GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 306
Mkuu nakuunga mkono - kitendo cha kumtoa Mnyika nje ya Bunge kitafanya watu wajadili kauli yake kona zote za Nchi. Kwa jinsi watu walivyopigika kimaisha asilimia kubwa wataunga mkono kauli ya Mnyika na hili litampa umaarufu mkubwa hata maeneo ambako hawakuwa wamewahi kusikia kwamba kuna mwanasiasa anaitwa John Mnyika! Bravo kijana wetu Mnyika!
Absolutely.Mnyika jembe..............................
Akifuta hii kauli. simpikura tena. Hakuna kufuta.
siku hizi unafanya kazi angaza! Uhuru wakusemahauombwi kwa mtu! Ndiyo maana mungu alitupa midomo ni uhuru niliozaliwa nao mie wewena wote!
Tanzania yangu, siasa za vyama vingi hamuziwezi! Ziacheni kama zilivyo na wazifanye wale wanaojua siasa nini maana yake. Huku Majuu watu wanaweza sema lolote kuhusu rais wao iwe bungeni au ktk TV kutokana na UDHAIFU wa kiongozi yeyote yule. Maana ya Upinzani ni pamoja na kuonyesha udhaifu wa kiongozi, chama kutokana na mipango yao ya maendeleo kwa Taifa. Udhaifu wowote ule hauwezi kujengewa kinga ya rais kwa sababu udhaifu ni kipimo cha uwezo wa mtu na unaweza kuepukwa ama kuondolewa.. Ifike wakati tukubali kukosolewa maana JK kweli dhaifu na hatuwezi kumpamba kwa mafuta wakati udhaifu wake upo wazi kabisa.
Mfumu mzima wa UJAMAA ambao unawafanya wananchi na viongozi wengine kuwa vikaragosi wa mkuu wa nchi ktk kujenga Nidhamu ya Woga, ndio kati ya makosa makubwa sana alotuachia Nyerere na siasa za Kikumunist ambazo chama kimoja tu ndicho chenye dhamana na mawazo mbadala ya ujenzi wa Taifa na fikra za mwenyekliti ndizo pekee zenye maana. Waswahili husema - Afichaye maradhi kifo humuumbua.
Maana ya Demokrasia ni kuwepo ushindani na asiyetaka kushindana siku zote hutumia maguvu kuonyesha ubabe hata akiwa ulingoni. Binafsi yangu ningependa sana wabunge wa CCM, spika nawengine wote watueleze vizuri Mnyika alitakiwa kusema maneno gani ili isionekane tusi ikiwa kuna udhaifu umefanyika ktk maandalizi ya bajeti hii. Nani wa kulaumiwa ikiwa sii rais mwenyewe na neno gani lingetumika badala ya DHAIFU.
Siasa za vitisho na ujenzi wa nidhamu ya woga haiwezi kutumiwa kama zana ya kuondoa demokrasia nchini. maadam tumekubali na kupokea siasa za vyama vingi ni muhimu sana na lazima tukubali kwamba kila mmoja wetu ana udhaifu wake na inapotokea kukosolewa tujiandae kutafuta suluhu na sii maguvu ya Ulazima. Nchi yetu inakabiriwa na adui Ujinga, hii ina maana sisi kwa wingi wetu ni wajinga, hatuna elimu yakutosha kuliendeleza Taifa letu. Haya sii matusi bali ni kuelewa mapungufu yetu hivyo tunaiweka nguvu kubwa ktk kuondoa Ujinga na kwa kufanya hivyo tutaweza kuendelea.
Nimesoma ktk mtandao kwani vipi?Mkuu nakuhshimu, umesikiliza bunge la leo?
Pole sana. Ukiwa gamba lazima utaumia sana hata mahali ambapo hustahili kuumia. kisa ni kwa kuwa gamba mwenzio ameambiwa ukweli, na ukweli siku zote unauma. Tuoneshe ni kamusi gani inayosema neno udhaifu (weakness) ni tusi au ni utovu wa nidhani?Nitapasua kioo cha laptop kwa hasira, mtu mzima una utovu wa nidhamu. Aisee inauma sana. watu wamekuchagua ukatoe maneno machafu bungeni?
KIKWEEEEEEEEEEEETEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee CCM JUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUP, JUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUP , JUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUP
Kuna haja ya kutafakari kwa kina kama neno dhaifu ni wakati gani likitumika linaleta tafasiri ya tusi na wakati gani linakuwa na maana ya sifa. Kwa uelewa wangu hakuna binadamu asiye dhaifu labda kama tunaukataa udhaifu wakati tukiishi na udhaifu.
Sasa kama Rais ni dhaifu kiuongozi, hiyo ndiyo sifa yake, ingawa kwa upande mwingine anaweza akawa si dhaifu kwenye mambo mengine.
Kuna haja ya kutafakari kwa kina kama neno dhaifu ni wakati gani likitumika linaleta tafasiri ya tusi na wakati gani linakuwa na maana ya sifa. Kwa uelewa wangu hakuna binadamu asiye dhaifu labda kama tunaukataa udhaifu wakati tukiishi na udhaifu.
Sasa kama Rais ni dhaifu kiuongozi, hiyo ndiyo sifa yake, ingawa kwa upande mwingine anaweza akawa si dhaifu kwenye mambo mengine.
UKisikia ushabiki wa kitoto ndio huu. Hivi sababu ya kusema Rais ni dhaifu na wewe unajua kabisa kutokana taratibu za Bunge utatolewa nje tena ukiwa na hoja za msingi kabisa za kusaidia taifa hili halafu ndiyo kuwa jembe???????? Acheni utoto nyie, hatujamtuma Bungeni kwenda kupoteza muda na kuchukua posho ambazo hakuzifanyia kazi. Yeye ana hoja nzuri kabisa, hivi hawezi kuziwasilisha bila kuvunja kanuni za Bunge. Hii dhana ya kufikiri kwamba kila jambo ni lazima kutumia lugha za matusi, maguvu, vitisho vitaigharimu CHADEMA. Jifunzeni kutoka kwa NCCR na TLP!!!!!!! CHADEMA ni chama ambacho kwa sera karibu kila mtu anavutiwa kujiunga lakini inapofikia wakati wa kupresent hizo sera ndipo shida inapoanzia na ndipo mahali wapinzani wenu watakapojengea hoja za kuwamaliza kama si leo ni kesho. Take care.