MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amemshambulia Mbunge wa Kigoma Kaskazi Zitto Kabwe na kumtaka aache kuwapotosha wananchi kuwa, jitihada zake ndiyo zilizosababisha ujenzi wa barabara ya Kigoma.
Akitoa majumuisho ya bajeti ya Wizara yake kwa mwaka 2009/10 bungeni jana Pinda alisema, ujenzi wa barabara hiyo ulikuwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Alisema, CCM imefanya mambo mengi mazuri ingawa wapinzani hawataki kukubaliana na ukweli huo.
"Mheshimiwa Spika rafiki yangu Zitto Kabwe alijaribu kujigamba kuwa amefanya mambo huko Kigoma mapaka wamepata barabara, lakini nilikwenda huko jimboni kwake na kuzunguka kote na kuwaahidi wananchi ujenzi wa barabara hiyo"alisema Pinda na kuongeza:
"Mheshimiwa Spika ujenzi wa barabara ya Kigoma ni mpango wa muda mrefu wa CCM na ulikuwa katika ilani yake ya uchaguzi." Pinda alisema, serikali ni ya chama tawala na fedha za barabara hiyo zimetolewa na serikali hiyohiyo.
"Mheshmiwa Spika labda niseme hivi serikali ni ya chama chetu, fedha ni za serikali ya CCM na barabara zinajengwa na CCM, labda mheshmiwa Zitto pamoja na Chadema yake wangeniambia tu, Waziri serikali yako imejitahidi sana"aliongeza Waziri Mkuu.
Pinda alisema, alitegemea Zitto angekiri kuwa serikali ya CCM imempa barabara bila ya kuonesha ubaguzi wa kiitikadi za kisiasa pamoja na kwamba Zitto ni wa chama kingine siasa.
Wakati huohuo Waziri Pinda aliahidi kuendelea kutumia upole katika kazi zake ili kuongeza tija katika ufanisi wa serikali.
"Mheshimiwa Spika wabunge wamenitaka kupunguza upole, lakini upole na ukali una karama zake nao, hivyo mimi nitaendelea kuwa mpole katika kazi zangu ili kuhakikisha kuwa ufanisi wa serikali unaongezeka na kuwa na tija kwa wananchi," alisema.
Habari hii imeandaliwa na Jackson Odoyo na Salim Said Mwisho.
Source: Mwananchi Read News