Trump ahaha kuzuia wahamiaji kuingia Marekani

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,996
Reaction score
61,229
RAIS Donald Trump amekuwa akiongea kwa nguvu kuliko kawaida kutokana na tishio jipya dhidi ya utawala wake: afanye nini pale maelfu kadhaa ya wakimbizi kutoka nchi tatu au nne za Amerika ya Kusini wakikaribia mpaka wa Marekani kutoka Mexico.

Licha ya kuzuiwa na polisi mara kadhaa kuanzia mpaka wa Honduras na Guatemala, halafu mpaka wa Guatemala na Mexico, polisi hao ambao walitumia zana hafifu kwani watu hao si wapiganaji na hawakuwa wanafanya fujo zozote walishindwa kuwazuia.

Katika kituo kimoja mpakani, polisi walirudi katika mabasi yaliyowaleta wakawaacha wakimbizi hao kuvuka mpaka kuingia Mexico, wakamalizane huko.

Na nchini Marekani inaelekea hawajui cha kufanya.Vitisho visivyoeleweka kutoka kwa Rais Trump vimesikika muda wote tangu msafara huo uanze safari yake kutoka Honduras, kwa lengo la kuingia Marekani, na kati ya vitisho hivyo kilichoeleweka zaidi ni kuanza kusitisha misaada kwa nchi zinazoruhusu msafara huo wa wakimbizi upite.

Waliojumuika katika msafara huo wanapata tabu hasa kwa sababu wanaenda kwa miguu kupitia nchi kama tatu, wengi wakiwa na hati za kusafiria bila visa (kibali cha muda maalum) kuingia Marekani.

Taarifa zilisema kuwa, wakati polisi mpakani walijaribu kuzuia wanamsafara kuvuka daraja, baadhi walitumia mitumbwi kuvuka mpaka wa baharini, kwani njia ni ukanda wa pwani ya Magharibi ya nchi hizo za Amerika ya Kusini.

Wakimbizi hao wanatazamia kuwa wingi wao na kujaribu kwao kuingia Marekani kwa amani kwa sababu tu ya kutafuta maisha bora zaidi kwao na watoto wao ni sababu tosha ya kuruhusiwa kuingia Marekani.

Si rahisi kwani Rais Trump ameapa kwa kila kiapo anachojua na kuanza kupambana na taasisi au mamlaka zinazotoa kinga kwa uundwaji wa msafara huo, hatua ya kwanza ikiwa ni kukata misaada kwa nchi za Amerika ya Kusini, zilizoruhusu msafara huo kupita.

Hatua nyingine ni kuanza kampeni ya kubadilishwa sheria za uhamiaji, ambako Rais Trump anasema Democrats wanazuia hilo.
Hata maofisa wa juu wa utawala wa Trump walikuwa hawajui nini hasa cha kufanya msafara huo ukifika mipaka ya Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo akisema kuwa msafara huo ni mkasa.

Hakufafanua ila hawezi kutofautiana na Trump kuwa msafara huo ni wa kisiasa, wenye nia ya kuijaribu Marekani kama ina ubavu – kwa maana ya ukatili – wa kutumia njia zozote zile kuzuia msafara huo usiingie Marekani, kama hawataamua wao wenyewe kurudi.

Na kweli baadhi ya wale walioanza safari hiyo walishaaga na kurudi makwao, wakisita kuendelea kwani ni giza nene nini kitafuata hapo mpakani.

Rais Trump ameashiria kuwa ataufunga mpaka wa Marekani na Mexico kuhusiana na msafara huo, suala ambalo si la jana au juzi, labda kama ni pamoja na kuzuia bidhaa za Mexico zisiingie kabisa, ambayo ina maana kuweka vikwazo, na siyo kuondoa tu misaada.

Wakimbizi au wanamsafara wenyewe wamepuuza onyo la Trump kuondoka katika msafara huo, wakitumainia kuwa wingi wao utakuwa nguvu yao dhidi ya Trump.

