Mungu akisema hapana hakuna wa kusema ndiyo na akisema ndiyo hakuna wa kusema hapana!
Kuna kila dalili kuwa Mungu amesema HAPANA kwa kifo cha Lisu! Japo ilitumika nguvu kubwa (risasi zaidi ya 30) kujaribu kutoa uhai wake lakini Leo bado yuko hai na anaonyesha USO wa furaha bila shaka kuliko ule wa wauaji wake!
Wakijaribu kulazimisha kutoa uhai wake kwa jaribio jingine, wajiandae kupambana na mkono wa Mungu, maana si haki kwa MTU kulipiza kisasi lakini ni haki kwa Mungu kulipizia kisasi wanaoonewa hadi kizazi cha tatu kwa waovu! Ni heri wahusika ("wasiojulikana") wakamwogopa Mungu! Waswahili husema kutenda kosa si kosa lakini kurudia kosa ni KOSA KUBWA!
Kwa jamii ya watanzania, naomba tukubali kusamehe yaliyotokea (maana tusiposamehe haitusaidii) na tumwachie Mungu!