Pichani: NAPE ATINGA MOSHI

Pichani: NAPE ATINGA MOSHI

Katibu wa Itikadina Uenezi wa CCM , Ndugu Nape Nnauye Alikuwa Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya ziara ya kisiasa. Katika ziara hiyo, alifanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Relini, katika kata ya Njoro mkoni humo. Katika ziara hiyo, Nape aliongozana na Juliana Shonza kwa lengo la kumsaidia Nape kufanya kazi maalum.

Miongoni mwa mambo mengine, Nape alisema; "CCM kimeendelea kuwa Chama bora kwa sababu kilijengwa tangu awali katika misingi ya haki na kujali wananchi na kuweka bayana misingi yake ya uongozi." Katika hili watu wengi walipenda Nape afafanue kwamba ni Ipi misingi bora ambayo CCM imejenga na inasimamia hadi sasa ambayo Nape alikuwa akikusudia na ubora wa CCM kwa sasa uko kwenye jambo gani hasa ukizingatia kwamba kwa sasa Viongozi wa chama wamepoteza uadilifu kwa kiwango cha juu kabisa. Hata hivyo Nape haku fafanua lolote na hivyo kuonekana kama mtu anaefavya mzaha.

Nape alisema, baada ya CCM kufanya kazi ya ukombozi na kuwaunganisha Watanzania na kuwa kitu kimoja, sasa kinafanyakazi ya kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuwa kazi hiyo ya ukombozi na kuunganisha watu ilikwisha kamilika kwa ufasaha mkubwa. Hata hivyo hakuweza kufafanua kwamba ni kivipi hadi sasa CCM imeboresha maisha ya Mtanzania wa kawaida.

Nape alisema mji wa Moshi ni miongoni mwa miji iliyowekwa kwenye mpango wa maendeleo.Hata hivyo hakutoa ufafanuzi wa kina juu ya mpango huo aliokuwa akiumaanisha na ni kwajinsi gani mpaka sasa umewasaidia watu wa Moshi, kinyume chake alihama kwa haraka na kuanza kuwalaumu CHADEMA. Katika lawama zake hizo, alisema;
"Hawa Chadema wanawadanganya Moshi, eti kwa kuwa wao ndiyo wenyeHalmashauri kwa hivyo wao ndiyo wameleta maendeleo. Huu ni uongo mkubwa", aliendelea kusema " Mipango yote ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Moshi, ni utekeleza wa ilani ya CCM kwa sababu mipango yote ipo na imeandikwa katika ilani ya chama hicho" .Jambo hili Liliibua maswali ikiwa Nape alikuwa anajua wajibu, majukumu, na mamlaka ya madiwani, wabunge na halimashauri na alikuwa akiwapotosha wananchi wa Njoro kwa makusudi; au naye alikuwa haelewi vizuri mambo haya hivyo akawa anaeleza kwa upeo wake na hivyo kujikuta akiwadanganya wananchi wa Njoro. Mwisho,Nape alimalizia kwa kuwataka waliohudhuria kusimama kwa dakika moja kuwaombea na kuwakumbuka wale wote walioathiriwa na matendo ya CHADEMA japo hakufafanua ni matendo gani,yaliwaathiri kina nani, na ni kivipi CHADEMA ilihusika katika adhari hizo.

Kwa upande wake Juliana Shonza, alipopata nafasi ya kuzungumza, kwanza alianza kuzungumzia suala la tatizo la ajira kabla hajaanza rasmi kuifanya kazi aliyokusudiwa kuifanya. Katika suala hili la tatizo la ajira, Juliana aliwaambia wananchi waNjoro kwamba serikali ya CCM kwa hakika imechukua hatua madhubuti kutatua tatizo la ajira nchini.Akidhibitisha hoja yake kwa mifano ili kuwafanya wananchi wa Njoro, waielewe hoja yake vyema, alisema "Serikali ya CCM imeruhusu bodaboda kuwa usafi rasmi kwa abiria, hivyo kuwapatia vijana ajira na hii inaonesha ni kwa kiasi gani CCM ilivyoj itahidi kutatua tatizo la ajira nchini". Baada ya hoja hii ambayo kimsingi iliwaacha hoi wananchi walio wengi, kwa haraka Juliana alianza kutekeleza lile lililomfanya Nape hata akavutiwa kuongozana na dada huyu hadi mkoa wenye mlima mrefu zaidi barani afrika. Juliana Shonza aliwataka Watanzania kuacha kuwaunga mkono CHADEMA katika mipango yao ya maandamano ya mara kwa mara ambayo yanavuruga nchi. Alikazia hoja yake kwa kusema;
"Vijana jihadharini sana na hawa Chadema, msipumbazike na kugeuzwa asusa zao, maana wao huandaa maandamano ili wawapige picha kisha picha hizo huzipeleka kwa wafadhili wao kwa ajili ya kujipatia fedha, je na ninyi fedha hizo huwa mnapewa" hoja iliyoonekana kupuuzwa na wananchi wa Njoro pengine kwa kuwa walitegemea kusikia hoja za namna hii kutoka kwa mtu huyu.

