Na Richard Makore
20th November 2011
B-pepe
Chapa
Maoni
Gavana wa Benki Kuu, Profesa Beno Ndulu
Serikali imemuagiza Gavana wa Benki Kuu, Profesa Beno Ndulu kuandaa Semina kwa ajili ya wabunge ili kuwapa elimu juu ya mdodoro wa uchumi unaolikumba taifa hivi sasa.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akiahirisha bunge ambapo alisema wabunge watapata fursa ya kujadili kwa kina hali ilivyo ya mwenendo wa viashiria vya uchumi, athari zake kwa nchi pamoja na hatua zinazochukuliwa na serikali.
Alisema semina hiyo itafanyika katika mkutano wa sita wa bunge utakaoanza mwezi Januari mwaka 2012 ambapo wabunge wote watapata fursa ya kushiriki na kutoa michango yao.
Kuhusu mchakato wa maandalizi ya mabadiliko ya katiba, Pinda alisema anaamini kwamba maelezo yaliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete juzi kupitia hotuba yake yatatoa uelewa na hivyo kuwafanya Watanzania kushiriki katika mchakato huo.
Alisema muswada wa kuunda tume ya kuratibu maoni ya kuandika katiba mpya ulisimamiwa vizuri na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria na kwamba ilifanya kazi nzuri na ambayo imeonyesha njia.
Aliwataka wananchi kutekeleza maelekezo ya Rais Kikwete kuhusu kushiriki katika hatua mbalimbali zinazofuata baada ya muswada huo kupitishwa na bunge ili mwisho wa siku katiba mpya iweze kuandikwa.
Aliwataka Watanzania wote kuungana kwa pamoja na kutekeleza hatua itakayofuata ambayo ni kutoa maoni yao kwa Tume itakayoundwa na Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein.
Aliwaomba viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa kupongeza hatua iliyofikiwa na kukubali muswada huo ambao tayari umepitishwa kwa maslahi ya taifa.
Alitoa wito kwa wananchi wote vikiwemo vyama vya siasa kuungana kwa pamoja katika hatua muhimu inayokuja ambayo itahusisha watanzania wote ya kutoa maoni ya katiba wanayoitaka.
Aliwasihi wananchi kuzingatia yale yote aliyoyasema Rais Kikwete katika hotuba yake ili hatua zote za kuelekea katiba mpya ziweze kufanyika kwa amani na utulivu wa Nchi yetu.
Aidha, Pinda alimpongeza Spika wa Bunge kwa namna alivyoongoza mijadala mbalimbali iliyoibuka bungeni.
Kuhusu hali ya chakula nchini, Pinda alisema, nchi imekuwa ikikabiliwa na hali ya ukame wa mara kwa mara kwa muda mrefu tangu mwaka 2006 hali ambayo imesababisha upungufu wa Chakula katika baadhi ya Mikoa ambayo imekuwa ikiathirika zaidi na ukame.
Hata hivyo, Pinda alisema chakula ambacho kimekuwa kikizalishwa katika maeneo yenye mvua za kutosha kimewezesha nchi kuendelea kujitosheleza kwa kiwango kikubwa. Alitoa mfano, katika mwaka 2010/2011 uzalishaji wa mazao ya chakula unakadiriwa kufikia tani milioni 12.81 ikilinganishwa na mahitaji ya jumla ya tani milioni 11.50 za chakula kwa mwaka 2011/2012.
Alisema uzalishaji huo unatosheleza mahitaji ya chakula kwa asilimia 111, sawa na ziada ya tani milioni 1.31 na kuongeza kuwa ziada hiyo inatokana na mazao yasiyo ya nafaka. Alisema uhaba wa nafaka ni kiasi cha tani 410,000 kwa nchi nzima na upungufu huo upo zaidi kwenye baadhi ya mikoa inayokabiliwa na ukame.
Pinda alisema tathmini ya kina ya hali ya chakula na lishe nchini iliyofanywa mwezi Agosti na Septemba 2011, inaonesha kuwepo kwa jumla ya watu 1,062,516 katika Wilaya 52 za Mikoa 15 wanaokabiliwa na upungufu wa chakula (Acute Food Insecurity) kwa viwango mbalimbali.
Wananchi hao wanahitaji tani 38,843 za chakula cha msaada kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2011.
Waziri Mkuu alisema, hadi Oktoba 31, jumla ya tani 13,905 za chakula zilikuwa zimechukuliwa kutoka maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na kusambazwa katika maeneo hayo yenye uhaba wa chakula na kwamba kazi hiyo inaendelea.
Kuhusu ununuzi wa chakula, Pinda alisema serikali itahakikisha kunawepo na akiba ya kutosha ya upungufu ambapo hadi Juni 30, 2011, NFRA ulikuwa na akiba ya tani 154,506 za mahindi na tani 1.96 za mtama.
Alifafanua kuwa Wakala umelenga kununua tani 200,000 za mahindi katika kipindi cha msimu wa mwaka 2011/2012 ambapo alisema hadi kufikia Oktoba, 2011 jumla ya tani 114,117 zilikuwa zimenunuliwa kutoka mikoa iliyozalisha ziada ya chakula.
Ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa fedha za kununulia chakula, serikali imeiruhusu NFRA kukopa Sh.bilioni 20 kutoka katika mabenki ya biashara nchini na kwamba mazungumzo yanaendelea.
Alisema pamoja na hatua hiyo, serikali pia imeiruhusu NFRA kuuza mahindi tani 50,000 kwa Shirika la Chakula Duniani (WFP), ambapo tayari tani 10,000 zimenunuliwa pamoja na kuuza tani 40,000 kwa wafanyabiashara binafsi.
Alionya kundi la walanguzi wa mbegu za pamba katika wilaya za Bariadi, Maswa, Magu, Meatu na Kishapu ambao wanapita Vijijini wakizinunua kwa kuwapa bei kubwa.
Alisema serikali imepokea majina ya walanguzi hao katika wilaya za Meatu, Bukombe, Bariadi, Bunda, Magu na Kishapu na operesheni ya kuwakamata inaendelea.
Kuhusu tatizo la ajira, Pinda aliliambia bunge kuwa ni baya kwa mustakabali wa nchi na kwamba linachangia kwa kiasi kikubwa umaskini nchini kwani yeyote asiyekuwa na kazi hana kipato.
Alisema watu wasio na ajira ni rahisi kujikuta wanaishi kwa njia zisizokubalika katika jamii zikiwemo za wizi, unyanganyi, biashara za ngono, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na uhalifu.
Alifafanua kuwa katika mwaka 2000, kiwango cha ukosefu wa ajira nchini kilikuwa asilimia 12.9 na kwamba matokeo ya utafiti wa nguvu kazi na ajira ya mwaka 2006 ilikuwa watu milioni 18.8 na kati ya hao milioni 2.2 walikuwa hawana ajira sawa na asilimia 11.7 ya nguvu kazi yote nchini.
Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini katika mwaka 2011 ni asilimia 10.7 ya nguvu kazi ya taifa ya watu milioni 22.2 ambapo alisema inakadiriwa kuwa idadi ya watu wasiokuwa na ajira kwa sasa ni milioni 2.4.
Kwa upande wa vitambulisho vy taifa, Pinda alisema vinatarajiwa kuanza kutolewa mapema mwaka 2012 baada ya taratibu zote kukamilika.
Alisema vitambulisho vya kwanza vitaanza kutolewa kuanzia mwezi Aprili 2012, wakati wa maadhimisho ya sherehe za muungano.
Kuhusu maandalizi ya sensa ya watu, Pinda alisema itafanyika mwezi Agosti 2012 ambayo itakuwa ya tano tangu nchi ilipopata uhuru wake 1961.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Mtazamo:
Kweli hatuna wabunge wala mawaziri jamani vipaumbele katika uchumi wetu ni semina kwa wabunge au uchumi imara? This is just another excuse ya kutafuna kodi zetu kama wabunge hawafahamu nini kinaendelea duniani wanunue magazeti ya Financial Times, Wall Street Journal na The Economist. Wanashindwa nini kutoa Tshs 20,000- Tshs 30,000 kila siku kununua magazeti hayo pale maeneo ya posta mpya pembezoni mwa askari monument na kwengineko Dar-es-Salaam ? Lazima wapatiwe semina halafu walipwe per diem yaani nchi kweli sisi hatuna vipaumbele hata kidogo!!!