Picha za MNYIKA akitolewa nje ya Viwanja vya Bunge

Chenge

JF-Expert Member
Oct 5, 2011
1,073
377
7.jpg

Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka nje ya viwanja vya Bunge la Tanzania leo mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.

3.jpg

Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika akiteta na Mbunge wa jimbo la Wawi Hamad Rashid Mohamed (kushoto) na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo mara baada ya kuondolewa Bungeni leo mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.
1.jpg

Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka katika ukumbi wa Bunge la Tanzania leo mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.
 
Sasa hao wabunge Hamad Rashid na John Cheyo walikuwa nje ya ukumbi kwa nini? Huo ni utoro!!!
 
My simple advise to Mnyika:
Dont let fame get to your head be calm and collected.
Kama una bifu na JK, jaribu kulinganisha notes na Godbless Lema.
Wewe ni mmoja wa vijana wenye akili CDM, dont go to waste!
 
My simple advise to Mnika:
Dont let fame get to your head be calm and collected.
Kama una bifu na JK, jaribu kulinganisha notes na Godbless Lema.
Wewe ni mmoja wa vijana wenye akili CDM, dont go to waste!

Siku hizi unafanya kazi angaza! Uhuru wakusemahauombwi kwa mtu! ndiyo maana mungu alitupa midomo ni uhuru niliozaliwa nao mie wewena wote!
 
msikubali kunenepeana wabunge wa CDM...unene unaleta kufikiri kudogo sana...waandgalieni wenzenu wanavyopata shida kusoma na kutafakari...mengine yamelala tu...ungalia wewe baba mwepesi hata kufikiri baba...CDM juuuuuu
 
Sasa hao wabunge Hamad Rashid na John Cheyo walikuwa nje ya ukumbi kwa nini? Huo ni utoro!!!

Cheyo ni kibaraka wa CCM na mmbeya tu;

Hapo alikuwa anatafuta kujua Mnyika atasema nini ili apeleke kwa waliomtuma.



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
My simple advise to Mnika:
Dont let fame get to your head be calm and collected.
Kama una bifu na JK, jaribu kulinganisha notes na Godbless Lema.
Wewe ni mmoja wa vijana wenye akili CDM, dont go to waste!
Hivi ni vitisho sasa. tena tusitishane kabisaaaaa
 
rais asiyejua kwa nini nchi yake ni
maskini wakat ina raslimaki kibao
huo sio udhaifu??4leni za magari
jijin dsm rais anasema eti hayo ni
maisha bora! Huo sio udhaifu??
Kumteua mgonjwa mahututi kuwa
wa wazir asiyekuwa na wizara
maalumu isiyo na ofc! Huo sio
udhaifu?? Brother mnyika we si wa
kwanza kusema kikwete ni
dhaifu.hata nyerere alishawah
kusema 95 kwamba 'hatumchagui
m2 awe rais kwa sura yake.kwa
sababu haendi kuwa rais wa mamiss
2nataka rais mchapa kazi na
muadilifu'
 
Kama ilifikia hatua hela za kusafiria kwenda nnje ya nchi kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha Ikulu hii pia kwa JK ni UDHAIFU!

Ipo siku si pesa zake tu watamwibia kitu kisichofikiriwa kuweza kutoroshwa. Alivyodanganywa siku zote kufungua hoteli na kesho yake zinabomolewa, magari anayosafiria kutiwa maji badala ya mafuita, sasa kama si udhaifu basi sifa gani apate?
 
Back
Top Bottom