Pinda aitia kitanzini CCM

Maseto

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
913
500
Sasa naamini sikio la kufa halisikii dawa kwa CCM.Walianza akina Nape na Kinana kuwataja mawaziri mizigo lakini jina la Pinda halikuwemo.Wabunge wakamtaja Pinda kuwa ndiye mzigo mzito mno kubebeka.

Jana Pinda ndiyo kaiharibia zaidi CCM kwa kusema kazi ya uwaziri mkuu hakuiomba na ni ngumu mno,akasema kama wakiona inafaa wakamtoa atafurahi.

Hapa kimantiki alimaanisha kuwa;

1.yeye hayuko tayari kujiuzuru,
2. Hayuko tayari kujirekebisha ili aongeze ufanisi,
3. Uwezo wake ndiyo umegota hapo,hana ziada ya uwezo wa utendaji.
4. Ameridhika na kiwango chake cha utendaji na anaona wanaosema hafanyi vizuri wanamuonea.

Ieleweke kuwa kwa nchi masikini kama hii,mtu anapopewa cheo maana yake ni kwa ajili ya kujikimu yeye,familia yake na ndugu siyo kwa ajili ya kutumikia wananchi wake.

Hapa ni vema tukakumbuka nadharia ya Abraham Maslow ambayo inaelezea kuwa mahitaji ya binadamu hujipanga kwa muundo wa piramidi,chini huanza mahitaji ya msingi kama vile chakula,mavazi na malazi.Baada ya kukidhi mahitaji ya msingi binadamu huhitaji yasiyo ya lazima sana kama vile ulinzi,starahe na kadharika na hatimaye binadamu hufikia kilele cha mahitaji kwa kuhitaji ufahari wa kujulikana,kuenziwa na kutukuzwa.Hapo ndipo mtu hugombea vyeo vya kisiasa au kutoa misaada kwa watu wenye mahitaji ili atukuzwe.

Kwa maana hiyo Pinda ambaye alikuwa kachero tu ikulu pale anashukuru sana kuwezeshwa kujikimu maisha yake yote ndiyo maana anasema atafurahi akiondolewa kwa kuwa lengo lake litakuwa limetimia.

Swali la kujiuliza CCM watamuondoa?mimi nitashangaa akiondolewa kwa sababu moja kubwa;yeye ni kachero na wanaopendekeza kuondolewa kiongozi ni makachero wenzake ndani ya utawala.

Hata hivyo wasipomuondoa madhara kwa CCM ni makubwa sana kwa sababu amekiri mwenyewe kuwa hana uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu ya waziri mkuu.
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
8,392
2,000
wewe ulichandika ni sawa kulingana na upeo wako,

ila sisi wenye upeo mpana zaidi yako tunasema tatizo siyo pinda. tatizo ni mfumo mzima wa utawala mbove ambao tunaupigia kelele kila siku, na mpaka sasa bado tupo kwenye mchakato wa kuubadlisha kupitia KATIBA MPYA

pinda anateuliwa tu hana meno kikatiba ya kungata mpaka aombe ruhusa kwa bosi wake, kama bosi hataki yeye atafanya nini?

kwa katiba tuliyo nayo waziri mkuu ni kama kiranja tu. hawezi kumwadhibu mwanafunzi , labda kumripoti kwa mwalimu mkuu yeye ndo atoe adhabu

kila mara tunapowaambia watawala kwamba katiba ni mbovu hawasikii, maneno ya pinda yanadhiirisha umuhimu wa katiba nzuri yeneye mifumo, na vyombo, taassisi imara za utawala, vinginevyo pinda ni mbuzi wa kafara

