Pinda aitia kitanzini CCM

Mh: Pinda hana tatizo namimi namuunga mkono kama wanataka utoke wakufukuze tu..... tatizo ni mfumo wautawala waziri mkuu hana meno na ambayo anayo ni kwa baadhi ya mawaziri na makatibu wa kuu coz kunawengine UNTOUCHABLE ...... baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu, wakuu wa mkoa , wakuu wa wilaya , wakurugenzi and the list goes on and on.. uteuzi wao umesukumwa na urafiki au undugu na Mkuu na kwa hili Mh:pinda hawezi kuwawajibisha ipasavyo..... sina wasiwasi na uwezo, uzoefu na uelewa wa uongozi aliyonao Mh Pinda
 
mfumo unamaanisha kama hao viongozi wawili wana maelewano mazuri na wanakubaliana katika kutekeleza maamuzi then utaona utendaji kazi wa waziri mkuu ila kama rais hayuko tayari kumpa back up waziri mkuu haswa katika maamuzi ya msingi utamuona waziri mkuu km sio mtendaji.
Mfumo unatakiwa umpe pm executive powers ili ahukumiwe kwa maamuzi yake kama mtendaji na sio kiranja.
nimekuelewa mkuu,kumbe tatizo si mfumo, tatizo ni mkuu wa nchi.lakini mbona katiba ya nchi inampatia madaraka ya kutosha waziri mkuu kutenda kazi kwa uhuru wa kutosha
 
nimekuwa nikipata tabu kuelewa kila ninaposikia "tatizo ni mfumo".naomba unisaidie mfumo unasababisheje mtu kama pinda asitekeleze majukumu yake vema.wakati wa sokoine mfumo ulikuwaje hadi akaweza kuwajibika ipasavyo.

mfumo uliopi wa kiutawala si huru ukiteuliwa unawekewa mipaka ya maamuzi.na kabla hujateuliwa unaambiwa ukubaliane kuwa inferior kwa waliokuteua.mfumo kana huo hata kama ni mchapa kazi utadhoofishwa tu.wakati wa sokonne mfumo ulikuwa wa uwajibikaji.nyerere aliwapa mawaziri meno ya kuamua na kuwajibisha.mfumo wa leo rushwa ni haki ya msingi ndani ya ccyenu.kama una dkdk nitarudi.
 
Akuambie wewe kama nani? Au kuna siku umeuliza ni hatua gani zilizochukuliwa kushughulikiamwavivu hao? Ukweli unabaki palepale kuwa kuna wanafiki wengi ambao wanajifanya wana uchungu sana na nchi hii. Hao hao ndo wanaongoza kwa kutowajibika kwa familiamzao. Kutwa wanashinda kwenya baa wakati watoto wao wanakosa karo.
Sijasema aniambie mimi. na kama kweli anawashughulikia basi angewaambia wabunge wanaotaka kumwajibisha. Sisi ni spectators tu. By the way kushindwa au kuweza kuwajibika kwenye familia haina uhusiano na uchungu wa nchi. Mafisadi wanafanikiwa kwa hili kwa ajili ya economic power not because they are good of doing that. Hao unaowasema wanashinda kwenye baa inawezekana ni matokeo ya kuwa frustrated na mfumo wa kifisadi wa Tanzania. Wewe unayetetea inaonekana unabenefit in a way .............. na unajitahidi kutetea maslahi tu!!
 
Mtu akishasema kitu ni kigimu maana kashindwa. Hata hao walimu tayari ugumu tunauona kwenye matoke siyo mpaka waache ndo ugundue ugumu. Vipi daktari kupasua kichwa badala ya mguu siyo ugumu kuelekea kwenye kushindwa?

Msimtetee pinda kweli kazi imemshinda na inabidi aache mwingine aingie, bora tuingie kazi ya kumtunza kuliko hasara anayotuingizia kwa sasa.
sure mkuu hata madakatari na walimu kila siku tunasikia wanasema kazi zao ni ngumu zinahitaji witto lakini siyo kama wameshindwa kufanya kazi.
 
PINDA ni wa ajabu ameshindwa kujua kazi ya uwaziri mkuu sio mzigo ila uwezo wake ndo mdogo??? MaPM wangapi wamepita mbona hawakuhi kusema uPM ni mzigo???
 
nimekuwa nikipata tabu kuelewa kila ninaposikia "tatizo ni mfumo".naomba unisaidie mfumo unasababisheje mtu kama pinda asitekeleze majukumu yake vema.wakati wa sokoine mfumo ulikuwaje hadi akaweza kuwajibika ipasavyo.

Majukumu unayatekeleza kama unayo mamlaka ya kumwajibisha aliye chini yako.
Kikatiba mfumo wetu uko hivi, Waziri au Katibu Mkuu au Mkurugenzi akivurunda Waziri Mkuu hana uwezo wa kumwadabisha
Ni lazima waziri Mkuu ashitaki kwa Rais. ( Unajua wote hawa ni wateule wa Rais)
Pinda angekuwa na mamlaka ya kuwateua mambo yasingekuwa kama ilivyo sasa.

Utasema mbona Sokoine alikuwa anafanya tofauti ? Ni kwamba zile enzi Kiongozi mkuu wa nchi (Nyerere) alikuwa hana mzaa na watu wavivu, kama ungempelekea mtendaji aliye chini yako au hata juu yako kimamlaka anaboronga , anachukua hatua mara moja.

Tunakumbuka amabavyo mawaziri walikuwa wanaweza kutimuliwa kazi hata na Makatibu wakuu , Kama mnakumbuka Mzee Mulokozi aliyekuwa Katibu Mkuu alivyokuwa anachapa waziri wake akipokuwa akiboronga kazi , waziri anaondolewa mara moja sio na waziri mkuu ni huyu mzee katibu mkuu, anapeleka ubovu wake kwa Rais.

Hizo enzi hazipo tena angalia swala la Jairo ( uteuzi wa kishikaji)
Kwa hiyo Sokoine alionekana nchapa kazi sababu bosi wake alikuwa mchapa kazi na hana mchezo na mtu.
Pinda anafanya kazi kwenye mazingira tofauti sana, huwezi kumpima utendaji wake kwa kuangalia wizara zilizo chini yake tu
 
Back
Top Bottom