Pinda aitia kitanzini CCM

ukiwa huna upeo huwezi kumwelewa pinda ila sisi tunaojua siasa tunamjua pinda anachofanya.
 
Pinda ni matokeo ya mfumo butu wa kisisasa ulioasisiwa na Chama Tawala.
Kwa mfumo huu mtu yeyote yule anaweza kuingia katika madaraka ya juu kwa maslahi na matakwa ya wanaoshikilia huo mfumo butu wa CCM ambao umeambukiza hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano!

Ubutu wa mfumo huu ndio huohuo unaowapa Ubunge wa Kugawiwa wateule wa Rais, wanaoungana na waliobebwa kwenye chaguzi huko majimboni kwenda kupitisha majina ya wachovu kama kina Pinda na kupitisha Katiba isiyo na maslahi kwa wananchi.

Ubutu wa nfumo wa CCM unaoshabikia Rais kuachiwa kuteua mawaziri mizigo ambao leo wanalaumiana wenyewe kwenye mikutano yao ya hadhara na vikao vya juu vinaitishwa kutafuta nusuru kwa athari tokana na udhaifu wa viongozi waliowekwa madarakani pasipo kuzingatia uwezo wala sifa, zaidi ya kujua kuimba sana, kushangilia kwa sauti, na kutumia pesa!

Acheni unafiki wenu Pinda anapokiri kuwa kazi ni ngumu anadhihirisha ubovu wa mfumo butu huo ulioasisiwa na CCM, na ndio maana anafanya kazi katika mazingira ya MIZENGWE iliyo PINDA!
 
jamani hili.swala la waziri mkuu. kusema yuko tiari kuachia ngazi mnaonaje. naleta kwenu wana jf

mkuu kama hujaweza kuilewa hii kauri ya pinda basi siasa huijui undani wake pinda ni mwanasiasa anayejua pakuingilia na pakutokea.
 
wewe ulichandika ni sawa kulingana na upeo wako,

ila sisi wenye upeo mpana zaidi yako tunasema tatizo siyo pinda. tatizo ni mfumo mzima wa utawala mbove ambao tunaupigia kelele kila siku, na mpaka sasa bado tupo kwenye mchakato wa kuubadlisha kupitia KATIBA MPYA

pinda anateuliwa tu hana meno kikatiba ya kungata mpaka aombe ruhusa kwa bosi wake, kama bosi hataki yeye atafanya nini?

kwa katiba tuliyo nayo waziri mkuu ni kama kiranja tu. hawezi kumwadhibu mwanafunzi , labda kumripoti kwa mwalimu mkuu yeye ndo atoe adhabu

kila mara tunapowaambia watawala kwamba katiba ni mbovu hawasikii, maneno ya pinda yanadhiirisha umuhimu wa katiba nzuri yeneye mifumo, na vyombo, taassisi imara za utawala, vinginevyo pinda ni mbuzi wa kafara

Na wewe ulichoandika kwa upeo wako unaona ni sahihi kuwa matatizo ya nchi hii yanatokana na katiba na tukibadilisha katiba tu tutaondoa matatizo haya, unachosahau au ambacho haukijui ni kuwa kuna nchi zinaendeshwa bila katiba na zimepiga mafanikio makubwa sana, kingine ambacho umesahau ni kuwa Nyerere aliongoza nchi hii kwa katiba hii hii na kuna matatizo lukuki ambayo yapo saa hizi hayakuwepo kipindi cha utawala wake, kilichomuangusha ni ile imani yake kuwa ujamaa ungeleta maendeleo.

Nchi zetu hizi za kiafrika Rais wa nchi ni kila kitu wengine ni label tu, rais akiwa na dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wake hakuna kinachoshindikana iwe ni sheria au taasisi itabadilishwa within 24hrs. Nikuulizwe swali fupi tu kukazia hii point; kwani katiba ya sasa inasemaje kuhusu mtu au kikundi cha watu kikipanga njama na kuiba kwenye akaunti ya madeni ya nje (EPA) pale BOT? wakithibitika wameiba hiyo hela kwa udanganyifu, Raisi anaruhusiwa kuwasamehe kabla ya kufikishwa mahakamani? Ukijibu vizuri hilo swali utajua tatizo liko wapi. TATIZO TUNALO MWAKA WA NANE HUU NA LITAONDOKA AU KUPUNGUA AU KUONGEZEKA 2015.
 
acha ujinga wewe mbona wizara ya TAMISEMI ndo inayoongoza kwa uozo na ipo ofisini kwako.
Tatizo la wwtanzania ni unafiki. Yaani huyu mleta uzi kaangalia yale yampendezayo tu kati ya mambo mengi aliyoongea Pinda jana. Kwani si kweli kwamba kazi ya uwaziri mkuu si ya kuomba? Kwani si kweli kwamba wabunge wanaweza kumuondoa waziri mkuu wakiona kuwa hafai? Sasa mbona hawamuondoi? Alichosema Pinda jana namuunga mkono. Kwamba ikiwa wizara moja inalegalega, huwezi kusema kuwa waziri Mkuu hawajibiki au ameshindwa kuisimamia. Hivi hata katika familia zetu, haijitokezi kuwa na mtoto mtukutu na asiyependa shule licha ya juhudi za wazazi?
 
Pinda ni matokeo ya mfumo butu wa kisisasa ulioasisiwa na Chama Tawala.
Kwa mfumo huu mtu yeyote yule anaweza kuingia katika madaraka ya juu kwa maslahi na matakwa ya wanaoshikilia huo mfumo butu wa CCM ambao umeambukiza hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano!

Ubutu wa mfumo huu ndio huohuo unaowapa Ubunge wa Kugawiwa wateule wa Rais, wanaoungana na waliobebwa kwenye chaguzi huko majimboni kwenda kupitisha majina ya wachovu kama kina Pinda na kupitisha Katiba isiyo na maslahi kwa wananchi.

Ubutu wa nfumo wa CCM unaoshabikia Rais kuachiwa kuteua mawaziri mizigo ambao leo wanalaumiana wenyewe kwenye mikutano yao ya hadhara na vikao vya juu vinaitishwa kutafuta nusuru kwa athari tokana na udhaifu wa viongozi waliowekwa madarakani pasipo kuzingatia uwezo wala sifa, zaidi ya kujua kuimba sana, kushangilia kwa sauti, na kutumia pesa!

Acheni unafiki wenu Pinda anapokiri kuwa kazi ni ngumu anadhihirisha ubovu wa mfumo butu huo ulioasisiwa na CCM, na ndio maana anafanya kazi katika mazingira ya MIZENGWE iliyo PINDA!
Kwani kukiri kuwa kazi ni ngumu ina maana nimkushindwa kazi? Mbona Mbowe amewahi kusema kuwa uenyekiti ni kazi ngumu, ina maana na yeye kazi imemshinda! Kama ndo hivyo, mbona anapambana na Zitto anayetaka nafasi hiyo?
 
acha ujinga wewe mbona wizara ya TAMISEMI ndo inayoongoza kwa uozo na ipo ofisini kwako.
Hujui kuwa TAMISEMI inabeba wizara za kisekta zote? Ndo inasimamia halmashauri zote ambazo zimejaa wakurugenzi waliowekwa na mafisadi akina Lowasa? Kwa hali hiyo unategemea kutakuwa na ufanisi? Watu wanafikiria kwibakwiba tu
 
nimekuwa nikipata tabu kuelewa kila ninaposikia "tatizo ni mfumo".naomba unisaidie mfumo unasababisheje mtu kama pinda asitekeleze majukumu yake vema.wakati wa sokoine mfumo ulikuwaje hadi akaweza kuwajibika ipasavyo.

Mfumo unamaanisha kama hao viongozi wawili wana maelewano mazuri na wanakubaliana katika kutekeleza maamuzi then utaona utendaji kazi wa waziri mkuu ila kama rais hayuko tayari kumpa back up waziri mkuu haswa katika maamuzi ya msingi utamuona waziri mkuu km sio mtendaji.
Mfumo unatakiwa umpe PM executive powers ili ahukumiwe kwa maamuzi yake kama mtendaji na sio kiranja.
 
acha ujinga wewe mbona wizara ya TAMISEMI ndo inayoongoza kwa uozo na ipo ofisini kwako.

Na wewe wa hovyo kweli unawezaje kuongea mambo jumlajumla kama litoto dogo unaposema uozo bila kuutaja au kuweka mfano wowote tunakuona huna kitu kichwani mwaka zaidi ya maji tu.
 
