PICHA; Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM - Diallo ashinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PICHA; Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM - Diallo ashinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  TUESDAY, OCTOBER 16, 2012

  DIALLO MWENYEKITI MPYA CCM MWANZA, MABINA KUKATA RUFAA KUPINGA MATOKEO .....!!!  [​IMG]
  Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, na mbunge wa zamani wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza, Anthony Mwandu Diallo, ameibuka mshindi kwa kura 611 katika wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, kisha kumgalagaza aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Clement Gregory Mabina aliyepata kura 328.


  [​IMG]
  Pichani Wadau wa uchaguzi wa mkutano mkuu wa mkoa wa mwanza wakijipanga kabla ya uchaguzi huo uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


  [​IMG]
  Wajumbe kupitia utaratibu uliowekwa walijipanga kwenye mistari kwenda kupiga kura kuchagua viongozi nafasi mbalimbali.


  [​IMG]
  Huu ndio utaratibu wa zoezi la kupiga kura katika Mkutano mkuu wa mkoa wa Mwanza.


  [​IMG]
  Kisha unatumbukiza hapa kwenye vyombo hivi vya wazi...


  [​IMG]
  Zoezi gumu la uhesabu kura ukafuata....


  [​IMG]
  Wajumbe wakaserebuka kusubiri matokeo ingawa simu zilizuiwa kuingia kwenye chumba cha kuhesabu kura.. lakini wapi...!! Habari zilipenya, mara tetesi kwa upande wa magharibi wakiwa wamenuna kumaanisha kuwa imekula kwao, nao mashariki wakifunguka kwa matabasamu kumaanisha yaliyomo yamo, ukiuliza aku tunafurahia muziki...tehe-te...


  [​IMG]
  Dj Chris kutoka Semira mobile Sound ndiye aliyekuwa akimwaga burudani kwa wajumbe kuvuta subira kungoja matokeo rasmi kutangazwa....kulikuwa hakuna pombe lakini watu walilewa.


  [​IMG]
  Wakati huo wajumbe wakifuatilia matukio mbalimbali ya mkutano huona habari nyinginezo duniani kupitia g sengo


  [​IMG]
  Mbali na Diallo, wagombea wengine wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, waliotangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na Bunge, William Lukuvi ni pamoja na Zebedayo Athumani (kura 4), Hussein Mashimba (kura15), Joseph Langula Yared (kura 30), na Mabina ambaye alipata (kura 328) wote kati ya kura zote 988 halali zilizopigwa.
  [​IMG]

  Wakati wa kutoa shukurani mwenyekiti aliyekuwa akitetea kiti hicho na kuangushwa Mh. Clement Mabina mbali na kupinga matokeo hayo waziwazi akidai kuwa atakwenda kukata rufaa, ilidaiwa kuwepo kwa mchezo mchafu ambapo mmoja wa wagombea alidaiwa kutoa rushwa ya sh. 50,000 kwa kila mjumbe, kati ya wajumbe wanaokadiriwa kufikia 988, na kwamba inadaiwa kigogo huyo alitumia zaidi ya sh. Milioni 56 kwa lengo la kutafuta ushindi wa nafasi uenyekiti.


  [​IMG]
  Maneno hayo yaliifanya meza kuu kuwa na tafakuri za kina huku minong'ono ya hapa na pale ikitawala... sssssSSSSSsssss!!!... sikiliza kesho Amlifaya na Millard Ayo.


  [​IMG]
  Diallo akitoa neno la shukurani...


  [​IMG]
  Msimamizi wa uchaguzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisimama na kusema kuwa mkutano huo ni halali na umefuata taratibu zote hivyo kama Mabina anadai kuwa si halali kwa vigezo alivyotaja basi akate rufaa na tume ya uchunguzi haito bagua kukagua mgombea anayelalamikiwa tu! bali itakaguwa wagombea wote wa nafasi ya U-enyekiti mkoa.


  [​IMG]
  Viongozi ambao pia ni wajumbe wa mkutano huo toka kada mbalimbali wakifuatilia hitimisho la mkutano huo ndani ya dimba la CCM Kirumba MZ.

  [TABLE="class: tr-caption-container"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Mwenyekiti mpya Dr. Anthony Diallo akizungumza na waandishi wa habari.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Uchaguzi huo ulifanikiwa pia kuwachagua wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza, ambapo waliochaguliwa na wilaya wanazotoka kwenye mabano kuwa ni Mwamba Makune na Christine Mwalu Jilala (Misungwi), Joseph Langula Yared na Marco Mabihya (Sengerema), Stella Aya, Raban Mageje (Magu).


