Wamarekani walidhania dunia bado iko kwenye "
The American Century"
Hebu sasa ona walivyojidhalilisha mbele ya dunia, tupilia mbali mikwara bubu yotee ile.
Leo hii Marekani hawezi kuacha kutoa misaada kwenye hizo nchi tajwa hapo juu.
Ukiangalia kwa makini utanona kuna sababu ngumu sana za kimkakati zitakazofanya Marekani iendelee kutoa misaada.
Mosi,
Kwenye hii vita Marekani alikuwa peke yake kwasababu hata Marafiki zake wakubwa hasa wale kutoka Umoja wa Kujihami wa nchi za Magharibi (
NATO) hawajapiga kura ya kumsaidia Marekani. Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Ubelgiji wamekubaliana na Azimio kwamba Kauli ya Marekani kuhusu Jerusalemu kuwa mji mkuu wa Israel inabidi iondolewe.
Marekani alihitaji ushawishi wa mataifa makubwa ya Ulaya ili aweze kufanikisha huo mkakati wake.
Mataifa mengi ya Ulaya hasa hasa Ujerumani yengekubali tu huu mchezo basi ni lazima ingekula kwao,
Yangeingia kwenye mtafaruku mkubwa sana wa kisiasa na waislamu hapa duniani,
Tena ingekuwa ni vibaya sana kwa Usalama wa nchi zao hasahasa ukiangalia kwamba kipindi hiki Ulaya kumejaa wakimbizi wa vita kutoka nchi za Mashariki ya kati na zile za Kaskazini mwa Afrika: Kungekuwa na matukio mazito sana ya kigaidi huko Barani Ulaya hivyo wazungu wa Ulaya wakaliona hili mapemaa.
Pili,
Marekani atendelea kutoa misaada hata kwa aibu tu kwasababu za Usalama wake yeye binafsi.
Jiulize swali rahisi tu. Hivi Marekani akisitisha Misaada kwa nchi kama:
Afghanistan- Ambako kuna wanajeshi wake kama
11, 000 kama ilivyosema
The Pentagon mnamo Mwezi Agosti mwaka huu. Je watakuwa salama kweli ??? Sidhani kabisaa, kwasababu hata kama akiamua kutoa vikosi vyake hatavitoa ndani ya siku mbili. Upande wa pili wa shilingi vikosi vya Marekani viko pale Afghanistani kwasababu za kimkakati kama kupambana na Maslahi ya nchi kama Iran, Uchina na Urusi. Leo hii wakisitisha msaada kwenye ile nchi, basi itakuwa neema kubwa sana kwa nchi ya Iran, maana Afghanistani na Iran ni kama Tanzania na Congo, zinapakana sana. Pia Afghanistan ikiwa na shida na hela basi itaomba kwa Uchina na ikiwa na shida kijeshi basi itaomba kwa Urusi. Habari za chini chini zinasema kwamba kundi la wanamgambo "
The Taliban" leo hii liko kwenye mahusiano mazuri sana na Urusi, Uchina na Iran. Hawezi jaribu kwasababu anajua atatengeneza Hezbollah ya pili na nguvu ya nchi kama Iran itakuwa kubwa mwisho wake itahatarisha usalama wa biashara yake kwenye
THE PERSIAN GULF.
Japan na Korea Kusini- Huku ndiyo hawezi kabisa kwasababu akisitisha kutoa msaada wa Kijeshi yule bwana Kiduku wa Korea Kaskazini wakisaidiwa na Uchina watatawala
The Korean Peninsula yoteee. Bila Ubishii hili litakuwa ni hatari kwake kibiashara na Kiusalama hasa ukichukulia Ujirani baina ya Uchina, Korea na Marekani.
Tatu,
Marekani hata akiuziria Umoja wa Mataifa bado ni hatari sana kwake.
Nafasi ya Ushawishi ya Taifa la Marekani ndani ya Umoja wa Mataifa ni kubwa sanaaa.
Nchi nyingi kama Urusi, Marekani, Ujerumani na Uingereza zinaionea gere kwa shauku kubwa.