Sasa naamini sikio la kufa halisikii dawa kwa ccm.walianza akina nape na kinana kuwataja mawaziri mizigo.lakini jina la pinda halikuwemo.wabunge wakamtaja pinda kuwa ndiye mzigo mzito mno kubebeka.
Jana pinda ndiyo kaiharibia zaidi ccm kwa kusema kazi ya uwaziri mkuu hakuiomba na ni ngumu mno.akasema kama wakiona inafaa wakamtoa atafurahi.
Hapa kimantiki alimaanisha kuwa;
1.yeye hayuko tayari kujiuzuru,
2. Hayuko tayari kujirekebisha ili aongeze ufanisi,
3. Uwezo wake ndiyo umegota hapo,hana ziada ya uwezo wa utendaji.
4. Ameridhika na kiwango chake cha utendaji na anaona wanaosema hafanyi vizuri wanamuonea.
Ieleweke kuwa kwa nchi masikini kama hii,mtu anapopewa cheo maana yake ni kwa ajili ya kujikimu yeye,familia yake na ndugu.siyo kwa ajili ya kutumikia wananchi wake.hapa ni vema tukakumbuka nadharia ya abraham maslow ambayo inaelezea kuwa mahitaji ya binadamu hujipanga kwa muundo wa piramidi.chini huanza mahitaji ya msingi kama vile chakula,mavazi na maradhi.baada ya kukidhi mahitaji ya msingi binadamu huhitaji yasiyo ya lazima sana kama vile ulinzi,starahe na kadharika.hatimaye binadamu hufikia kilele cha mahitaji kwa kuhitaji ufahali wa kujulikana,kuenziwa na kutukuzwa.hapo ndipo mtu hugombea vyeo vya kisiasa au kutoa misaada kwa watu wenye mahitaji ili atukuzwe.
Kwa maana hiyo pinda ambaye alikuwa kachero tu ikulu pale anashukuru sana kuwezeshwa kujikimu maisha yake yote.ndiyo maana anasema atafurahi akiondolewa kwa kuwa lengo lake litakuwa limetimia.
Swali la kujiuliza ccm watamuondoa?mimi nitashangaa akiondolewa kwa sababu moja kubwa;yeye ni kachero.na wanaopendekeza kuondolewa kiongozi ni makachero wenzake ndani ya utawala.
Hata hivyo wasipomuondoa madhara kwa ccm ni makubwa sana kwa sababu amekiri mwenyewe kuwa hana uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu ya waziri mkuu.
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
Tafadhali edit panaposomeka "maradhi"pasomeke "malazi" panaposomeka "ufahali" pasomeke "ufahari"

bila ku-edit hata wanaochangia watakuwa hawajui kuelewa.
 
Maseto

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
913
500
wewe ulichandika ni sawa kulingana na upeo wako,

ila sisi wenye upeo mpana zaidi yako tunasema tatizo siyo pinda. Tatizo ni mfumo mzima wa utawala mbove ambao tunaupigia kelele kila siku, na mpaka sasa bado tupo kwenye mchakato wa kuubadlisha kupitia katiba mpya

pinda anateuliwa tu hana meno kikatiba ya kungata mpaka aombe ruhusa kwa bosi wake, kama bosi hataki yeye atafanya nini?

Kwa katiba tuliyo nayo waziri mkuu ni kama kiranja tu. Hawezi kumwadhibu mwanafunzi , labda kumripoti kwa mwalimu mkuu yeye ndo atoe adhabu

kila mara tunapowaambia watawala kwamba katiba ni mbovu hawasikii, maneno ya pinda yanadhiirisha umuhimu wa katiba nzuri yeneye mifumo, na vyombo, taassisi imara za utawala, vinginevyo pinda ni mbuzi wa kafara

nimekuwa nikipata tabu kuelewa kila ninaposikia "tatizo ni mfumo".naomba unisaidie mfumo unasababisheje mtu kama pinda asitekeleze majukumu yake vema.wakati wa sokoine mfumo ulikuwaje hadi akaweza kuwajibika ipasavyo.
 
Maseto

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
913
500
Tafadhali edit panaposomeka "maradhi"pasomeke "malazi" panaposomeka "ufahali" pasomeke "ufahari"

bila ku-edit hata wanaochangia watakuwa hawajui kuelewa.
Mkuu,nakushukuru kwa masahihisho,nimetekeleza.
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,873
1,500
Bora wamuache tu huyo tumechoka wapigwe tu (Read Pinda).

Kuchagua WM mwingine mpya katika kipindi hiki kifupi kilichobaki kabla ya 2015, ni kujiongezea MZIGO sisi Watanzania walipa KODI masikini. Kumbuka hawa viongozi wakuu wa KITAIFA tunawadumia wao na familia zao maisha yao yote. Wanapata 80% ya salary ya current sitting PM, RAIS, VP, SPIKA, CJ etc plus marupurupu mengine kama ofisi, dereva, house maid, walinzi, matibu bure, kusafiri nje ya nchi at least mara 3 kwa mwaka bure, etc.

Therefore kumchagua WM mpya mwingine ni kuongeza idadi ya hawa viongozi wakuu wa Kitaifa. From economic point of view it is not COST EFEECTIVE. Bearing in mind that WM mpya atatoka huko huko CCM ambao ni mfumo ume prove beyond reasonable doubt it is UNEFFECTIVE. In a nutshelll WM mpya hakuna atakachobadilisha katika mfumo huu wa ki-CCM, CCM. Bora tubane matumizi kwa kutoongeza viongozi wakuu wa kitaifa wa kuwahudumia.
 
mwa 4

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,392
1,250
tatizo lenu bavicha mmezoea siasa za kuviziana na kumwagiana sumu siasa safi kamwe hamtaziweza ufafanuzi wa pinda ulikuwa mpana kama unaulewa mdogo huwezi kuambulia kitu.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,903
2,000
Tatizo la wwtanzania ni unafiki. Yaani huyu mleta uzi kaangalia yale yampendezayo tu kati ya mambo mengi aliyoongea Pinda jana. Kwani si kweli kwamba kazi ya uwaziri mkuu si ya kuomba? Kwani si kweli kwamba wabunge wanaweza kumuondoa waziri mkuu wakiona kuwa hafai? Sasa mbona hawamuondoi? Alichosema Pinda jana namuunga mkono. Kwamba ikiwa wizara moja inalegalega, huwezi kusema kuwa waziri Mkuu hawajibiki au ameshindwa kuisimamia. Hivi hata katika familia zetu, haijitokezi kuwa na mtoto mtukutu na asiyependa shule licha ya juhudi za wazazi?
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,903
2,000
mnafiki nani sasa aliyezomewa kigoma au anayebadili katiba ya chama ili awe kiongozi wa chadema wa milele?
Mkuu, yaani unanikumbusha aibu ya Dr Slaa kigoma. Pamoja na juhudi za ITV kuungaunga picha ili yao:rip:nekane mahudhurio mengi, bado wameumbuka na hakika huwezi kuamini kuwa huyu ndiye DR Slaa yule aliyekuwa anawakusanya watu 2010
 
mwa 4

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,392
1,250
nimekuwa nikipata tabu kuelewa kila ninaposikia "tatizo ni mfumo".naomba unisaidie mfumo unasababisheje mtu kama pinda asitekeleze majukumu yake vema.wakati wa sokoine mfumo ulikuwaje hadi akaweza kuwajibika ipasavyo.

nini ambacho pinda kashindwa kutekeleza siyo kuongea maneno matupu yasiyokuwa na maana.
 
Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
Mi huyu jamaa sasa hivi sitaki tena kumsema maana naona anaweza kumalizia hasira kwa mtu... hasa nikiwaza katokea huko karibia na sumbaWANGA..
 
mwa 4

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,392
1,250
Mkuu, yaani unanikumbusha aibu ya Dr Slaa kigoma. Pamoja na juhudi za ITV kuungaunga picha ili yao:rip:nekane mahudhurio mengi, bado wameumbuka na hakika huwezi kuamini kuwa huyu ndiye DR Slaa yule aliyekuwa anawakusanya watu 2010
mlinzi wa slaa aliipata mawe yalikuwa yanatua kwake moja kwa moja yeye ndiye alikuwa ngao ya slaa.
 
mwa 4

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,392
1,250
Mi huyu jamaa sasa hivi sitaki tena kumsema maana naona anaweza kumalizia hasira kwa mtu... hasa nikiwaza katokea huko karibia na sumbaWANGA..

haya mambo anayajua ben na bavicha wenzake pinda hausiki na haya mambo mabaya.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,903
2,000
Bora wamuache tu huyo tumechoka wapigwe tu (Read Pinda).

Kuchagua WM mwingine mpya katika kipindi hiki kifupi kilichobaki kabla ya 2015, ni kujiongezea MZIGO sisi Watanzania walipa KODI masikini. Kumbuka hawa viongozi wakuu wa KITAIFA tunawadumia wao na familia zao maisha yao yote. Wanapata 80% ya salary ya current sitting PM, RAIS, VP, SPIKA, CJ etc plus marupurupu mengine kama ofisi, dereva, house maid, walinzi, matibu bure, kusafiri nje ya nchi at least mara 3 kwa mwaka bure, etc.

Therefore kumchagua WM mpya mwingine ni kuongeza idadi ya hawa viongozi wakuu wa Kitaifa. From economic point of view it is not COST EFEECTIVE. Bearing in mind that WM mpya atatoka huko huko CCM ambao ni mfumo ume prove beyond reasonable doubt it is UNEFFECTIVE. In a nutshelll WM mpya hakuna atakachobadilisha katika mfumo huu wa ki-CCM, CCM. Bora tubane matumizi kwa kutoongeza viongozi wakuu wa kitaifa wa kuwahudumia.
Umenena mkuu. Si hayo tu bali pia Waziri Mkuu tuliyenaye anachapa kazi sana. Pia ni mtu mwenye huruma kwa watu. Hakika kama angetawala kama watakavyo hawa wambulu na wachaga, ni wazi kuwa image ya nchi hii ingeharibika kabisa kwa maana hakuna aliye msafi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom