Pikipiki ipi nzuri kati ya boxer 150 na yamaha

Pikipiki ipi nzuri kati ya boxer 150 na yamaha

KISHINDO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
2,209
Reaction score
1,973
Habari zenu wapendwa!!!

Naomba msaada kati ya Boxer 150 na Yamaha ipi ni pikipiki nzuri ya kutembelea na si ya kufanyia biashara.

Kuna ndugu kachangaywa na wenye nazo alipowauliza, kila mmoja alivutia kwake so nikaona ni vyema nije kwa wataalamu wa vifaa hivyo.
 
Zote zinafaa, kikubwa ni kufikiria mtembeleaji anahitaji nini katika pikipiki, kama lengo lake ni kufukuzana barabarani basi anunue boxer, lkn kama lengo ni matumizi ya kawaida basi Yamaha Crux inamtosha. Kwa sababu zote zinakaribiana katika matumizi ya mafuta na bei za spares zake. Ila tofauti kubwa ni kwamba boxer imetulia barabarani kwa sababu ni nzito ila Yamaha Crux inapea kwa sababu haina uzito wa kutosha.
 
Ahsante sana Kisusi Mohammed kwa ufafanuzi wako mzuri.
 
Pia nitawezaje kutambua boxer original na ile isiyo original maana nasikia kuna za mchina.

Naombeni msaada kwa hilo.

Thanks
 
Pia nitawezaje kutambua boxer original na ile isiyo original maana nasikia kuna za mchina.

Naombeni msaada kwa hilo.

Thanks

dah wabongo bana... Kumbe ni wewe mwenyewe, sio tena 'ndugu aliyechanganywa' unanikumbsha habari ya ''kuna jamaa yangu anaomba ushauri ana uume mdogo''... Nway poa mazee, kula kitu cha SunLg.. Fuel friendly.. Achana na hizo proposal zako.. For the two go for Boxer..
 
Ni mimi ninayeomba ushauri ili nimpe huyo ndugu.

Thanks Sexologist kwa ushauri wako ila punguza mabango kijana
 
KISHINDO mkuu chukua boxer hutojutia yamaha ni nyepesi sana inahama barabaran ikiwa speed kidogo
 
Last edited by a moderator:
Ok, Ahsante sana Jambazi.

Ila punguza ujambazi maana unaweza kuuawa at any time.
 
Last edited by a moderator:
Kama kwa matumizi ya mizunguko yako tu chukua Platina 125 nayo ipo vizuri sana.
 
Yamaha DT cc125 bei yake si chini ya milioni 5. Ndo maana nyingi ni za serikali au taasisi fulani lkn sio mtu kumiliki. Yamaha ni mjapani. NB:huwezi linganisha yamaha na boxer hata siku moja.
 
Jamani mnaongelea Yamaha gani? Hii ya mjapani originali au kuna za fake za mchina
Kama ni Yamaha ninazo zijua mimi huwezi kulinganisha na michina ya boxer wala sunlg kuanzia ubora hadi bei
Ni watu binafsi wachache wanaweza nunua Yamaha ambayo ni bora kutafuta katoyota used mtaani
Kuanzia m5
 
Jamaa wa Boxer haoo.Ngoja nikimbilie benki nikatoe kisalio changu cha 139,999/= wasije wakapita nacho
 
Jamani mnaongelea Yamaha gani? Hii ya mjapani originali au kuna za fake za mchina
Kama ni Yamaha ninazo zijua mimi huwezi kulinganisha na michina ya boxer wala sunlg kuanzia ubora hadi bei
Ni watu binafsi wachache wanaweza nunua Yamaha ambayo ni bora kutafuta katoyota used mtaani
Kuanzia m5

Waambie hao
 
Back
Top Bottom