Balozi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa
Bi.Nikki Haley jana alitishia
United Nations General Assembly (UNGA) "kwamba sisi ndiyo tunaochangia sana Umoja wa Mataifa hivyo hatuwezi kukubali kudharauriwa na mataifa ambayo yanachukua mchango wetu bure" . Ameongea kwa kujiamini sana huku akihisi hizi ndizo zama za Clinton au Bush mdogo (Miaka ya 1991-2008) ambapo Marekani aliweza kusema na kufanya lolote bila kuwajibishwa.
Kwenye siasa kuna kitu kinaitwa
"Power Vacuum"
Kwamba taifa lenye nguvu linapoamua kuacha kutumia hizo nguvu zake katika mahusiano basi linatengeneza kitu kinachoitwa
"Power Vacuum" au "
Ombwe la Kisiasa". Ombwe la kisiasa linapotokea basi ni lazima nchi nyingine yenye nguvu au pinzani itachukua nafasi ile ili kuziba pengo kwa ajili ya maslahi yake yenyewe.
Ushahidi wa hili hapa ni huu,
Kipindi chote cha Vita Baridi (
1947-1989) dunia ilikuwa chinia ya utawala wa kambi mbili za Urusi ya Kisovyeti na Marekani. Hii iliitwa
"Bipolarity Rule" hivyo kupelekea maamuzi yoyote muhimu ya dunia hii kupata Baraka za hizi kambi mbili. Na ili mambo yaende shwari kambi hizi mbili ni lazima zikubaliane.
Lakini sasa mwaka
1950 Korea Kaskazini ilivamia
Korea Kusini ili kuiunganisha iwe nchi moja,
Umoja wa Mataifa ulilaani kitendo hicho lakini kumbe Urusi alikuwa amekibariki na hivyo akakwaruzana na wenzake.
Akaamua kabisa kuondoka kwenye vikao vya Umoja wa Mataifa akiamini kabisa kichwani kwamba hawawezi kufanya lolote bila wao kuwepo. Bahati mbaya sana kutokuwepo kwake kulitengeneza kitu kinachoitwa "
Power Vacuum" ambapo taifa pinzani lenye nguvu kama Marekani liliamua kuijaza hiyo nafasi na kuitumia vilivyo.
Baraza la Ulinzi na Usalama likazingatia akidi na kuamua kupitisha Waraka wa Kuzuia Uvamizi wa Korea Kaskazini kijeshi.
Waraka ukapita na Urusi akaja kuambiwa umepitishwa bila yeye kuwepo ambapo angekuwepo basi hata angeweka
VETO.
Hivyo
NATO wakiongozwa na Marekani wakavamia Korea Kaskazini, hadi kupelekea
The Korean War 1950-1953.
Lakini huenda Urusi angekuwepo na kuweka kura ya
VETO basi ingewalazimu
NATO kutumia njia nyingine mbadala.
Kibaya zaidi kipindi hicho Uchina haikuwepo kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa kwasababu ya mapinduzi ya kikomunisti yaliyofanyika mwaka moja nyuma (
1949) hivyo Serikali ya Taiwan ndiyo ikawa na kura turufu ya
VETO.
NB: Marekani akizira basi nakuhakikishia itakula kwake.
Nchi kama Uchina ni lazima atatoa mapesa na huu ndiyo utakuwa mwanzo wa "
The Era of the Dragon"
Atapelekesha sana maamuzi mazito mle ndani, kuanzia The General Assembly hadi The International Court of Justice.
Halafu hapo Marekani atakapokuja kustuka atakuwa amechelewa sanaaaa.
Tano,
Mataifa ya dunia yanajua dhahiri Marekani hawezi kufanya hivyo kwasababu ya Usalama wake mwenyewe,
Hii ndiyo imewafanya kuamua hivyo walivyoamua bila kuogopa chochote kile kuhusu yale mapesaa.
Jarida Maarufu la maswala ya Asia liitwalo
"The Diplomat" linasema kwamba nchi kama Uchina haikubaliani kabisa na mambo mengi ambayo Utawala wa Korea Kaskazini unfanya, lakini hawawezi kufanya lolote kwasababu wakiuminya Utawala wa Korea Kaskazini basi ni lazima watakuwa wanaumiza maslahi yao wenyewe pale kwenye
Korean Peninsula.