Hakika kipofu akimuongoza kipofu mwenzie mwishowe wote wataishia kutumbukia shimoni! Watu wa namna hii ni bora wasifanye safari ikiwa hawaoni mbele na hawana uhakika wakule wanakotaka kuelekea.

Last edited by a moderator:
Wananchi wanaojua NA KUELEWA MAMBO lazima watawapuuza tu safi sana wananchi wa njoro.
 
Inaelekea bila Juliana Shonza, mikutano ya Nape haijakamilika!
 
Kwanza ukombozi wa nchi hii haukuwahi kuletwa na CCM bali TANU sema walichokuja kukifanya CCM ni kuifilisi nchi yetu
 
Bodaboda ajira??hizo bodaboda ananunua nani??inamaaana ccm vijana wamekwisha huko mpaka stella mwampamba na juliana shonza kuonekana ni mashuhuri sana???
 
Inabidi mtu uwe na moyo wa mwendawazimu kusimama hadharani na kuzungumza huku ukijua wanaokusikiliza wanakupuuza. Hawa watu lazima wana moyo huo vinginevyo wasinge thubutu hata kidogo.
 
Mimi nachojua mwisho wa hawa vijana ni miezi mitatu ijayo.Nape akiisha watumia sehemu mmbalimbali ya inchi hii kinachofuata ni msoto tu.
 
Viongozi wengi wa CHADEMA siasa wamezijulia ukubwani ndiyo maana kwa kuliona hilo chama kilipewa hela kikajenge chuo cha kuwafundisha siasa lakini hadi leo chuo hakijajengwa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
wale wale wa ukabila na udini badilika,pole sana hachana na mawazo mpauko.
UNAJUA FIKA KITU NINACHOKIONGELEA... nitasimamia ukweli daima hata kama nitabaki peke yangu dhidi ya dunia nzima.. mapenzi na ushabiki hayawezi kunipofusha nikaukataa ukweli ulio dhahiri mbele ya macho yangu....
 
Nape vipi kishamfahamu mazazi wake?
 
Viongozi wengi wa CHADEMA siasa wamezijulia ukubwani ndiyo maana kwa kuliona hilo chama kilipewa hela kikajenge chuo cha kuwafundisha siasa lakini hadi leo chuo hakijajengwa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Kwa hiyo kwa kuwa CHADEMA wamejulia siasa ukubwani; unataka utuambie ndio maana wamekuwa wakifanya siasa za kikubwa kadhalika, ukilinganisha na vyama vingine!
 
UNAJUA FIKA KITU NINACHOKIONGELEA... nitasimamia ukweli daima hata kama nitabaki peke yangu dhidi ya dunia nzima.. mapenzi na ushabiki hayawezi kunipofusha nikaukataa ukweli ulio dhahiri mbele ya macho yangu....

"Vijana jihadharini sana na hawa Chadema, msipumbazike na kugeuzwa asusa zao, maana wao huandaa maandamano ili wawapige picha kisha picha hizo huzipeleka kwa wafadhili wao kwa ajili ya kujipatia fedha, je na ninyi fedha hizo huwa mnapewa" hoja iliyoonekana kupuuzwa na wananchi wa Njoro pengine kwa kuwa walitegemea kusikia hoja za namna hii kutoka kwa mtu huyu.
MKUU HOJA YA COMMENT YANGU ILIJIKITA HAPO!!!
 
nimekuelewa mkuu... lets work hard for the better of our nation..
 
Ok mimi wacha nikubaliane tu na Nape Nnauye kwamba mambo yote yanayofanyika Moshi ni utekelezaji na ni ilani ya CCM, sasa basi swali langu hii ilani inaonekana ni nzuri sana maana Moshi ndio Mji unaoongoza kwa usafi, je Ilani hii hii Dar es salaam haitumiki? maana jirani ya Ikulu tu ndio makao makuu ya uchafu na uvundo.
 
Kwa hiyo kwa kuwa CHADEMA wamejulia siasa ukubwani; unataka utuambie ndio maana wamekuwa wakifanya siasa za kikubwa kadhalika, ukilinganisha na vyama vingine!

Yap! Utekaji watu nyara, ugaidi na maandamano yasiyokwisha.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
haswa hao wananchi wakiwa wanaongozwa na UMANGI... A.K.A UKASKAZINI

single ya udini imeshakolea hadi kumWaga damu,sasa mnajitahidi kuingiza single nyingine ya ukabila halafu mje kutulazimisha tukubali kwamba watunzi na chadema.
Tatizo dhaifu kawaambukiza kutotumia akili.
 
Back
Top Bottom