Picha ya mtuhumiwa wa ugaidi Arusha

Picha ya mtuhumiwa wa ugaidi Arusha

MWANA WA UFALME

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2010
Posts
578
Reaction score
144
Nimekuwa nikijaribu kufuatilia picha
ya mtuhumiwa wa ugaidi Arusha bila mafanikio, labda kuna mlio nayo mtuwekee.

kama haipo basi yapo maswali mazito.
Tumeshuhudia picha za watuhumiwa hasa yanapokuja matukio ya kitaifa kama haya. Si tu ndani bali nje ya Tanzania.

Huyu mtuhumiwa ameshasomewa mashitaka 21 mahakamani ila coverage sina uhakika kama imekuwa ya kina ukilinganisha na uzito wa tukio

Kupata taarifa ni haki ya mwananchi na kama taarifa ndogo kama hii haipatikani ni jambo la kushangaza.

Update kwa hisani ya Ndibalema

attachment.php
 
Ndio Ambrose au!?? a victim of a pathetic ............ malizia wenyewe, bado nazipenda kucha na meno yangu..
 
Huyu hapa.
attachment.php

Lol........Balagashia yake iko wapi?

Inawezekana kuwa gaidi bila ndevu, kanzu na kibalagashia?

Au neno "ugaidi" na "gaidi" limefanyiwa ukarabati?

!!!!!!!!!!!!???????????? ***
 
Balagashia yake iko wapi?

Inawezekana kuwa gaidi bila ndevu, kanzu na kibalagashia?

Au neno "ugaidi" na "gaid"i limefanyiwa ukarabati?
Tunamzungumzia 'mtuhumiwa wa ugaidi' na sio 'gaidi'.
 
Tunamzungumzia 'mtuhumiwa wa ugaidi' na sio 'gaidi'.

Niliona FBI walichora "mtuhumiwa wa ugaidi" akiwa na kibalagashia au haukuhitajika mchoro(kibozo) kumtambua mtuhumiwa?

Sisi wengine, tunaweweseka,tunafikiri, tunapata picha kwenye bongo zetu za watu wenye vibagalashia tu tunaposikia mambo ya ugaidi, gaidiz na watuhumiwa wa ugaidi..

Media na usanii wa "SIRI- kali" mkuu imetuchakachua bongo!
 
Mtuhumiwa fake amekamatwa ila bingo ya 50mil ipo pale pale! uonevu dhahiri wanamtesa tu mtoto wa watu innocent kabisa, hajui lolote, amempakia mtu kama abiria wengine, leo anapewa kosa la ulipuaji!

wakubali tu intellijensia ya walipuaji imewazidi akili wao wameizoea ya maandamano!kumshikilia huyo dogo na kumpa makosa 21 yote fake imepunguza ari ya wananchi kuisaidia polisi maana wanaona si watenda haki!hata kanisa linashangaa!!
 
Mkuu kama upo arusha tusaidie kufika polisi na mahakamani kujua mwenendo mzima wa kesi yawezekana ukapata na picha za mtuhumiwa.
 
Niliona FBI walichora "mtuhumiwa wa ugaidi" akiwa na kibalagashia au haukuhitajika mchoro(kibozo) kumtambua mtuhumiwa?

Sisi wengine, tunaweweseka,tunafikiri, tunapata picha kwenye bongo zetu za watu wenye vibagalashia tu tunaposikia mambo ya ugaidi, gaidiz na watuhumiwa wa ugaidi..

Media na usanii wa "SIRI- kali" mkuu imetuchakachua bongo!
Mkuu mbona unaleta utani kwenye mambo ya msingi habari ya zazibar unataka kuihamishia arusha acha utani mkuu.
 
Mkuu tunashukuru kwa kututumia picha ya huyo kijana mkuu.
 
Lol........Balagashia yake iko wapi?

Inawezekana kuwa gaidi bila ndevu, kanzu na kibalagashia?

Au neno "ugaidi" na "gaidi" limefanyiwa ukarabati?

!!!!!!!!!!!!???????????? ***
Mkuu usipende utani kwa kila kitu nadhani tuache vyombo vya kisheria vifanye kazi yake na haki lazima itendeke.
 
Mtuhumiwa fake amekamatwa ila bingo ya 50mil ipo pale pale!uonevu dhahiri wanamtesa tu mtoto wa watu innocent kabisa,hajui lolote,amempakia mtu kama abiria wengine,leo anapewa kosa la ulipuaji!wakubali tu intellijensia ya walipuaji imewazidi akili wao wameizoea ya maandamano!kumshikilia huyo dogo na kumpa makosa 21 yote fake imepunguza ari ya wananchi kuisaidia polisi maana wanaona si watenda haki!hata kanisa linashangaa!!
Awamu hii ya nne watu wengi wemepewa ajira bila ya kuwa na talent/uelewa wowote wa kazi yenyewe. Ajira imekuwa ni sehemu ya kuvuta mishahara na kupiga madili- na yote hii kwa gharama ya walalahoi.
 
Any way hii ni ngumu kweli, na hasa katika maswala haya yanayohusu uchunguzi wa kipolisi. Ndio yale mambo ya kukalia kuti kavu...kama lile la Lulu na Kanumba!

Dogo ndio hivyo tena atasota ndani kweli! Na kama hawatampata mhusika ndio basi tena. Hii inaonyesha ilivyo hatari kwa vijana wanaojitafutia riziki zao kihalali wanavyokumbana na hatari na risk nyingi. Sijui vijana wetu wa boda boda, bajaji na taxi sasa watajilindaje wasijikute wanabeba wahalifu!

Yeye ndie fist lead kwa sasa maana ndie alikuwa na mhusika kabla ya tokeo kutokea regardless alijua au hakujua, alihusika au hakuhusika. Natamani tu haki itendeke kwake na kwa waliohusika.

Ikiwa hakuhusika haki yake isiwe delayed, ichukue kasi ya wale jamaa wa falme za kiarabu walioachiwa huru
 
Any way hii ni ngumu kweli, na hasa katika maswala haya yanayohusu uchunguzi wa kipolisi. Ndio yale mambo ya kukalia kuti kavu...kama lile la Lulu na Kanumba! Dogo ndio hivyo tena atasota ndani kweli! Na kama hawatampata mhusika ndio basi tena. Hii inaonyesha ilivyo hatari kwa vijana wanaojitafutia riziki zao kihalali wanavyokumbana na hatari na risk nyingi. Sijui vijana wetu wa boda boda, bajaji na taxi sasa watajilindaje wasijikute wanabeba wahalifu!

Yeye ndie fist lead kwa sasa maana ndie alikuwa na mhusika kabla ya tokeo kutokea regardless alijua au hakujua, alihusika au hakuhusika. Natamani tu haki itendeke kwake na kwa waliohusika. Ikiwa hakuhusika haki yake isiwe delayed, ichukue kasi ya wale jamaa wa falme za kiarabu walioachiwa huru
Ufanini umekamilika...

quote_icon.png
By Hiroshima
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA MAENDELEO YA UPELELEZI WA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA LA MT. JOSEPH – OLASITI JIJINI ARUSHA LILILOTOKEA TAREHE 05/05/2013

Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba mara ya mwisho nilipokutana nanyi niliwaahidi kwamba nitaendelea kuwapa mara kwa mara taarifa juu ta maendeleo ya upelelezi wa tukio la mlipuko wa bomu lililotokea katika kanisa katoliki la mtakatifu joseph mfanyakazi parokia ya olasiti tarehe 05/05/2013 na kusababisha vifo vya watu watatu(3) na wengine kudhaa kujeruhiwa.

Kama nilivyowaeleza hapo awali, baada ya tukio hilo jumla ya watuhumiwa tisa(9) walikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani. Watuhumiwa haoa ni victor Ambros Kalist, (20), dereva wa bodaboda na mkazi wa kwa Morombo; Yusuph Lomayani Josee (18) mwendesha bodaboda mkazi wa kwa Morombo na George Bathlomeo Silayo (23) mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni raia watatu toka nchi za falme za kiaruabu (UAE) Abdul Aziz Mubrak (30) mfanyakazi wa mamlaka ya mapato katika falme za kiarabu, Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha zimamoto katika Falme za Kiarabu, Saeed Abdulla Saad (28) askali polisikitengo cha traffic katika falme za Kiarabu, pamoja na raia mmoja wa Saudi Arabia Al-Mahri Saeed Mohseens (29)

Rai hao wa kigeni walikamatwa pamoja na wenyeji wao wawili ambao ni raia wa tanzania wenye asili ya Yemen. Majina ya watanzania hao ni Mohamed Suleiman Saad, (38) mkazi wa ilala jijini Dar es Salaam na Jasm Mubarak (29) mkaazi wa mtaa wa Bondeni jijini Arusha.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na timu ya upelelezi ukihusisha taaasis nyingine za upelelezi FBI pamoja na INTERPOL kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani umebaini kuwa raia hao wanne wa kigeni hawakuhusika katika shambulio hilo.

Baada ya jalada la tukio hilo kufikishwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali Arusha – divisheni ya mashtaka imeelekeza kuwa watuhumiwa hao wakabidhiwe ofisi za idara ya uhamiaji mkoa wa arusha ili kuona kama kuna taratibu zozote za kiuhamiaji ziikiukwa na wageni hao wakati walipoingia nchini ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Pia ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imeandaa mashitaka dhidi ya victor S/O Ambros kalisti na amefikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za mauaji na kujaribu kuua. Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa waliosalia unaendelea kwa sasa tunao wataalamu kutoka kenya na Uganda ambao tunashirikiana nao katika upelelezi wa shauri hilo.

Aidha, hadi sasa idadi ya majeruhi wa tukio hilo la mlipuko wa bomu wanaoendelea kupata matatibabu katika hospitali mbalimbali ni 31 ambao kati yao 19 wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa mount Meru arusha, 4 katika hospitali ya St. Elizabeth arusha na wengine 8 katika hospitali ya taifa muhimbili jijini dar es salaam na taarifa zinaonyesha hali zao zinaendelea kuimarika.

Hata hivyo jeshi la polisi linaendelea kufuatilia taarifa za watuhumiwa wengine wanaohusishwa na tukio hilo ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani pia jeshi la polisi linaendelea kuwaomba wananchi au raiayeyote mwenye taarifa zitakazowezesha kubaini mtandao wa kigaidi nawatuhumiwa wengine wanaohusika na tukio hilo wajitokeze na kuwasilisha taarifa hizo; tayari mkuu wa jeshi la polisi (IGP) amekwishaahidi zawadi nono ya Tshs. 50,000,000/= kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa hizo za siri kwa kukamatwa kwa watu hao.


ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
LIBERATUSI SABAS – ACP
TAREHE 13/05/2013.
 
Lol........Balagashia yake iko wapi?

Inawezekana kuwa gaidi bila ndevu, kanzu na kibalagashia?

Au neno "ugaidi" na "gaidi" limefanyiwa ukarabati?

!!!!!!!!!!!!???????????? ***
Akili fupi utazijua tuu..na kungekua na choo humu jf wengi mngekuwa mnaweka mzigo pembeni


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom