Pigo lingine kwa wastaafu

Pigo lingine kwa wastaafu

Nanoli

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2015
Posts
3,739
Reaction score
5,979
Maamuzi ya Serikali kununua korosho za wakulima limekua ni jambo jema na zuri kwa kuwainua wakulima, lakini maamuzi ya Serikali kununua ni hakika kuwa haukupangwa ndio maana kumetokea kauli za kutofautiana kati ya PM na JPM, limekuwa jambo la kukurupuka kwa serikali kwani nina imani kubwa serikali haikuweka bajeti ya manunuzi.

Na kama gharama ya manunuzi na usafirishaji huenda ikawa serikali inahitaji pesa za kutosha ili kuendesha zoezi hili, kama alivyotangulia PM kusema, serikali haikuwa na mpango wa kununua wenyewe bali kuwatumia mabalozi kutafuta kampuni.

Sasa kwa mkurupuko huu naona boti la wastaafu linazidi kuzama kwani pesa zao zitahusika manunuzi ya korosho.

Kwahiyo wastaafu wajiandae kisaikolojia, tuendelee kuvumilia mpaka tutapofanya mauzo nje nchi.
 
Sisi wastaafu tutasubiri faida itakayopatikana....tunaiamini sirikali yetu
 
Kwani hela za ile bank ya wakulima ndipo hela za wastafu huifadhiwa?
 
Dah!, utaratibu huu bana!, unalima mwenyewe
halafu unakuja kupangiwa utaratibu wa kuuza
bidhaa yako!, wakulima tunateseka sana!
 
Kijimbuzi cha bwana heri, kijishamba cha bwana heri, basi sote tuseme heriiiiiiiiii.
 
Kumbuka serikali inayo fedha za dharula kwa ajili ya majanga vita njaa nk acha uchonganishi.
 
Back
Top Bottom