Kwa jamii yetu ya Tanzania, wengi wanaweza kufikiri kuwa ni Mu-Islaam.
Ila ukweli unaweza kuwa kwamba, binti ni Mkristo na ndiyo maana kapata nguvu ya kwenda hadi kwa huyo Mwanajeshi (KAFIRI) na kumpa uwa. Kama Watanzania wangelijua kuwa binti ni Mkristo, wasingeliona hata haja ya kuangalia hii picha.
Kwa kijana kama huyo kumwita Muovu au Mbakaji ni DHAMBI kubwa sana maana unamhukumu hata humfahamu. Siyo wote huko ni Wabakaji au Wauwaji. Hawa watoto wa watu nao wanauliwa kama mchwa kila siku kwa amri ya watu wachache wanaotawala White house. Kwa Israel huko ndiyo usiseme maana wao wanakiri kabisa kuwa wanazaliwa kwenye vita, kukulia kwenye vita na kufia kwenye vita na hivyo, vita hawaogopi kabisa.
Kila mtu mwenye busara, inabidi kuwaonea HURUMA hao wote wawili maana wako pale kwa AMRI ya watu kadhaa huko juu yao. Mtoto hawezi kukataa vita maana ni Baba zake, kaka zake ndiyo wanapigana. Kijana hawezi kukataa vita maana ni WAKUU wake juu wameamua. Akikataa na yeye ni Mwanajeshi, hukumu yake inajulikana. Kilichobaki ni kwenda tu.
Wanaoenda huko, wengine ni wale Vibaka, majambazi na kila mijitu yenye tabia mbaya za kila aina. Sasa yakifika huko, usitegemee kutakuwa salama usalimini. Castro wa Cuba alifanya hivyo kwa kumwaga Vibaka wote walioko gerezani na mitaani wakaingia USA. Florida na Miami kukawa na UWANJA wa Majambazi na Vibaka.
Ukisoma pia historia ya NJIA YA MSALABA, utakuta kuwa, watawala wa Europe baada ya kusimamisha vita zao ndani ya Europe, wale Askari na vibaka, walikosa kazi na sehemu ya kwenda. Lilipokuja ombi la kusaidia Wakristo huko Jerusalemu, wakafurahi sana na kuyapeleka haya majamaa. Hii mijitu ilikuwa na tabia mbaya sana na miuwaji isiyo na huruma. Kilichotokea ni kuchinja hadi Kuku walioko ndani ya Jerusalem.
Vita na UBAKAJI ni kama gari linalopita kwenye sehemu ya vumbi, vumbi lazima litimke tu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.