Pilau Ya Kuku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pilau Ya Kuku

Discussion in 'JF Chef' started by X-PASTER, Jan 17, 2012.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160

  Pilau Ya Kuku

  Vipimo

  • Mchele wa basmati........................ 3 Vikombe
  • Kuku.............................................½
  • Viazi.............................................. 4
  • Vitunguu........................................ 2
  • Thomu iliyosagwa........................... 2 Vijiko vya supu
  • Binzari ya pilau nzima...................... 1 Kijiko cha chakula
  • Binzari ya pilau.................................½ kijiko cha chai
  • Pilipili manga nzima......................... ½ kijiko cha chai
  • Karafuu nzima................................. 8
  • Iliki nzima......................................... 6
  • Mdalasini nzima................................. 5 Vijiti
  • Pilipili mbichi iliyosagwa...................... 2
  • Chumvi............................................. Kiasi
  • Mafuta ya kupikia...............................¼ Kikombe

  Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
  1. Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
  2. Kata kuku vipande upendavyo, safisha kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu na tangawizi.
  3. Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria.
  4. Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi.
  5. Tia thomu na tangawizi na binzari zote kaanga kidogo
  6. Kisha tia viazi kanga kidogo kisha tia kisha tia vipande vyako vya kuku na supu acha ichemke kidogo kisha tia maji ukisie kutokana na mchele unaotumia.
  7. Mwisho tia mchele koroga uchanganye na vitu vyote acha ichemke kiasi kisha funika na punguza moto mpaka uive (huku ukiugeuzageuza)
  8. Ukishakuwa tayari pakua kwenye sahani tayari kwa kula na salad na pilipili.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,452
  Likes Received: 19,822
  Trophy Points: 280
  hii kitu nilikuwa naitafuta sana
   
Loading...