Picha ya leo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,139
05_10_8xwpnx.jpg
Licha ya Tanesco kuondoa umeme katika nguzo hii lakini nyanya zake zilizolalia katika nyaya za nguzo nyingine ni hatari kwa usalama wa wapita njia katika eneo la Manzese Midizini Dar es Salaam kama ilivyoonekana jana. (Picha na Mroki Mroki).
 
watalaam ktk idara hii wawe na utalatibu wa kufanya regular inspection itakayowezesha kurekebisha kabla ya hatari kama hii
 
Du hii hatari!!

Hivi Bongo pia bado tuna neno hatari? I doubt si unaona hapo watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida? Nahisi senses za hatari kuanzia serikalini mpaka kwa raia mmoja mmoja zimekufa kabisa otherwise tusingeendesha maisha yetu kimaigizo kama tunavyofanya. Nimeshuhudia ajali ambayo mtu aliungua kama mshikaki na kwisha kabisa lakini dereva wangu hapo hapo eneo la tukio alindesha gari kwa speed ya ndege tulipokuwa tunaondoka eneo la tukio as if keshasahau kuwa speed kills.
 
Ni kutokujali tu wananchi...kama Rais hawajali wafanyakazi na hababaishwi na kura za 319,000 ndivyo nayo Tanesco isivyobabaishwa na kujali maisha ya wakazi Manzese Midizini.
 
Dah ikishuka hapo na kuua utaona Rais nae anaenda eneo la tukio kutoa rambi rambi
 
are you sure?

Hilo la TANESCO kuchukua miezi bila kushughulikia nguzo hiyo siyo swali ndivyo ilivyo. Haya ndo nilolalamikia kwa upande kwa Kilimanjaro kufuatia vifo vya wanakijiji wawili huko Marangu baada ya kugusa waya unaotumika kushikilia nguzo na kumbe ulishaangukiwa na vyaya za mojo juu. Nilitaja pia kuwepo nguzo zilizoliwa mchwa na kuegemea miti mashambani au kuninginia kwa msaada wa nguzo jerani. Mpaka leo yako vilevile. Sasa kama Manzese inawezekana, kwa TANESCO Himo sijui tena.
 
Je wametoa taarifa? Na hali ya hapo wanapokanyaga umepaona? Napo nani anahusika?
 
idara husika kwa maana ya Tanesco wanatakiwa wawe macho
na kazi yao vinginevyo ni hatari:cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::cheer2:
 
Tz kuliko uijuavyo!! hatari kitu gani bana......malaria, ukimwi, kugongwa na magari, kulogwa, kupata ajali ukiwa kwenye gari yote hayo ni hatari...hata hili la ka-nguzo tu mnataka kuita hatazi??!!! sio bongo
 
Bongo hakuna Hatari Nchi imepoteza mwelekeo, Viongozi ndio hao wa mipasho. Wafanyakazi wanadai haki yeye anakuja na mipasho kwa Wadai haki.
 
Back
Top Bottom