Piiiiiii!!!! Matangazo ya ajira feki

mbasamwoga

Member
Jul 6, 2011
70
11
wabongo bwana wamezidi kuchakachua,
kutokana na watumiaji wa mawasiliano kwa njia ya mtandao kuongezeka, na matumiaji wengi ni wasomi hasa wale waliomaliza vyuo na wanatafuta kazi, sasa imekuwa balaa.

Kuna mitandao ya kibiashara inapachika matangazo feki ya ajira ili kuvutia watumiaji ili mtandao huo ujipatie umaarufu na kupata ulaji wa matangazo ya kibiashara. Ili wana jf wafike kwenyekurasa zao wanaweka kazi hizo feki kwa kutumia link za mitandao yao. Mara dar everything, mara people power zile kazi ni uongo mtupu.... Kama wanajf mnataka kuamini mtu mmoja ajaribu kwenda manualy kwenye hizo ofisi wanazodai zimetangaza ajira aone ataambiwa nini???

Hebu jiulize kama kweli ni kazi za ukweli kwanini kila siku ni hizo hizo bali wanabadili tarehe??
Kama kweli wanania njema ya kutujuza wanajf nafasi za kazi kwanini waweke link nyigine na sio tangazo halisi????

jamani msitumalizie visarafu vyetu kutuma maombi ya kazi feki...... Wala msitafute umaarufu kupitia jf!!!!!
 
boss80

Member
Mar 15, 2011
45
7
Mdau umeongea suala la msingi sana maana nakubaliana na wewe moja kwa moja kuwa matangazo ya kazi yaliyomengi ni feki na nadhani wahusika wanakuwa na nia nyingine ya kujinufaisha ama kiuchumi au kiumaarufu. Jamani tuwe wakweli katika hili.
 
zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,502
7,827
huu nao ni ufisadi! tena wanakoleza kweli kweli kwenye kutangaza hizo nafasi za kazi, chombo cha ukweli na chakuaminika ni kupitia magazeti kama mwananchi, daily news, the gurdian nk. na matangazo ya kuaminika ni yale ya serikali tu japo nao sometimes wanachakachua kwakutangaza nafasi wakati tayari wameshaajiri ndugu zao.
 
hiakaman

Member
Jun 27, 2011
40
5
Inaweza kuwa kweli, Maana na mimi nimeona kazi ya Data Entry wanasema mshahara $500 per day ukilinki wanakuacha uchocholoniJe ni mabadiliko ya Uchumi na Ubunifu Tanzania?Je wanafanya ni ubunifu?Je JF itaendelea kuaminiwa milele kama haitakuwa makini?NAKUSHI MWENZANGU PIGANA, USICHOKE, BADO UNA NAFASI KUBWAHOPE WLL WIN.CHEERS
 
mchakachuaji

Member
Aug 12, 2010
58
7
that's true, pia kuna taasisi na makampuni yanayojifanya kutangaza kazi na scholarships wakati tayari wana watu wao.TAKUKURU VP HAPA?
 
Inanambo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
3,663
2,334
naamini hakuna nafasi ya kazi inaweza patikana kwenye hii mitandao ya Jamii. Kazi kujuana. kama huna network sahihi ya wakubwa wenye NGO'S hupati kazi na hata ukiandika ukidhani unaqualification hupati. Ziko wapi zile kazi za Ifakara Health Institute? watu walipigana vikumbo kule kupeleka barua lakini wapi hadi leo hakuna majibu. Kazi bongo Network sahihi tuu siyo elimu wala ujuzi.
 
kaygeezo

Senior Member
Jul 31, 2008
193
10
wabongo bwana wamezidi kuchakachua,
kutokana na watumiaji wa mawasiliano kwa njia ya mtandao kuongezeka, na matumiaji wengi ni wasomi hasa wale waliomaliza vyuo na wanatafuta kazi, sasa imekuwa balaa.

Kuna mitandao ya kibiashara inapachika matangazo feki ya ajira ili kuvutia watumiaji ili mtandao huo ujipatie umaarufu na kupata ulaji wa matangazo ya kibiashara. Ili wana jf wafike kwenyekurasa zao wanaweka kazi hizo feki kwa kutumia link za mitandao yao. Mara dar everything, mara people power zile kazi ni uongo mtupu.... Kama wanajf mnataka kuamini mtu mmoja ajaribu kwenda manualy kwenye hizo ofisi wanazodai zimetangaza ajira aone ataambiwa nini???

Hebu jiulize kama kweli ni kazi za ukweli kwanini kila siku ni hizo hizo bali wanabadili tarehe??
Kama kweli wanania njema ya kutujuza wanajf nafasi za kazi kwanini waweke link nyigine na sio tangazo halisi????

jamani msitumalizie visarafu vyetu kutuma maombi ya kazi feki...... Wala msitafute umaarufu kupitia jf!!!!!

haswa peoplepower
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom