Piganieni kupata Haki zenu kupitia wabunge watakao wawakilisha bungeni kwa hoja zitakazobeba msingi wa CHADEMA

Don Nalimison

JF-Expert Member
Jun 26, 2020
646
1,000
TUIOKOE CHADEMA KWA WABUNGE VITI MAALUM. VIBURI VYA VIONGOZI WAO VISIPOTEZE WATETEZI WA WANANCHI

TUANZE NA HISTORIA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019.

Don Nalimison naanza kwa hoja:

CHADEMA ilijitoa Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa na hivyo wagombea wote wa CCM nchi zima walipita bila kupingwa na hivyo CCM wakajitwalia Vijiji, Vitongoji na Mitaa kwa bwerere.

Pamoja na CHADEMA kujiondoa lakini hakuna kilichoharibika na mpaka leo Viongozi wa Serikali za Mitaa wanakula maisha tu. Kujitoa kwa CHADEMA kuliinufaisha CCM kushinda kwa kishindo.

NB: Unapopambania Demokrasia hutakiwi kujitoa; ni bora uanguke kuliko kumpa nafasi mpinzani wako. Kosa la CHADEMA ni ujuaji usio na faida.

TUANGALIE SASA UTEUZI WABUNGE VITI MAALUM BAADA YA UCHAGUZI MKUU 2020.

Kama Chadema hawatapeleka Wabunge wao wa Viti Maalum hakuna chochote watakachofaidi zaidi ya kuwaachia CCM wafanye maamuzi bungeni, hata kwenye Mambo ya kijinga.

Kidogo kilichopo ndicho kitumike kuleta MABADILIKO. Ni heri moja yenye nguvu kuliko mbili isiyo na mashiko. Ni heri kupeleka hao wabunge wachache wakatie chachu bungeni kuliko kuwaachia Uhuru wote CCM.

Ruzuku ya trilioni mbili kuikosa Serikali kisa kukosekana wabunge wa upinzani ni sawa na bure maana CCM ndio Serikali wanaweza kubuni miradi au vyanzo vingine vya mapato na kufidia pengo la trioni mbili.

Hivyo haisaidii kuacha kupeleka wabunge Viti Maalum. Ni bora wateuliwe waende bungeni wakatetee hoja za wananchi na mapendekezo ya Chama na hoja za Chama.

NB: Piganieni kupata haki zenu kupitia wabunge watakao wawakilisha bungeni kwa hoja zitakazobeba msingi wa CHADEMA.

Mimi Don Nalimison najaribu kujenga hoja ya kuokoa jahazi tu.

Siku njema na karibuni Kahama, Shinyanga.

DON NALIMISON
 

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
3,670
2,000
Mimi naamini kabisa kuwa Tundu Lissu ni mtu ambae ametumwa kuja kuua upinzani Tanzania na hasa chadema take my words.

Anaposema wasipeleke wabunge wa viti maalum wakati anajuafika msimamo wa serikali yetu ni Miaka mitano no siasa.

Kwa maana hiyo chadema Watakaa Miaka mitano bila kusikika popote hapa Tanzania.

Na ndio maana Lissu mwenyewe amesepa na hatorudi tena mpaka next uchaguzi.

Chadema wanatakiwa kuwaza mara mbili.
 

Luggy

JF-Expert Member
Aug 6, 2012
2,956
2,000
Kwani hao wabunge wa viti maalumu wana weza kuwazuia CCM kufanya watakayo?
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,322
2,000
Kama Chadema walijitoa uchaguzi SM, hivyo vyama vingine vya upinzani vilienda wapi?
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,189
2,000
Mtaanzisha nyuzi nyingi tu lakini mmebuma.

Hamuwezi kuwaibia Chadema wabunge wa majimbo, kisha mkazunguuka mkataka wawepo wale wa Asante NEC ili muweze kuwahadaa wahisani kuwa bunge ni la vyama vingi.

Sasa mko peke yenu leteni hayo maendeleo mliyokuwa mkisema wapinzani wanawakwaza tuone!
 

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
3,670
2,000
Mtaanzisha nyuzi nyingi tu lakini mmebuma.

Hamuwezi kuwaibia Chadema wabunge wa majimbo, kisha mkazunguuka mkataka wawepo wale wa Asante NEC ili muweze kuwahadaa wahisani kuwa bunge ni la vyama vingi.

Sasa mko peke yenu leteni hayo maendeleo mliyokuwa mkisema wapinzani wanawakwaza tuone!