Bahati mbaya sana,Korea Kaskazini kashajua huu udhaifu na Uhitaji wa Uchina juu yake hivyo anajifanyia anavyotaka tu.
Lakini bado Uchina anaendelea kumimina mapipa ya misaada mbali mbali.
Upande wa pili wa huu mfano,
Ni kwamba Marekani naye huwa hakubaliani sana na mambo mengi yanayofanywa na Serikali ya Israel lakini kwasababu anajua dhahiri kabisa maslahi yake pale
Persian-Gulf yatakuwa salama pindi Serikali ya
Tel Aviv inakuwa salama.
Bahati mbaya sana, Israeli naye kashajua huu udhaifu na Uhitaji wa Marekani juu yake hivyo anajifanyia anavyotaka tu.
Lakini bado Marekani anaendelea kumimina mapima ya misaada mbali mbali.
Mwisho kabisa,
Kipindi cha Vita Baridi serikali ya Sovieti ya Urusi ilikuwa haikubaliani kabisa na Mambo yanayofanywa na Serikali ya Ujerumani Mashariki na Serikali ya Cuba. Ilifika hadi kipindi KGB ikawa inalalamika na kuchukizwa na michezo inayofanywa na shirika la Kijasusi la Ujerumani Mashariki "
STASI" au shirika la kijasusi la Cuba "
DI"
Wajerumani na Wacuba waliyajua haya kwamba Warusi wanawahitaji hasa kwa ajili ya kuwazima NATO hivyo walikuwa wanafanya sana vurugu na Warusi hawasema chochote kile, na huku wanaendelea kutoa misaada mingi tu.
Ilifika kipindi miaka ya 1980's kipindi cha Gorbachev,
Fidel Castro alianza kufanya tena fujo dhidi ya Raisi wa Marekani Ronald Reagan.
Lakini Warusi walikuwa hawana tena Maslahi na Vita Baridi hivyo wakamwambia Castro.
"If this time you provoke the Americans, you are on your own"
NB: Hivyo Marekani ataacha kutoa misaada pale ambapo anaona nchi hizo hazimpi maslahi mapana kiuchumi na kiusalama.
Sita,
Marekani asitishie watu kwasababu hiyo Misaada huwa hatoi bure.
Wale ni mabepari na wana amini katika kitu kinachoitwa "Quid-Pro-Quo" au "Nipe nikupe"
Leo hii Marekani hawezi kusema anatoa misaada kwa upendo tu, laah hasha: Anapata kitu.
Kifupi nchi zote huwa zinatoa misaada zikitegemea kupata kitu fulani baadae au kujenga ushawishi.
Professor John Mearshimer,
Aliwahi kusema kuna sehemu kubwa tatu ambazo Marekani hawezi kuziacha hata siku moja kwasababu ndizo uhai wake.
Sehemu hizo ndizo uti wa mgongo wa Uchumi wake pamoja na ushawishi wake kisiasa. Sehemu hizo ni:
- Europe- Hapa anaangalia sana kwasababu anaogopa nguvu ya Urusi, anauza sana silaha na pia anazuia nguvu ya Umoja wa Ulaya. Tangu vita baridi wakina George Kennan na George Marshall walijua kabisa kwamba Marekani hawezi kushindana na Ulaya iliyounganika, na ikiwa upande wa Urusi. Hivyo basi ni lazima Marekani awe katika hali mbaya na Urusi ili Ulaya imwogope Urusi na hivyo kuwafanya wao wategemee sana uwepo wa Marekani barani hapo. Uwepo wa Marekani pale unapunguza ukuaji wa ushawishi wa bara la Ulaya kwasababu bajeti karibia yote ya nano analipia yeye. Kama ikatokea Ulaya yote ikaungana na kuwa taifa moja basi wao ndiyo wanaweza kuwa taifa lenye nguvu kuwahi tokea duniani kwasababu ya Idadi ya wasomi, ukubwa wa uchumi wao na uwepo wa nguvu ya viwanda. Marekani anajua kabisa atapoteana kama ilivyokuwa karne ya 20 ambapo Ulaya ndiyo ilikuwa sehemu ya viwanda na kila kitu.