  Wengine ni Angelina Mabula, Dede Swila (Ilemela), Sikitu Sanziyote na Charles Marwa Nyamasiriri (Nyamagana), George Nyamaha na Benadethar (Ukerewe), huku wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza wilaya Kwimba waliochaguliwa ni Bujiku Philip Sakila na Dominic Kadaraja.


  Posted by Albert G.Sengo No comments: [​IMG] Links to this postEmail ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
  [​IMG]
  Mkutano mkuu wa mkoa wa Mwanza 2012 kupitia CCM unaendelea sasa kwenye uwanja wa CCM Kirumba ambapo wajumbe takribani 1015 kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza wanasifa za kushiri uchaguzi huu kumpata Mwenyekiti, Wajumbe mkutano mkuu wa mkoa kwa kila wilaya, Katibu Itikadi na uenezi pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha.

  [​IMG]
  Yote tisa kumi kiu ya wengi wanachama wa CCM na wananchi wa mkoa huu wanasubiri kwa hamu matokeo ya nafasi ya U-enyekiti CCM Mkoa wa Mwanza, kuna wagombea watano ktk nafasi hiyo, na wagombea wanaotajwa na vinywa vya wengi kuitwaa nafasi hiyo ambao ni Diallo na Mabina mbao tangu awali wamekuwa wakipeana vijembe vya chini chini kimtindo. Swali jeh! ni wao au mwingine asiyetarajiwa?
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Wajumbe kutoka Ukerewe.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Wajumbe kutoka Nyamagana.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Wajumbe kutoka Sengerema.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Wajumbe kutoka Kwimba.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi mkoa wa Mwanza mbunge wa Sengerema Mh. William Ngereja akitoa maelezo juu ya taratibu mbalimbali za mchakatomzima unaoendelea uwanjani hapa akiwa meza kuu na Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge Mh. William Lukuvi (katikati) na katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Joyce Masunga.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Mwenyekiti wa CCM wilaya Geita Joseph Kashegu aka Musukuma (kushoto) na Mstahiki meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani Shanslaus Mabula. [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]
  WajumbezZZZ mkutanoni ....

  WAZIRI wa zamani wa Maliasili na Utalii, na mbunge wa zamani wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza, Anthony Mwandu Diallo, ameibuka mshindi kwa kura 611 katika wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, kisha kumgalagaza aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Clement Gregory Mabina.

  Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa CCM Kirumba jijini hapa, ulionekana kuwashangaza baadhi ya wajumbe kutokana na kitendo cha baadhi ya wanafunzi wa kike kutoka katika shule ya Sekondari ya Bwiru ya Wasichana, kuachishwa masomo yao kisha kupewa jukumu la kuhesabu kura za wagombea.

  Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wana CCM na wananchi wa kawaida waliohudhuria uchaguzi huo, walisikika wakilalamikia kitendo cha wanafunzi hao waliokuwa wamevalia sare za shule hiyo, kuachishwa masomo yao shuleni kisha kupewa kazi hiyo ya kisiasa ya kuhesabu kura.

  Mbali na hilo, ilidaiwa kuwepo kwa mchezo mchafu ambapo mmoja wa wagombea alidaiwa kutoa rushwa ya sh. 50,000 kwa kila mjumbe, kati ya wajumbe wanaokadiriwa kufikia 988, na kwamba inadaiwa kigogo huyo alitumia zaidi ya sh. Milioni 56 kwa lengo la kutafuta ushindi wa nafasi mojawapo zilizokuwa zikiwaniwa.

  Mbali na Diallo, wagombea wengine wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, waliotangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na Bunge, William Lukuvi ni pamoja na Zebedayo Athumani (4), Hussein Mashimba (15), Joseph Langula Yared (30), na Mabina ambaye alipata kura 328 kati ya kura zote 988 halali zilizopigwa.

  Awali, wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi walijikuta wakilipuka kumshangilia kwa nguvu kubwa aliyekuwa Waziri wa Naishati na Madini na mbunge wa jimbo la Sengerema, William Ngeleja, baada ya jina lake kutajwa kuwa mwenyekiti wa muda wa uchaguzi huo.

  Uchaguzi huo ulifanikiwa pia kuwachagua wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza, ambapo waliochaguliwa na wilaya wanazotoka kwenye mabano kuwa ni Mwamba Makune na Christine Mwalu Jilala (Misungwi), Joseph Langula Yared na Marco Mabihya (Sengerema), Stella Aya, Raban Mageje (Magu).

  Wengine ni Angelina Mabula, Dede Swila (Ilemela), Sikitu Sanziyote na Charles Marwa Nyamasiriri (Nyamagana), George Nyamaha na Benadethar (Ukerewe), huku wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza wilaya Kwimba waliochaguliwa ni Bujiku Philip Sakila na Dominic Kadaraja.

  ---
  Habari via
  FikraPevu.com

  Source:
  http://www.wavuti.com/#ixzz29Vx9AJct
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mwanza yetu ina Visa; Kwanini CCM Kirumba???
  CCM Vituko kwanini Wanafunzi kuwatoa darasani????
   
 3. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbona hujaweka zile za wanafunzi wa shule wakiwa na uniform zao wakihesabu kura?
   
 4. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  ukiangalia critically sura za wajumbe zote zinaonyesha uovu fulani ulifichika ndani yao, wanajua kwa dhati kabisa wanatetea chama kilichojaa uovu na wapo kwa ajili ya matumbo yao sio kwa maslahi ya taifa kwa ujumla pia wanaonyesha sura za hofu, hofu za anguko kuu hapo 2015 au hata kabla!!
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,467
  Trophy Points: 280
  Kama M/K wa CCM Mwanza ni Dialo, sijui hatima na usalama wa yale majimbo 2 kwa 2015!. Kwa vile Wasukuma sio kabila la "waendekeza njaa", bali ni la "maskini jeuri", then walioichoka CCM, wameichoka!, hata aje nani!, Kanda ya Ziwa gone!.
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Kwani Diallo hana ndoto za kugombea ubunge tena?Mwenyekiti wa Mkoa ni deal sana?kwa karne hii ambayo vijana wameshika hatamu na chama chetu cha vijana kile?au atawaongoza wafu wenzake kisiasa?naona kama wanapambana kwa mapesa kwa nafasi isiyo na tija,wakicheza cheza 2015 watakimbiana baada chama kufanya vibaya sana,hasa kwenye ubunge!Urais najua watatumia nguvu kulinda nafasi yao ya urais isipokwe!
   
 7. Jagarld

  Jagarld JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,534
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Hii nchi,mwanafunzi umtoe darasani aende kuhesabu kura tena za chama! Siasa ifanywe na watu walioamua wenyewe sio kuchukua wadogo zetu mnaweza kujikuta wanaingia kwenye shutma mbaya ambazo ndiyo michezo ya siasa zetu
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  2015 kazi ipo
   
 9. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Sasa rushwa imekuwa ni ya kawaida. Nashangaa wanapoanza kulalama baada ya kutafunwa na rushwa wanayoilea na kuipalilia wenyewe. Bado watalalama wengi.....
   
 10. N

  Nyota Njema Senior Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliyeshindwa Ubunge na kijana Kiwia kwenye Nusu Sunami, atawezaje kuyasimamia Majimbo yote ya Mkoa wa Mwanza kwenye Sunami kamili ya mwaka 2015? Sipati picha!

  Mwaka 2015 ni aibu tupu kwa CCM!
   
 11. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nikiona hayo ma rangi napatwa na hasira sana!
   
 12. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Vipi yule dereva wa kafara ameshazikwa?

  RIP dereva
  Hongera Diallo
   
 13. mjombo's

  mjombo's JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  vizuri km haki ilitendeka ingawa kwa m2 aitwaye dialo kushinda kunanipa wasiwasi coz kwa nn wa2 wenye pesa ndio wawe wanashinda alwayz? daz t min dat ukiwa na pesa ndio unaweza siasa au da z siasa goes simulteneous na utajiri, ninachojjua the ansa z no bt pesa mara zote humanipulate uchaguz na wachaguaj yaani voterz
   
 14. m

  mjuaji Senior Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanza yetu chadema
   
 15. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Kuna watu wapuuzi kabisa, yaani wamekatisha masomo ya wanafunzi (tena wa kike) wakawapeleka kuhesabu kura!
  Halafu yanajifanya kukataza siasa mashuleni, au walimaanisha siasa za vyama vingine nn?
   
 16. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ndio maana wanafunzi wa bwiru girls wana feli sana siku hizi
   
 17. piper

  piper JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Haingii akilini watu wazima kuwatoa wanafunzi darasani ili wawahesabie kura
   
 18. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  CCM Bwana. Ngereja anasimamia uchaguzi, ha ha ha ha ha ha ha haaaaaah ha ha ha ha haaaa haa aaaa
   
 19. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Umeona enhe. hili lazima tulifuatilie kwa karibu zaidi.
   
 20. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Siasa ndani ya CCM hazina mvuto kiasi kwamba yoyote anaweza kushinda sio yeyote tu.
   
Loading...