wa amani.Katika hali inayoonyesha kukerwa na siasa za namna hiyo, wananchi hao jana walibeba mabango yanayosomeka 'maandamano, vurugu, jeshi haviwezi kuongoza nchi, hiyo si demokrasia' na ëTendwa chukua hatua dhidi ya CHADEMA sasa'.

Hata hivyo, mabango mengine yalikuwa yakitoa pongeza na kumkaribisha Pinda wilayani humo, ambayo yalisomeka: ëHongera Rais Jakaya Kikwete kwa ushindi katika uchaguzi mkuu' na 'Karibu Missenyi mtoto wa mkulima Mizengo Pinda'.Waziri Mkuu alipokewa kwa mabango hayo katika uwanja wa Mashujaa, Gunazi, ambako aliyasoma baadhi kabla ya kuanza kuhutubia wananchi.

"Tangu nimeanza ziara mkoani Kagera sijakutana na hali hii," alisema Pinda baada ya kusoma mabango hayo yaliyokuwa yamebebwa na wananchi wa rika tofauti.

Awali, akiwa katika wilaya za Karagwe na Ngara, Pinda aliwataka wananchi kukataa kitu chochote kinachoweza kuwaondoa katika amani waliyoizoea.

Waziri Mkuu Pinda alitoa kauli hiyo baada ya baadhi ya wananchi waishio mipakani kutoa kilio chao kuwa, viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakipita na kuwatisha, wakitaka wawaunge mkono kuiondoa serikali madarakani watakapoamua kuingia msituni kutumia nguvu ya umma.

Pinda aliwataka wananchi kutokubali jambo lolote linaloweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi, hivyo wapuuze wanaoneza chuki.

ìUkimuona mtu anahamasisha watu kufanya maandamano na kuwashawishi kutumia mapanga ili wapate serikali huyo ni mtu aliyekosa kazi ya kufanya, msimsikilize wala kumpa nafasi. Wasiwanyime usingizi, fanyeni kazi ili kujiletea maendeleo, alisema.

Crap of the month!

(congratulations kashaga, ama kweli we umeshaga sana by the way huko makwetu kushaga= kuzidi)
 
Congratulation Mashaga for archieving ''Holy Crap of the Month" thread.....by the way if u could try to upload the photoz,it could the Crap of the year 2011.
 
Photos please!!!!!!!! ...hata photoshop pia bomba tuu man.....kashaga......
 
Mabango siyo ishu: maneno yaliyoandikwa kwenye mabango hata kwenye kanga yapo. Hiyo ni danganya toto. Kagera hawadanganyiki.
 
na yale ya CHADEMA si huwa yanaandaliwa na chadema au na TLP,CUF au CCM? try to be realistic man

Kadanganye Vihiyo wenzako, kila mwenye akili analijua hili haha wakati wa kampeni mlikuwa mnasafirisha watu kuja kwenye mikutano yenu ili mwonekane mnakubalika.................puuuuuuuuuuuuu, fyuuuuuuuuuu.
 
Sasa nimeelewa kumbe kwa nyie watu wa misenyi AMANI ni kutosikika kwa milio ya risasi na makombora, ila kulala njaa na kufa kama kuku wanaougua kideri kwa kukosa dawa hata ya malaria ni sharehe, basi tutachelewa sana kuendelea kama hatuna tafsiri ya pamoja juu ya amani.

KAKA UMETUMWA na kwa sababu hujui ulitendalo tunakusamehe saba mara sabini na kukuombea wewe na wenzio wenye mtazamo kama wako.
 
Kadanganye Vihiyo wenzako, kila mwenye akili analijua hili haha wakati wa kampeni mlikuwa mnasafirisha watu kuja kwenye mikutano yenu ili mwonekane mnakubalika.................puuuuuuuuuuuuu, fyuuuuuuuuuu.
Sasa hivi wanajifanya wamesahau
 
..hongereni CCM!! hiyo inabadilisha ukweli wa yale wanayoyasema CDM?? mimi nitafurahi na kuwaona mna akili kama mta-deal na wanayowashtakia CDM kwa wananchi-FULL STOP!

Hata kama hayo mabango yatabandikwa kila baada ya mita 50 (kama ilivyokuwa wakati wa kampeni) haitasaidia. Kwa faida yenu, chuki ya wananchi dhidi ya serikali inazidi kuongezeka na si suala la CDM bali wananchi wenyewe wanaona uhalisia wa blunders zenu. Hivyo nyie jifarijini tu na mabango na kauli za vitisho za watu wasio na moral authority yeyote kwa jamii.

Kama mnategemea kusalimika kwa vitisho dhidi ya CDM kupitia mtu kama Wassira (Tyson), Tambwe Hizza, Chiligati you're finished...honestly, hawa watu hawana thamani, heshima wala tunu mbele za wananchi wa JMT.
 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amepokewa wilayani Missenyi kwa mabango yanayokemea kauli za CHADEMA zinazoashiria uvunjivu wa amani.Katika hali inayoonyesha kukerwa na siasa za namna hiyo, wananchi hao jana walibeba mabango yanayosomeka 'maandamano, vurugu, jeshi haviwezi kuongoza nchi, hiyo si demokrasia' na ëTendwa chukua hatua dhidi ya CHADEMA sasa'.

Hata hivyo, mabango mengine yalikuwa yakitoa pongeza na kumkaribisha Pinda wilayani humo, ambayo yalisomeka: ëHongera Rais Jakaya Kikwete kwa ushindi katika uchaguzi mkuu' na 'Karibu Missenyi mtoto wa mkulima Mizengo Pinda'.Waziri Mkuu alipokewa kwa mabango hayo katika uwanja wa Mashujaa, Gunazi, ambako aliyasoma baadhi kabla ya kuanza kuhutubia wananchi.

"Tangu nimeanza ziara mkoani Kagera sijakutana na hali hii," alisema Pinda baada ya kusoma mabango hayo yaliyokuwa yamebebwa na wananchi wa rika tofauti.

Awali, akiwa katika wilaya za Karagwe na Ngara, Pinda aliwataka wananchi kukataa kitu chochote kinachoweza kuwaondoa katika amani waliyoizoea.

Waziri Mkuu Pinda alitoa kauli hiyo baada ya baadhi ya wananchi waishio mipakani kutoa kilio chao kuwa, viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakipita na kuwatisha, wakitaka wawaunge mkono kuiondoa serikali madarakani watakapoamua kuingia msituni kutumia nguvu ya umma.

Pinda aliwataka wananchi kutokubali jambo lolote linaloweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi, hivyo wapuuze wanaoneza chuki.

ìUkimuona mtu anahamasisha watu kufanya maandamano na kuwashawishi kutumia mapanga ili wapate serikali huyo ni mtu aliyekosa kazi ya kufanya, msimsikilize wala kumpa nafasi. Wasiwanyime usingizi, fanyeni kazi ili kujiletea maendeleo, alisema.
NIWAELIMISHE NDUGU ZANGU:
CCM tukitaka tukubalike kwa wananchi KWA HIARI, tutekeleze ilani ya Chama na ahadi za uchaguzi. pia tuache kuogopana na kupendeleana....hivi vtiatuondoa madarakani na kukataliwa katika jamii, tupende tusipende huo ndio mwelekeo. MWENYE MACHO? KILA MWENYE SIKIO....
 
Back
Top Bottom