Picha ya Kumbukumbu

Picha ya Kumbukumbu

Taarifa ya mwanzo ilisema ni wa kiume wote au nlikosea?! Picha inaongea mengi ila wazazi na walezi wa watoto hao Bwana awafanyie wepesi
 
Inauma saaana ila ndio ishatokea haina jinsi Mungu wapumzishe mahali pema peponi
 
Dah! Mwenyez Mungu mwing wa Rehma, Kwa nin umeyaruhusu haya! Innalillah wainaillah Rajjiun
 
Duh hakika sisi ni waja na kwake tutarejea.
 
Dah!!!Nijuavyo kikawaida watoto wanapendaga safari,so kuanzia usiku wa kuamkia safari wanalala usngizi wa mang'amng'am wakiwaza kukuche tu safari ianze.,lakini hapo kwenye picha yaonyesha hawakua na furaha.,ama kweli MWENYE ENZI MUNGU MUUMBA WETU ametuumba na hisia ya yajayo mbele yetu pamoja na kuwa mara nyingi hatuyatambui moja kwa moja ama hatuyaongelei.
R.I.P watoto wetu wapendwa.
Umeni-pre empty.Walikuwa hawana furaha kabisa.Mambo ya mungu makubwa.
 
Nlivyoona mara ya mwanzo kabla ya kusoma nilidhani hawa ni waliobaki shule baada ya kupata habari ya msiba.
 
Dahh! They didn't know they are going to die!
Tuwaombeeni wadogo zetu waende salama, na wazazi na ndugu Mungu awape nguvu na utulivu
 
Kweli asee hawakuwa na nyuso za furaha hata kidogo! Sio kawaida ya watoto kwa safari kama hizi.
Mungu awape pumziko la milele!
Hebu acha uzushi! Utakuwaje na furaha huku mvua inanyesha ni kibaridi cha arusha kinakutafuna?
 
Mimi nina shida moja hivi tunauhakika gani kuwa kwenye hiyo picha ndo waliopata ajali kwa sababu kwa mujibu wa mmliki wa shule alisema kulikuwa na bus zaidi ya moja. Nafikiri tusubiri tupate official statement tunaweza kutoa pole za watu walio hai.
 
Èe Mungu uliye mfariji, kaa ndani ya mioyo ya ndg, jamaa, wazazi na walezi ukiwafariji kuanzia sasa na milele..... ni hisia zenye maumivu makali sana ambazo hazitafutika kirahisi!
 
Hakika Picha inaonyesha dalili za huzuni
Mwenyezi Mungu aziweke roho zoo mahala pema peponi Amen.
 
View attachment 505465
Kabla ya safari wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent ya Arusha walipiga picha hii. Mungu twakuomba uwasamehe watoto wetu na uwahifadhi mahala pema peponi. Aamiin.
Ukiiangalia hiyo picha ya hao watoto, usoni hawaonekani wenye furaha kwa trip. Miili na roho zao zilikuwa na hisia fulani ambayo haikutafsirika. Mwenyezi Mungu azipokee na kuzilaza roho zao mahali pema
 
Aisee, Paka Jimmy nae kapoteza mtoto? Pole sana kwa wazazi wote waliopoteza watoto wao! Inasikitisha sana!
Ndio mkuu.Arusha wing wametoa tangazo habari na hoja mchanganyiko kueleza yaliyomfika mwenzetu paka jimmy.
 
Back
Top Bottom