Picha za Rais zitumike kutangaza bidhaa zetu

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
821
2,070
Na Dr. Christopher Cyrilo anaandika.

Unaona nini?

Unamuona Rais mwenye unyenyekevu na mkuu wa mkoa mwenye unyenyekevu zaidi?
Au mtu mwenye suti ya kijivu aliyeduwaa? Au walinzi wenye 'rain coats'?

Mimi nimeona maandishi juu ya mwamvuli yakisomeka "PRINGLE OF SCOTLAND"
Pringle of Scotland ni kampuni ya mavazi iliyopo Hong Kong, China. Chimbuko la kampuni hii ni Scotland.

Ni ujumbe gani tunapata kwenye picha hii inayomuonesha Rais wa nchi na mwamvuli wenye nembo ya kampuni la mavazi la nje?

Picha ya Rais ni 'icon', inaweza kutumika kutangaza bidhaa za nje bila nchi kunufaika. Lakini ni rahisi kuwa na miamvuli yenye nembo ya Mlima Kilimanjaro, au Seregeti, au mnyama wa Taifa - Twiga, au kitu kingine ambacho kikitangazwa kinaweza kuingiza faida kwa nchi.

Wakati tukifikiria namna ya kuitangaza nchi yetu, na kutangaza utalii wa nchi yetu, tusisahau vitu vidogo kama hivi.

"Inapobidi, picha za viongozi wa nchi zitumike kutangaza bishara zenye manufaa kwa nchi"
Hili si jambo dogo kama baadhi ya watu wanavyoweza kufikiri.

Aliyepiga picha hii ajifunze!


Nawasilisha!
FB_IMG_1618245724515.jpg
 
Kwa Lugha ya picha hapa wote wanaogopana si rais wala mkuu wa mkoa,kwanini inakuwa hivyo au rais hajiamini
 
Katika kosa kubwa alilofanya magufuri kipindi cha uhai wake ni kuchagua mwanamke kuwa makamu wake, sina imani na mwanamke kabisa

Ndio maana ulijizaa!!! Yaani uliachia goli ukajitoa😀😀😀😀

Acha kashfa mzee alafu kibaya zaidi ukute umeoa na unafamilia kabisa na wanakuita baba MBUGILA kama wewe😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom