Piganieni kupata Haki zenu kupitia wabunge watakao wawakilisha bungeni kwa hoja zitakazobeba msingi wa CHADEMA

Si kimeishakufa? Kwa nini unasumbuka na chama mfu? Hata hivyo mamlaka ya kukifuta si mnayo? Kwa nini msikifute tu kama kinawspa shida?

Amandla...
Ww Sasa lengo lako ni kama Lisu
Nimeshakusoma

Mapambano yote Yale kumbe ni geresha tu
 
Hoja yako haina mashiko kwasababu wawakilishi wanachagukiwa na wananchi siyo wawakilishi wa chama, kama wako hao wa CCM si ndiyo watawakilisha wananchi vizuri zaidi maana hata Rais alisikika akisema anataka wabunge wa CCM atakaoweza kuwadhibiti.

Wote tumeona nguvu iliyotumika na state organs zetu kuhakikisha wanapita wabunge wa CCM. Rais alishasema hataki kuwepo na upinzani sasa kama maendeleo yatapatikana kwa haraka kuwaondoa wapinzani kwenye uwakilishi sasa si ndiyo wakati mzuri nchi yetu ipate hayo maendeleo.

Sasa kutaka wabunge wa CHADEMA wakapunguze kasi ya kuleta maendeleo siyo ushauri mzuri. Ushauri mzuri CHADEMA pamoja na vyama vingine waondoe wawakilishi walioshinda ili wasiweze kupunguza kasi ya maendeleo tena katika nchi yetu
Hayo sasa ni mambo ya kitoto, Sasa mnaenda huko ulaya kulialia nini?
 
Mimi naamini kabisa kuwa Tundu Lisu ni mtu ambae ametumwa Kuja kuua upinzani Tanzania na hasa chadema take my words

Anaposema wasipeleke wabunge wa viti maalum wakati anajuafika msimamo wa serikali yetu ni Miaka mitano no siasa

Kwa maana hiyo chadema Watakaa Miaka mitano bila kusikika popote hapa Tanzania

Na ndio maana Lisu mwenyewe amesepa na hatorudi Tena Mpaka next uchaguzi,

Chadema wanatakiwa kuwaza Mara mbili

CHADEMA ipi ambayo Tundu Lissu amekuja kuua si tuliambiwa CHADEMA ilishakufa kabla hata Lisu hajaja. Mbona tunataka kumuonea Lissu. Hivi wale waliokuwa wameshika mabegi ya kura zilizopigwa walikuwa wafuasi wa Lissu kumbe maana ule wizi ndo umesababishwa wapinzani wasiweze kwenda bungeni.

Ni aibu sana kulaumu vyama vya upinzani kwa wizi wa kura uliofanyika wazi wazi. Je huko Zanzibar ambako kuna ngome ya ACT ni Lissu ndiye ameua hicho chama hadi kikapoteza majimbo karibu yote.

Unafiki siyo kitu kizuri kwakuwa madhara ya wizi wa kura ni kuwa na viongozi wezi na ndicho tutakachoshuhudia serikali inayotokana na wizi wa kura itaandamwa na mikosi hadi miaka 5 itakwisha hakuna kilichofanyika na wataamua kuiba tena sababu hakuna mwananchi anayejitambua anataka huu umasikini inatokana na uongozi mbaya.
 
TUIOKOE CHADEMA KWA WABUNGE VITI MAALUM. VIBURI VYA VIONGOZI WAO VISIPOTEZE WATETEZI WA WANANCHI.

TUANZE NA HISTORIA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019.

Don Nalimison naanza kwa hoja: CHADEMA ilijitoa Uchaguzi Mkuu wa Serikali za mitaa na hivyo wagombea wote wa CCM Nchi zima walipita bila kupingwa na hivyo CCM wakajitwalia Vijiji, Vitongoji na mitaa kwa bwerere, pamoja na CHADEMA kujiondoa lakini hakuna kilicho haribika na mpaka leo Viongozi wa Serikali za mitaa wanakula maisha tu. Kujitoa kwa CHADEMA kuliinufaisha CCM KUSHINDA kwa kishindo.
NB: Unapopambania Demokrasia hutakiwi kujitoa ni Bora uanguke kuliko kumpa nafasi mpinzani wako. Kosa la CHADEMA ni ujuaji usio na faida.

TUANGALIE SASA UTEUZI WABUNGE VITI MAALUM BAADA YA UCHAGUZI MKUU 2020.

Kama Chadema hawatapeleka Wabunge wao wa Viti Maalum hakuna chochote watakacho faidi zaidi ya kuwaachia CCM wafanye maamuzi bungeni hata kwenye Mambo ya kijinga. Kidogo kilichopo ndicho kitumike kuleta MABADILIKO ni heri moja yenye nguvu kuliko mbili isiyo na mashiko. Ni heri kupeleka hao wabunge wachache wakatie Chachu bungeni kuliko kuwaachia Uhuru wote CCM.

Ruzuku ya trioni mbili kuikosa Serikali kisa kukosekana wabunge wa upinzani ni sawa na bure maana CCM ndio Serikali wanaweza kubuni miladi au vyanzo vingine vya mapato na kufidia pengo la trioni mbili. Hivyo haisaidii Kuacha kupeleka wabunge Viti maalum. Ni bora wateuliwe waende bungeni wakatetee hojaza wananchi na mapendekezo ya Chama na hoja za Chama.

NB: Piganieni kupata Haki zenu kupitia wabunge watakao wawakilisha bungeni kwa hoja zitakazobeba msingi wa CHADEMA. Mimi Don Nalimison najaribu kujenga hoja ya kuokoa jahazi tu. Siku njema na Karibuni Kahama, Shinyanga.

DON NALIMISON.
Hakuna haja kushiriki ushenzi huu wa siku hizi.
 
Kama cdm walijitoa uchaguzi SM, hivyo vyama vingine vya upinzani vilienda wapi?

Ni swali zuri sana utadhania Tanzania kuna chama cha upinzani kimoja tu. Sasa wamekiandama CHADEMA kwanini lazima CHADEMA si waende hivyo vyama vingine waliokuwa wameunga mkono mgombea wa CCM. Viko vyama 9 vimetambua uchaguzi sasa kwanini mnahangaika na CHADEMA acha kife si kuna vingine vipo
 
Tunataka chama chetu kisikike, kuliko kukaa kimya kwa miaka mitano

Hakuna mtu mtamkomoa zaid ya nyie wenyewe chadema

Kwani chama kiko kimoja tu si muache hivyo vya TLP na UPDP visikike Kwani siyo vyama vya Siasa na kila mwaka vinasimamisha wagombea
 
Mimi nashauri Chadema ichague wabunge 264 moja kwa kila jimbo na wawe na bunge lao nje ya bunge! Hawa watetee wananchi kwa kuita wanahabari kila mwezi na kusema shida za wananchi! Watalipwaje?? Wananchi!!
 
Mimi naamini kabisa kuwa Tundu Lisu ni mtu ambae ametumwa Kuja kuua upinzani Tanzania na hasa chadema take my words

Anaposema wasipeleke wabunge wa viti maalum wakati anajuafika msimamo wa serikali yetu ni Miaka mitano no siasa

Kwa maana hiyo chadema Watakaa Miaka mitano bila kusikika popote hapa Tanzania

Na ndio maana Lisu mwenyewe amesepa na hatorudi Tena Mpaka next uchaguzi,

Chadema wanatakiwa kuwaza Mara mbili
Kwani Lissu ndiye aliyesema hadi ikifika 2020 anataka upinzani uwe umekufa?.Au wewe hii kauli hukuwahi kuisikia?.
 
Tunataka chama chetu kisikike, kuliko kukaa kimya kwa miaka mitano

Hakuna mtu mtamkomoa zaid ya nyie wenyewe chadema
Wewe nani kakwambia kuna mtu anakomolewa?.Acha kua na fikra ndogo.Wacha cdm wawaze nakuamua vile wanaona kwao ni sahihi.kwasababu sidhani kama walipokua wanakutwa na madhila mbalimbali ulijitokeza kuwasaidia.
 
Sasa basi nanyie futeni Hiko chama coz hakuna siasa Mnafanya

Kama miaka mitano ya nyuma mlishindwa kutetea mikutano ya hadhara Sasa hapa unaongea uharo gani?
Wewe kwako siasa ni nini maana inaonekana hata maana ya siasa hujui ni nini.
 