Sasa basi nanyie futeni Hiko chama coz hakuna siasa Mnafanya

Kama miaka mitano ya nyuma mlishindwa kutetea mikutano ya hadhara Sasa hapa unaongea uharo gani?
 

kasulavenance

JF-Expert Member
Jan 23, 2020
723
1,000
Wabunge 10 wa kuteuliwa wa Magu
1.Queen Sendiga
2.Anna Mghwira
3.James Mbatia
4.Selasini Joseph
5.Lwakatare
6.Hashim Rungwe
7.Aggrey Mwanri
8.Angela Kariuki
9.Ibrahim Lipumba
10.Julius Mtatiro
 

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
1,773
2,000
TUIOKOE CHADEMA KWA WABUNGE VITI MAALUM. VIBURI VYA VIONGOZI WAO VISIPOTEZE WATETEZI WA WANANCHI.

TUANZE NA HISTORIA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019.

Don Nalimison naanza kwa hoja: CHADEMA ilijitoa Uchaguzi Mkuu wa Serikali za mitaa na hivyo wagombea wote wa CCM Nchi zima walipita bila kupingwa na hivyo CCM wakajitwalia Vijiji, Vitongoji na mitaa kwa bwerere, pamoja na CHADEMA kujiondoa lakini hakuna kilicho haribika na mpaka leo Viongozi wa Serikali za mitaa wanakula maisha tu. Kujitoa kwa CHADEMA kuliinufaisha CCM KUSHINDA kwa kishindo.
NB: Unapopambania Demokrasia hutakiwi kujitoa ni Bora uanguke kuliko kumpa nafasi mpinzani wako. Kosa la CHADEMA ni ujuaji usio na faida.

TUANGALIE SASA UTEUZI WABUNGE VITI MAALUM BAADA YA UCHAGUZI MKUU 2020.

Kama Chadema hawatapeleka Wabunge wao wa Viti Maalum hakuna chochote watakacho faidi zaidi ya kuwaachia CCM wafanye maamuzi bungeni hata kwenye Mambo ya kijinga. Kidogo kilichopo ndicho kitumike kuleta MABADILIKO ni heri moja yenye nguvu kuliko mbili isiyo na mashiko. Ni heri kupeleka hao wabunge wachache wakatie Chachu bungeni kuliko kuwaachia Uhuru wote CCM.

Ruzuku ya trioni mbili kuikosa Serikali kisa kukosekana wabunge wa upinzani ni sawa na bure maana CCM ndio Serikali wanaweza kubuni miladi au vyanzo vingine vya mapato na kufidia pengo la trioni mbili. Hivyo haisaidii Kuacha kupeleka wabunge Viti maalum. Ni bora wateuliwe waende bungeni wakatetee hojaza wananchi na mapendekezo ya Chama na hoja za Chama.

NB: Piganieni kupata Haki zenu kupitia wabunge watakao wawakilisha bungeni kwa hoja zitakazobeba msingi wa CHADEMA. Mimi Don Nalimison najaribu kujenga hoja ya kuokoa jahazi tu. Siku njema na Karibuni Kahama, Shinyanga.

DON NALIMISON.
Kumbe jela ni chuo cha mafunzo!
 

REALNEGRONEVABROKE

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
2,901
2,000
Mimi naamini kabisa kuwa Tundu Lisu ni mtu ambae ametumwa Kuja kuua upinzani Tanzania na hasa chadema take my words

Anaposema wasipeleke wabunge wa viti maalum wakati anajuafika msimamo wa serikali yetu ni Miaka mitano no siasa

Kwa maana hiyo chadema Watakaa Miaka mitano bila kusikika popote hapa Tanzania

Na ndio maana Lisu mwenyewe amesepa na hatorudi Tena Mpaka next uchaguzi,

Chadema wanatakiwa kuwaza Mara mbili
Acha unafiki, umeshasahau aliyesema mpaka kufika 2020 atahakikisha upinzani ameufuta?
Hakuna mwananchi mwenye hofu juu ya kufuta CHADEMA sijui ACT ..hofu na woga mmebaki navyo ninyi msijue cha kufanya kunusuru tril.2 + msizikose .

Upinzani washamwaga mboga sasa,kuleni ugali mtupu au mkipenda kwa chumvi!
 

Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,126
2,000
Wapinzani wamekwamisha maendeleo sasa why mnawalazimisha kuingia bungeni, wapeni police wajaze viti maalumu. Yote haya ni uroho wa tilloni mbili
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,775
2,000
Wabunge 10 wa kuteuliwa wa Magu
1.Queen Sendiga
2.Anna Mghwira
3.James Mbatia
4.Selasini Joseph
5.Lwakatare
6.Hashim Rungwe
7.Aggrey Mwanri
8.Angela Kariuki
9.Ibrahim Lipumba
10.Julius Mtatiro
Mtoto mpendwa Makonda sehemu yake ni ipi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom