Pinda amuagiza Gavana kuandaa semina ya wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda amuagiza Gavana kuandaa semina ya wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Nov 20, 2011.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Na Richard Makore  20th November 2011


  [​IMG]
  B-pepe  [​IMG]
  Chapa  [​IMG]
  Maoni
  [​IMG]
  Gavana wa Benki Kuu, Profesa Beno Ndulu


  Serikali imemuagiza Gavana wa Benki Kuu, Profesa Beno Ndulu kuandaa Semina kwa ajili ya wabunge ili kuwapa elimu juu ya mdodoro wa uchumi unaolikumba taifa hivi sasa.
  Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akiahirisha bunge ambapo alisema wabunge watapata fursa ya kujadili kwa kina hali ilivyo ya mwenendo wa viashiria vya uchumi, athari zake kwa nchi pamoja na hatua zinazochukuliwa na serikali.
  Alisema semina hiyo itafanyika katika mkutano wa sita wa bunge utakaoanza mwezi Januari mwaka 2012 ambapo wabunge wote watapata fursa ya kushiriki na kutoa michango yao.
  Kuhusu mchakato wa maandalizi ya mabadiliko ya katiba, Pinda alisema anaamini kwamba maelezo yaliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete juzi kupitia hotuba yake yatatoa uelewa na hivyo kuwafanya Watanzania kushiriki katika mchakato huo.
  Alisema muswada wa kuunda tume ya kuratibu maoni ya kuandika katiba mpya ulisimamiwa vizuri na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria na kwamba ilifanya kazi nzuri na ambayo imeonyesha njia.
  Aliwataka wananchi kutekeleza maelekezo ya Rais Kikwete kuhusu kushiriki katika hatua mbalimbali zinazofuata baada ya muswada huo kupitishwa na bunge ili mwisho wa siku katiba mpya iweze kuandikwa.
  Aliwataka Watanzania wote kuungana kwa pamoja na kutekeleza hatua itakayofuata ambayo ni kutoa maoni yao kwa Tume itakayoundwa na Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein.
  Aliwaomba viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa kupongeza hatua iliyofikiwa na kukubali muswada huo ambao tayari umepitishwa kwa maslahi ya taifa.
  Alitoa wito kwa wananchi wote vikiwemo vyama vya siasa kuungana kwa pamoja katika hatua muhimu inayokuja ambayo itahusisha watanzania wote ya kutoa maoni ya katiba wanayoitaka.
  Aliwasihi wananchi kuzingatia yale yote aliyoyasema Rais Kikwete katika hotuba yake ili hatua zote za kuelekea katiba mpya ziweze kufanyika kwa amani na utulivu wa Nchi yetu.
  Aidha, Pinda alimpongeza Spika wa Bunge kwa namna alivyoongoza mijadala mbalimbali iliyoibuka bungeni.
  Kuhusu hali ya chakula nchini, Pinda alisema, nchi imekuwa ikikabiliwa na hali ya ukame wa mara kwa mara kwa muda mrefu tangu mwaka 2006 hali ambayo imesababisha upungufu wa Chakula katika baadhi ya Mikoa ambayo imekuwa ikiathirika zaidi na ukame.
  Hata hivyo, Pinda alisema chakula ambacho kimekuwa kikizalishwa katika maeneo yenye mvua za kutosha kimewezesha nchi kuendelea kujitosheleza kwa kiwango kikubwa. Alitoa mfano, katika mwaka 2010/2011 uzalishaji wa mazao ya chakula unakadiriwa kufikia tani milioni 12.81 ikilinganishwa na mahitaji ya jumla ya tani milioni 11.50 za chakula kwa mwaka 2011/2012.
  Alisema uzalishaji huo unatosheleza mahitaji ya chakula kwa asilimia 111, sawa na ziada ya tani milioni 1.31 na kuongeza kuwa ziada hiyo inatokana na mazao yasiyo ya nafaka. Alisema uhaba wa nafaka ni kiasi cha tani 410,000 kwa nchi nzima na upungufu huo upo zaidi kwenye baadhi ya mikoa inayokabiliwa na ukame.
  Pinda alisema tathmini ya kina ya hali ya chakula na lishe nchini iliyofanywa mwezi Agosti na Septemba 2011, inaonesha kuwepo kwa jumla ya watu 1,062,516 katika Wilaya 52 za Mikoa 15 wanaokabiliwa na upungufu wa chakula (Acute Food Insecurity) kwa viwango mbalimbali.
  Wananchi hao wanahitaji tani 38,843 za chakula cha msaada kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2011.
  Waziri Mkuu alisema, hadi Oktoba 31, jumla ya tani 13,905 za chakula zilikuwa zimechukuliwa kutoka maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na kusambazwa katika maeneo hayo yenye uhaba wa chakula na kwamba kazi hiyo inaendelea.
  Kuhusu ununuzi wa chakula, Pinda alisema serikali itahakikisha kunawepo na akiba ya kutosha ya upungufu ambapo hadi Juni 30, 2011, NFRA ulikuwa na akiba ya tani 154,506 za mahindi na tani 1.96 za mtama.
  Alifafanua kuwa Wakala umelenga kununua tani 200,000 za mahindi katika kipindi cha msimu wa mwaka 2011/2012 ambapo alisema hadi kufikia Oktoba, 2011 jumla ya tani 114,117 zilikuwa zimenunuliwa kutoka mikoa iliyozalisha ziada ya chakula.
  Ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa fedha za kununulia chakula, serikali imeiruhusu NFRA kukopa Sh.bilioni 20 kutoka katika mabenki ya biashara nchini na kwamba mazungumzo yanaendelea.
  Alisema pamoja na hatua hiyo, serikali pia imeiruhusu NFRA kuuza mahindi tani 50,000 kwa Shirika la Chakula Duniani (WFP), ambapo tayari tani 10,000 zimenunuliwa pamoja na kuuza tani 40,000 kwa wafanyabiashara binafsi.
  Alionya kundi la walanguzi wa mbegu za pamba katika wilaya za Bariadi, Maswa, Magu, Meatu na Kishapu ambao wanapita Vijijini wakizinunua kwa kuwapa bei kubwa.
  Alisema serikali imepokea majina ya walanguzi hao katika wilaya za Meatu, Bukombe, Bariadi, Bunda, Magu na Kishapu na operesheni ya kuwakamata inaendelea.
  Kuhusu tatizo la ajira, Pinda aliliambia bunge kuwa ni baya kwa mustakabali wa nchi na kwamba linachangia kwa kiasi kikubwa umaskini nchini kwani yeyote asiyekuwa na kazi hana kipato.
  Alisema watu wasio na ajira ni rahisi kujikuta wanaishi kwa njia zisizokubalika katika jamii zikiwemo za wizi, unyangÂ’anyi, biashara za ngono, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na uhalifu.
  Alifafanua kuwa katika mwaka 2000, kiwango cha ukosefu wa ajira nchini kilikuwa asilimia 12.9 na kwamba matokeo ya utafiti wa nguvu kazi na ajira ya mwaka 2006 ilikuwa watu milioni 18.8 na kati ya hao milioni 2.2 walikuwa hawana ajira sawa na asilimia 11.7 ya nguvu kazi yote nchini.
  Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini katika mwaka 2011 ni asilimia 10.7 ya nguvu kazi ya taifa ya watu milioni 22.2 ambapo alisema inakadiriwa kuwa idadi ya watu wasiokuwa na ajira kwa sasa ni milioni 2.4.
  Kwa upande wa vitambulisho vy taifa, Pinda alisema vinatarajiwa kuanza kutolewa mapema mwaka 2012 baada ya taratibu zote kukamilika.
  Alisema vitambulisho vya kwanza vitaanza kutolewa kuanzia mwezi Aprili 2012, wakati wa maadhimisho ya sherehe za muungano.
  Kuhusu maandalizi ya sensa ya watu, Pinda alisema itafanyika mwezi Agosti 2012 ambayo itakuwa ya tano tangu nchi ilipopata uhuru wake 1961.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

  Mtazamo:

  Kweli hatuna wabunge wala mawaziri jamani vipaumbele katika uchumi wetu ni semina kwa wabunge au uchumi imara? This is just another excuse ya kutafuna kodi zetu kama wabunge hawafahamu nini kinaendelea duniani wanunue magazeti ya Financial Times, Wall Street Journal na The Economist. Wanashindwa nini kutoa Tshs 20,000- Tshs 30,000 kila siku kununua magazeti hayo pale maeneo ya posta mpya pembezoni mwa askari monument na kwengineko Dar-es-Salaam ? Lazima wapatiwe semina halafu walipwe per diem yaani nchi kweli sisi hatuna vipaumbele hata kidogo!!!
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii ni fedheha kwa watanzania. Uchumi unayumba, shilingi imepoteza thamani badala ya wabunge kuwakewa kiti moto Gavana wa bank kuu na waziri wa fedha waeleze wanafanya nini Waziri mkuu anataka wabunge wapewe darasa? (semina ni darasa). Hivi Zitto ambaye ni waziri kuvuli anahitaji kufundishwa nini? Tumechagua wabunge ili waende kujifunza au wafanye kazi? Nchi hii ni lini tutakuwa na viongozi?
   
 3. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mtazamo wa viongozi wetu si elimu, ni kuongeza mianya ya kupata kipato zaidi. Watu makini wanafuatilia wenyewe masuala ya uchumi na fedha ya kimataifa, hawahitaji kuelekezwa yaliko magazeti/majarida na wala web links za kupata taarifa hizo.
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  another misuse of government revenues
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  I always said kuwa the wabunge ni white elephants na ni mzigo kuwa maintain na kuwa entertain hawa wadudu, pretty useless.
   
 6. l

  laun Senior Member

  #6
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Semina=poshooo,per diem,sitting allowance
  Hii nchi imenona kweli,kuna mdororo wa uchumi halafu bado mabilioni yanaenda kwenye shimiwi,miaka hamsini ya uhuru ,mwenge na upupu mwingine mwiiingi unaowasha........
   
 7. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Shilingi haitasimamam na kuwa imara wakati tumeamua kutumia dollar ya kimarekani ndani ya nchi yetu. Hata mataifa makubwa kama USA, UK, hayakubali kutumia currency nyingine nchini mwao. Kazi ya Pinda imekuwa kuwalinda mafisadi yanayoongozwa na Fisadi papa.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Posho mil 4 Magamba kiboko
   
 9. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...wabunge tena!?,kwa nini asiende kuongea na wazee wa dar?...
   
 10. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Sasa bunge letu lina kamati ya fedha, uchumi na mipango kama sikosei je inafanya kazi gani?

  Halafu viashiria uchumi Tanzania ni vipi na vimekuwepo tokea lini?

  Je, soko la ajira na ujasirimali vimekaaje mpaka watu asilimia 2.2 (nina shaka na takwimu hizi) wanakuwa hadi leo hii hawana ajira?

  Na mwisho ni kwamba, kwa kuwa hakuna kumbukumbu za takwimu zinazoeleweka kutokana na hizo sensa zinazofanywa ambazo lengo lake ni kufahamu idadi ya watu ili kuwianisha mipango ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu ya kutosha na huduma za jamii, zoezi la kutoa vitambulisho limechelewa sana kwani eneo la uhamiaji kuna tatizo kubwa sana.
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mie naona labda wabunge wetu hawajui wapi taarifa zinapatikana tunawashauri wasome magazeti ya dunia na kusave pesa za semina ziende katika kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali. Badala yake wanazidisha gharama ya matumizi ya serikali kwa kutenga semina ya kitu ambacho utakipata katika magazeti na internet. Watenge 20,000-30,000 ya kununua magazeti kila siku. Na vile wasome katika internet kufahamu kitu gani kinaendelea.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,545
  Likes Received: 81,981
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa mara nyingine tena Pinda kakurupuka na kutoa kauli ambayo haina kichwa wala miguu. Sijui hii semina itawasaidia vipi Wabunge katika ushiriki wao wa mijadala kule Bungeni. Mie huyu Ndullu alinimaliza nguvu kabisa aliposema kwamba kutoa rangi kwa noti mpya ni kuonyesha kwamba ziko more durable.
   
