Pinda anamwamulia Rais? Kuongeza ukubwa wa Serikali

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,463
2,289
Pinda akubali wazo la kuigawa Wizara

Mwananchi
13 August 2011 20:37
Habel Chidawali, Dodoma

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameahidi kuwasilisha kwa Rais Jakaya Kikwete pendekezo la kuigawa Wizara ya Nishati na Madini ili ziwe wizara mbili.Pinda alisema hayo akikubali mapendekezo ya wabunge waliosema wizara hiyo imelemewa na majukumu hivyo wazo la kuigawa itaboresha muundo wa Tanesco pamoja sekta ya madini.

Jambo la kugawa Wizara ni zuri sana na ni jambo jema, hivyo tutalipeleka kwa Rais ili kuona namna bora ya kulifanyia kazi na kwa kuwa sisi ndio washauri wake, bila shaka atakulikubali kwa maslahi ya nchi, alisema Pinda.

Awali, Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), alishauri Wizara hiyo igawanywe kwa kile alichokieleza kwa imekuwa na mzigo mzito. Waziri ametumia zaidi ya asilimia 90 ya muda wake kujibu masuala ya umeme tu ambayo hata hivyo hakumaliza wakati asilimia 10 ya muda wake ndio ametumia kujibu mambo ya madini kwa hiyo mnaweza kuona ni namna gani Wizara hiyo ilivyo na kazi kubwa, lazima igawanywe, alisisitiza Cheyo.

Hata hivyo Pinda alisema hana ubavu kugawa Wizara, lakini akasisitiza kuwa atawasilisha ombi hilo pamoja na kumshauri Rais ili apunguze mzigo wa Wizara hiyo.Kuhusu kauli ya Serikali kuwa lini tatizo la dharura litakoma, Pinda alishindwa kutoa jibu la moja kwa moja na badala yake akasema Tutajitahidi kwa kuwa suala hili limekuwa ni la muda mrefu.

======

Itakumbukwa wakati wa kulipuliwa skandali la Katibu Mkuu Madini na Nishati, David Jairo, Waziri Mkuu Pinda alitamka Bungeni ana hakina Rais atafanya vile atakavyomwambia na anavyodhani yeye inatakiwa kufanywa kuhusu Jairo.

Kuna baadhi tunaamini ni makosa kutangaza yale utakayoenda kumshauri Rais na kuuhakikishia umma kwamba yatapita, kwa vile kufanya hivyo ni kumweka mkubwa wako wa kazi pabaya mbele ya umma kwa yeye kulazimika kuamua vile ulivyowaahidi wewe wananchi. Halafu baadae analaumiwa ambae hakuwa na jinsi (Rais) katika mchakato wa uamuzi fulani.

Sasa Waziri Mkuu anaahidi Rais atakubaliana na ushauri wake kwamba Wizara ya Madini igawanywe, kitu ambacho ukikiangalia vizuri kina pande mbili. Kuongeza ukubwa wa serikali nalo ni tatizo, mawaziri wengi na wizara nyingi na matumizi makubwa si suluhisho la matatizo yetu.
 
Back
Top Bottom