Pichani Mtoto wa WASSIRA aliyenusurika kuchomwa Moto... ESTER BULAYA alazimika kumuokoa..

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

IMG_1296.JPG
Kambarage Wasira(Kulia)

Mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Jimbo la Bunda Mjini, Ester Bulaya, amesema amemwokoa mtoto wa Waziri wa Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, aliyetaka kuchomwa moto ndani ya nyumba na wananchi kwa madai ya kugawa rushwa.

Bulaya alisema mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Kambarage, alikumbana na mkasa huo juzi kwenye Kata ya Kunzugu eneo la Bukore.

Alisema Kambarage akiwa na baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wengine, wakiwamo watumishi wa Serikali, walifungiwa ndani ya nyumba na wananchi na kutaka kuwachoma moto baada ya kugundua kwamba walitaka kuwapa baadhi ya vijana rushwa ili wafanye fojo kwenye mkutano wake.

Bulaya alisema wananchi wa Bukore baada ya kuwafungia watu hao ndani ya nyumba, kabla ya kuchukua uamuzi wa kuwachoma moto, baadhi yao walimpigia simu ndipo alipochukua askari na kwenda eneo hilo.

Kengete Blog
 
mmmh mbona hawachukuliwi hatuwa hawa unajua ndo wanaotaka kupoteza amani ya nchi then waseme ni vyama pinzani. Huu ukimya wa vyombo vya usalama unatisha sana mbona hawako kazini kabiza au kazi ni kwa vyama pinzani tu.
 
Wassira anatakiwa kumshukuru sana mbunge mtarajiwa wa bunda Esther Bulaya kwa kumsaidia kumwokoa mwanaye kwani ccm mwaka huu wana hali ngumu sana hasa huko majimboni na rushwa huko ccm imeshakuwa ni sera.

TANZANIA MPYA INAKUJA CHINI UTAWALA WA RAISI MTARAJIWA LOWASA.
 
Kweli huruma ya kike ni hasara kuubwa. Sasa, Ester, ulidhani kuwa hilo lijamaa litakuhurumia?? Tangu lini umefundishwa kuokoa mamba kwenye mafuriko?? Huko ndio kwake. Huyu m-ccm hongo ndo lugha yao, matusi ndo salaam zao, fujo ndo usingizi wao unavyopatikana.
Ester, amini usiamini; huyu shukrani yake ni kukutesa mpaka usambaratike. Utajutia huruma yako, ulitakiwa uende baada ya masaa 6
 
mmmh mbona hawachukuliwi hatuwa hawa unajua ndo wanaotaka kupoteza amani ya nchi then waseme ni vyama pinzani. Huu ukimya wa vyombo vya usalama unatisha sana mbona hawako kazini kabiza au kazi ni kwa vyama pinzani tu.
Serikali inavyombo vya usalama wa ccm tu.Kama usalama wa taifa ndo wanatumika kama maroboti kwa masilah ya muda mfupi
 
IMG_1296.JPG
Kambarage Wasira(Kulia)

Mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Jimbo la Bunda Mjini, Ester Bulaya, amesema amemwokoa mtoto wa Waziri wa Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, aliyetaka kuchomwa moto ndani ya nyumba na wananchi kwa madai ya kugawa rushwa.

Bulaya alisema mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Kambarage, alikumbana na mkasa huo juzi kwenye Kata ya Kunzugu eneo la Bukore.

Alisema Kambarage akiwa na baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wengine, wakiwamo watumishi wa Serikali, walifungiwa ndani ya nyumba na wananchi na kutaka kuwachoma moto baada ya kugundua kwamba walitaka kuwapa baadhi ya vijana rushwa ili wafanye fojo kwenye mkutano wake.

Bulaya alisema wananchi wa Bukore baada ya kuwafungia watu hao ndani ya nyumba, kabla ya kuchukua uamuzi wa kuwachoma moto, baadhi yao walimpigia simu ndipo alipochukua askari na kwenda eneo hilo.

Kengete Blog

Halafu kalegea kweli..!
Hivi tatizo ninini cku hizi watoto kuwa legelege kuliko wazazi wao?!
 
Duh kaponaje watu wa bunsda wastaarabu sana chukulia ingekuwa town wangemfanyeje
 
Bavicha bana kwa drama wanakubaliana kila pumba ili muladi iwafurahishe tu.
 
Back
Top Bottom