TUIOKOE CHADEMA KWA WABUNGE VITI MAALUM. VIBURI VYA VIONGOZI WAO VISIPOTEZE WATETEZI WA WANANCHI.

TUANZE NA HISTORIA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019.

Don Nalimison naanza kwa hoja: CHADEMA ilijitoa Uchaguzi Mkuu wa Serikali za mitaa na hivyo wagombea wote wa CCM Nchi zima walipita bila kupingwa na hivyo CCM wakajitwalia Vijiji, Vitongoji na mitaa kwa bwerere, pamoja na CHADEMA kujiondoa lakini hakuna kilicho haribika na mpaka leo Viongozi wa Serikali za mitaa wanakula maisha tu. Kujitoa kwa CHADEMA kuliinufaisha CCM KUSHINDA kwa kishindo.
NB: Unapopambania Demokrasia hutakiwi kujitoa ni Bora uanguke kuliko kumpa nafasi mpinzani wako. Kosa la CHADEMA ni ujuaji usio na faida.

TUANGALIE SASA UTEUZI WABUNGE VITI MAALUM BAADA YA UCHAGUZI MKUU 2020.

Kama Chadema hawatapeleka Wabunge wao wa Viti Maalum hakuna chochote watakacho faidi zaidi ya kuwaachia CCM wafanye maamuzi bungeni hata kwenye Mambo ya kijinga. Kidogo kilichopo ndicho kitumike kuleta MABADILIKO ni heri moja yenye nguvu kuliko mbili isiyo na mashiko. Ni heri kupeleka hao wabunge wachache wakatie Chachu bungeni kuliko kuwaachia Uhuru wote CCM.

Ruzuku ya trioni mbili kuikosa Serikali kisa kukosekana wabunge wa upinzani ni sawa na bure maana CCM ndio Serikali wanaweza kubuni miladi au vyanzo vingine vya mapato na kufidia pengo la trioni mbili. Hivyo haisaidii Kuacha kupeleka wabunge Viti maalum. Ni bora wateuliwe waende bungeni wakatetee hojaza wananchi na mapendekezo ya Chama na hoja za Chama.

NB: Piganieni kupata Haki zenu kupitia wabunge watakao wawakilisha bungeni kwa hoja zitakazobeba msingi wa CHADEMA. Mimi Don Nalimison najaribu kujenga hoja ya kuokoa jahazi tu. Siku njema na Karibuni Kahama, Shinyanga.

DON NALIMISON.
Wakwenu wakapiganie haki zenu keanu walishashindwa kuzingatia haki za wengine.
 
Hayo sasa ni mambo ya kitoto, Sasa mnaenda huko ulaya kulialia nini?

Kwahiyo wewe unawapangia kwa kulilia. Aibu ya hii nchi ni ple vyombo vya dola vinapojiingiza kwenye kuchaguwa wawakilishi badala ya kuwaachia wananchi wachague. Hii nchi sasa haina tofauti na nchi inayoongozwa kijeshi maana vyombo vya dola ndo vimechagua wawakilishi wa wananchi. Tuache wafanye hiyo kazi tusihangaike na wapinzani ambao vyombo vya dola vinaona hawatakiwi ila utafika wakati vitangundua umuhimu wa wapinzani.
 
Sasa si mfute chama ili ijulikane hakuna kitu kinaitwa chadema
Kwani kikiwepo hivyo kilivyo wewe kinakuuma nini?.Mmetaka wenyewe kusiwepo na wakuwachelewesha kuleta maendeleo sasa yanini kutapatapa.Waache cdm nyie fanyeni yenu.
 
Kwahiyo wewe unawapangia kwa kulilia. Aibu ya hii nchi ni ple vyombo vya dola vinapojiingiza kwenye kuchaguwa wawakilishi badala ya kuwaachia wananchi wachague. Hii nchi sasa haina tofauti na nchi inayoongozwa kijeshi maana vyombo vya dola ndo vimechagua wawakilishi wa wananchi. Tuache wafanye hiyo kazi tusihangaike na wapinzani ambao vyombo vya dola vinaona hawatakiwi ila utafika wakati vitangundua umuhimu wa wapinzani.
Hao wanainchi mbona wako kimya hawajapinga watu waliochaguliwa?

Au ww unasemea wanainchi gani
 
Back
Top Bottom