Hata hivyo, ni vigumu kusema ni wangapi watafika mpakani kwa walioondoka Honduras ambako msafara huo uliundwa walishapungua kwa kiasi cha watu 1 ,000 lakini njiani, huko Guatemala, kiasi cha 2,000 au zaidi walishajiunga na wengine walikuwa wanadandia njiani. Wamexico wangejiunga.

Jambo la msingi ni kuwa kuna mianya katika sheria za Marekani ambayo inawezesha wanamsafara kuwa na matumaini kuwa jitihada yao itazaa matunda, licha ya kuwa msafara huu hauhusiki katika mzozo kati ya Rais Trump na watetezi wa haki za binadamu, hata mkewe Melania akampinga hadharani.

Ilikuwa ni suala la kurudisha wahamiaji haramu kwa kila njia, ila kuwaacha watoto waliozaliwa Marekani hata wakiwa na umri mdogo. Hiyo ikaleta mzozo wa kutenganisha familia, huku sintofahamu ikitanda kama hao watoto warudishwe pamoja na wazazi wao au hao wazazi wabaki kutokana na uhusiano na mtoto aliye raia wa Marekani.

Inaelekea kuna vipengele vingine vya jinsi ya kushughulikia ukimbizi vinagomba.

Kwa upande fulani wimbi hilo la wakimbizi au msafara wa wanaotaka kuingia Marekani kinyume cha sheria unaweza kumsaidia Rais Trump katika uchaguzi mkuu katikati ya muhula kurudisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na theluthi moja ya wajumbe Baraza la Senate.

Mabaraza hayo kwa pamoja ndiyo yanaunda Bunge la Marekani, yaani Congress, na mazingira ya sasa siyo mema kwa Rais Trump kwani kuna uchunguzi kama alifaidika na vitendo vya kijasusi vya Russia vya kuweka habari potofu kwa makundi tofauti ya wapiga kura kuelekeza nia zao za kupiga kura dhidi ya chama cha Democrat unatesa.

Wakati huo huo, hatari ya wimbi kubwa la ukimbizi uchumi wa aina hiyo itawahamasisha wafuasi wake.

Kwa maana hiyo kuna uwezekano wa utawala wa Trump kuacha suala hilo lisumbue watu kwa kiasi fulani huku akijaribu kila anachoweza kuonyesha kuwa ukimbizi huo au uhamiaji wa kulazimisha kuingia Marekani unalenga hisia za chama hicho ambacho sasa kiko upinzani.

Inategemea watafika langoni mwa Marekani wakiwa wangapi na vipengele vya sheria vinasemaje kuhusu kundi la watu wanaotaka kuingia, tofauti na kumkamata mtu mmoja mmoja ambaye ni rahisi kumchukulia hatua na kumrudisha kwao.

Kuna chembe ya siasa za kutaka huruma, kwani wengi kati ya wahamiaji haramu wa msafara siyo makundi ya wanaume kama hawa wanaopitia jangwa la Sahara ila wanawake, watoto, wazee wapo pia.

Wachambuzi wa habari wanasema kuwa, moja ya misukumo ya kuunda msafara kwenda kwa pamoja ni tabia ya makundi ya maharamia katika maeneo ya mipakani au njia kuu, wakiona kuna watu wachache wanapita kuelekea mpaka wa nchi nyingine.

Wanajua kuwa wamejitahidi kuwa na fedha kiasi fulani mfukoni za kujikimu, hivyo wanawateka na kuwanyang’anya kila walichonacho, kuanza kuwatumikisha kwa nguvu wapate vijisenti kurudi kwao, safari iwe imeharibika.

Kuunda msafara ilikuwa ni njia ya kutafuta usalama katika safari hiyo, licha ya kuwa ni ya mashaka matupu kwani hawatakiwi Marekani.

Msafara huo ulianzishwa katika mtandao na kikundi cha kupigania haki za binadamu kinachojiita ‘Watu Wasio na Mipaka’ na kwa maana hiyo dhamira yao ni kueneza itikadi kuwa kila mtu duniani au katika bara la Amerika ana haki ya kuingia na kuishi Marekani.

Ni tatizo ambalo pia limetanda Afrika ambako mamilioni ya vijana wana hisia za karibu na Ulaya kutokana na utandawazi kwa jumla na michezo kwa karibu zaidi, na wanafikia imani kuwa wana haki ya kuhamia huko kutafuta maisha.

Tatizo ni kuwa iwe ni Amerika ya Kusini au Afrika hao ambao watu wanahamia kwao hawatakiwi huku, na hata wangekuwa wanatokea huku, wakishapata uraia wa huko (baada ya kukaa kihalali kwa mfano kwa miaka 10 na zaidi) wanapoteza uraia wa huku.

Wakirudi wanaingia kama wawekezaji, waombe uraia upya – sasa katika hali hiyo ni haki zipi za binadamu wa huku kuhamia Ulaya ambazo wale wa Ulaya hawana hapa?

Screenshot_20181024-085624.jpeg
 
Wazungu ni wanafiki tu,Tanzania ni nchi maskini lkn inabebeshwa mzigo mzito wa wakimbizi wa kivita kutoka Drc,Rwanda,Burundi etc lkn inajitahidi hivyo hivyo na umaskini wake,iweje wao matajiri US wazingue kusaidia hao wakimbizi wa kiuchumi?

Wapambane na hali yao aisee.
 
Wakimbiz wa kiuchumi!! Wakiruhusu hilo baada ya miezi miwili TZ itakuwa na RAIA 10,000,000 tu badala ya 50,000,000 waliopo sasa.
 
Wazungu ni wanafiki tu,Tanzania ni nchi maskini lkn inabebeshwa mzigo mzito wa wakimbizi wa kivita kutoka Drc,Rwanda,Burundi etc lkn inajitahidi hivyo hivyo na umaskini wake,iweje wao matajiri US wazingue kusaidia hao wakimbizi wa kiuchumi?

Wapambane na hali yao aisee.
Alafu hayoematukio wameyatengeneza wenyewe, hizo ni nguvu kazi kwa ajili ya viwanda walahi
Hawa watu huwa wanaangalia miaka 50 na Zaidi ijayo, nia yao ni kumpiga chini mchina walahi
Wadhungu wakikuonyesha njia ya kushoto ujue njia sahihi ni kulia walahi
Mola a tuongoze milele yote walahi
 
View attachment 908818
Matatizo ya Nchi za America ya Kati yamesababishwa na sera za nje za Marekani, kwahiyo wawapokee tu hao wakimbizi, ni Sawa na Sarkozy na Bulsconi walivyomuuwa Gadafi wakasababisha mlipuko wa wakimbizi Ulaya
 
Wazungu ni wanafiki tu,Tanzania ni nchi maskini lkn inabebeshwa mzigo mzito wa wakimbizi wa kivita kutoka Drc,Rwanda,Burundi etc lkn inajitahidi hivyo hivyo na umaskini wake,iweje wao matajiri US wazingue kusaidia hao wakimbizi wa kiuchumi?

Wapambane na hali yao aisee.
hao wakimbizi una walisha wewe???mbona karibia kila kitu hao wazungu ndio wana wahudumia?
 
Kwanini na sasa wasiwalishe hao wakimbizi wanaoenda kuishi ndani ya USA?

Kwa jinsi akili yako ilivyo ndogo kama punje ya haradanu,unawaza msosi tu,madhara mengine huyaoni sio?

Hao wakinkimbizi wanavyokuja bongo na silaha za kivita na kuteka magari na watu huko mipakani Kigoma na Ngara hao wazungu walisaidia nini?Wanavyoharibu mazingira huku Tz hao wazungu walisaidia nini?
 
Back
Top Bottom