Kwani kukiri kuwa kazi ni ngumu ina maana nimkushindwa kazi? Mbona Mbowe amewahi kusema kuwa uenyekiti ni kazi ngumu, ina maana na yeye kazi imemshinda! Kama ndo hivyo, mbona anapambana na Zitto anayetaka nafasi hiyo?

sure mkuu hata madakatari na walimu kila siku tunasikia wanasema kazi zao ni ngumu zinahitaji witto lakini siyo kama wameshindwa kufanya kazi.
 
Tafadhali edit panaposomeka "maradhi"pasomeke "malazi" panaposomeka "ufahali" pasomeke "ufahari"

bila ku-edit hata wanaochangia watakuwa hawajui kuelewa.

Ana tatizo la kuchanganya L na R. Kujiuzulu anasema 'Kujiuzuru'. 'Kadharika' badala ya Kadhalika
 
nimekuwa nikipata tabu kuelewa kila ninaposikia "tatizo ni mfumo".naomba unisaidie mfumo unasababisheje mtu kama pinda asitekeleze majukumu yake vema.wakati wa sokoine mfumo ulikuwaje hadi akaweza kuwajibika ipasavyo.

Umeswema kweli Mkuu! Katika mfumo unaomfanya pinda ashindwe, Mwakyembe na maghufuli wamewezaje? Pinda ni dhaifu tu, tena dhaifu kuliko bosi wake!!
 
Ndo wizara yake ainyooshe isiwe na madudu ili akituambia anasimamia wizara nyingi tumuelewe.Kama TAMISEMI imemshinda apige chini hana mpya manake akizongwa sana hatachelewakutoa machozi.
Hujui kuwa TAMISEMI inabeba wizara za kisekta zote? Ndo inasimamia halmashauri zote ambazo zimejaa wakurugenzi waliowekwa na mafisadi akina Lowasa? Kwa hali hiyo unategemea kutakuwa na ufanisi? Watu wanafikiria kwibakwiba tu
 
Hivi lowasa anaweza kuweka wakurugenzi akiwa nje ya ulingi ? hii ni akiri ya wapi mkuu.Kwahiyo wanapochagua wakurugenzi EDDO ndo anayewapendekezaeeee !!!!!!!
Hujui kuwa TAMISEMI inabeba wizara za kisekta zote? Ndo inasimamia halmashauri zote ambazo zimejaa wakurugenzi waliowekwa na mafisadi akina Lowasa? Kwa hali hiyo unategemea kutakuwa na ufanisi? Watu wanafikiria kwibakwiba tu
 
Kwani kukiri kuwa kazi ni ngumu ina maana nimkushindwa kazi? Mbona Mbowe amewahi kusema kuwa uenyekiti ni kazi ngumu, ina maana na yeye kazi imemshinda! Kama ndo hivyo, mbona anapambana na Zitto anayetaka nafasi hiyo?
Soma kati ya mistari....Pinda hajakiri kushindwa kazi.. Bali amekiri kuwa kazi ni ngumu na kama utamwelewa, maneno yake yanaashiria mfumo uliopo ndio haumpi nguvu ya kurekebisha mambo moja kwa moja. Yeye hakuteua hao Mawaziri mnaowaita leo mizigo na wala hawezi kuwaondoa kwa maamuzi yake. Ubovu wa mfumo butu wa CCM ndio kiini cha yote haya....kazi kwenu!
 
Uongozi muda mwingine bora kuwapa matajiri au watu wa level ya kati, kuwapa watu wa level ya chini ni nuksi tu, kama mtu kashindwa kujichomoa yeye mwenyewe kwenye umaskini utampa atoe taifa zima kwenye umaskini unadhani ni kazi rahisi kiac hicho. Nchi za watu wanaoshikiria ni wenye hela, hata wakijiendeleza, wanaendeleza nchi pia kinaonekana vizuri.. Bongo maskini kujijaza bungeni wakipata hela wanazirukiarukia tu wanaona wamefika.. Sawa na kumtoa house gal village ukamleta town, akishaona TV mwezi moja tu tayari, kushnehi afu akipata mimba anarudi zero...
 
Back
Top Bottom