 13. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kaswali ka kizushi:

  BOT wana budget item kwa ajili ya semina hiyo?
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Jibu ni ndiyo. Na wabunge wanataka nao wazitafune kidogo.
   
 15. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #15
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kumbe tuna tatizo kubwa zaidi la ku-set priorities.
   
 16. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #16
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Let's face it. Wabunge wetu wengi ni mbumbumbu na haya masuala ya uchumi umekuwa ni mwiba mchungu kwa wabunge wengi ambao uelewa wao ni mdogo sana. Mimi nafikiri wanahitaji kuelewa matatizo yaliyopo, chanzo chake na changamoto zilizopo katika kuyatatua. Gavana ana uwezo mkubwa sana wa kulifanya hilo kutokana na uelewa wake na hata uzoefu wake kama profesa wa muda mrefu.
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ok mkuu,

  So you think a seminar of a week kwa wabunge will help to ease umbumbu wao wa masuala ya uchumi? Since when kazi ya gavana imebadilika kutoka kuwa msimamizi wa pesa zetu na uchumi wetu kuwa professa wa darasani? Ulishamuona Ben Benarke anatoa semina kwa wabunge wa congress? Au gavana Mervyn King anawafundisha wabunge wa commons? Au Mario Draghi wa ECB akitoa darasa kwa wabunge wa EU? Hao wote ni maprofessa wanaoheshimika duniani kwenye uchumi lakini sijawahi kuwaona wakitoa seminar kwa law makers (wabunge) katika nchi zao.

  Mie naona tunakosa vipaumbele badala ya wabunge kumpa kiti moto waziri na gavana ndani ya bunge ikawepo katika hansard ya bunge sisi tunakimbilia seminar ambapo baada ya semina maswali na majibu yote yanatupiliwa katika dust bin na hakuna mabadiliko yeyote yatakayofanyika. Kama wabunge wanajiona wao mbumbumbu kuna short course za uchumi au waingie darasani part time kujiendeleza katika vyuo vikuu mbali mbali nchini. Otherwise huu ni upotezaji wa pesa na kujitengenezea miradi ya pesa hakuna lengine.
   
 18. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #18
  Nov 21, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Kama mtoto wa bepari angekuwa na akili nzuri (bahati mbaya hana!) angewaagiza UDOM waandae programu maalumu ya mafunzo ya certificate ya masuala ya uchumi na fedha mida ya usiku kuanzia saa moja hadi saa nne kwa muda wa mwezi mmoja ili waishiwa wabonge wote watakiwe kuhudhuria na hatimaye wapewe mtihani. Atakayeshindwa arudie tena darasa hadi wote wafuzu. Bwana Profesa Ndullu na wengineo wanaweza kuomba kazi ya kuwa wakufunzi wa darasa hilo. Potelea mbali hata Bibi Kiroboto akilipia hayo mafunzo. Atakayeshindwa mtihani wa mwisho pesa hizo zirejeshwe kwa kukata posho yake. Baada ya hapo hawa waishiwa wabonge watakuwa na uwezo wa kumweka kiti moto bwana profesa ndullu na waziri wa fedha na hiyo taarifa kurekodiwa katika hansard angaa kwa kufurahisha masikio yetu na kwa marejeo ya wajukuu wetu siku za usoni!!!!.:eyebrows:
   
 19. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #19
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sasa nimeamini kweli HII NCHI IMELAANIWA!Hivi semina kwa wabunge yawezakuwa kipaumbele katika kipindi hiki ambacho nchi inapita kwenye wakati mgumu hivi?Hivi hiyo semina si inatafuna hata hicho kidogo kilichopo?Tunaelekea wapi watanzania?
   
Loading...