- The Persian Gulf- Hapa ni eneo la Mashariki ya kati ambako Marekani anafanya biashara zake za Mafuta na kuuza silaha. Wataalamu wanasema Uchumi wa Marekani kama nchi uliyumbishwa sana na vita za Iraq na Afghanistani lakini makampuni binafsi ya mafuta na silaha yalipata sana pesa. Leo hii unaambiwa vita ya Iraq pekee imelifanya kampuni la mafuta la Marekani "Halliburton" limepata faida mara tano kuliko kawaida yake. Makampuni ya silaha ndiyo usiseme kabisaa, Serikali za Israel, Saudi Arabia na Qatar zimefanya biashara nzito sanaa na mwaka huu na kuiletea Marekani Matrillioni ya faida. Sasa leo hii akiwaacha hawa unategemea kwamba hizi dili atazipata kweli ???Makampuni ya binafsi ya Ulinzi kama BLACKWATER yanafanya kazi kama MERCENARIES na yanalipwa mabilioni ya pesa. Juzi nasikia Marekani imetoa kama USD million 28 kwa ajili ya kununulia jeshi la Afghanistani magwanda ya kijeshi ambayo yanafanya mwanajeshi asionekani kirahisi "Camouflage Uniform" na hapa kuna makampuni yashapiga pesa tayari. Leo hii akizira basi nchi kama Urusi na Iran zitapiga vigelegele kwasababu watamiliki wao biashara kubwa za mafuta ili kuua upinzani kabisa na pia Urusi atauza silaha.
- Western Hemisphere- Hili ni eneo la Bara la Marekani Kaskazini na Kusini ambapo kama Marekani atasema ayaache baadhi ya mataifa yaliyo jirani naye kama Japan, Taiwan na Korea Kusini basi ushawishi wa china utasambaa pale Pacific Belt yote na kufika nyumbani kwake kitu ambacho Marekani alijifunza sana mwaka 1812-1814 (Anglo-American War) baada ya Vita na Muingereza akishuhudia Ikulu yake ikichomwa moto. Na mwaka 1962 baada ya kuona Cuba inaweza ikatumika kumuumiza.
NB: Urusi alikuwa na maslahi makubwa sana nchini Libya,
Alikubaliana kwamba atawauzia silaha zenye thamani ya Trillioni kumi na moja kwa awamu.
Hakuingilia sana ule ugomvi zaidi ya kulaani tu akitegemea Serikali ya Libya itaheshimu mikataba ile ya kibiashara.
Lakini baada ya Gaddafi kufa serikali mpya ikapiga chini mikataba ile yote na kumpa Mfaransa,
Urusi ikala kwake kama ilivyokuwa kule Iraq kwa Saddam Hussein ambapo Yevgeny Primakov alikubali kuwapa mkopo wa Vifaru zaidi ya 1000 lakini baada ya vita lile deni limesuasua mpaka leo.
MY TAKE: Marekani akiendelea kutishia hivyo watamkomoa sanaaa.
kuna kipindi Ulaya walitishia asana umoja wa Afrika kuhusiana na Mzee Mugabe lakini AU wakakomoa kwa kumchagua awe mwenyekiti wa Umoja huo.
Dunia imebadilika sanaaa kwa miaka michache,
Mataifa mengi sana siku hizi yanepesa za kutoa kwa mataifa madogo.
Urusi anakwepa vikwazo kwasababu Uchina na Iran wapo hivyo sidhani kama Marekani atakomoa.
Anayajua vizuri haya na ataishia kutishia tu....
CC:
Consigliere ,
MSEZA MKULU ,
Red Giant,
Bukyanagandi,
Dragoon ,
Mbimbinho,
Maalim Shewedy,
zitto junior ,
Kingdom_man ,
herikipaji ,
Dotworld ,
Gide MK ,
mtembea kwa miguu ,
cognition