Picha - Soko Kuu Songea - Nchimbi aibu hii wajiteteaje?

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
soko.jpg


Jambo moja muhimu ambalo linalalamikiwa na watu muda mrefu wabunge kupewa nyadhifa nyingine serikalini na hivyo kutokuwa karibu na wananchi ili kusaidia kuihimiza serikali kuleta maendeleo kwa wananchi. Waziri Nchimbi hapa atatoa utetezi gani, kwani ni mbunge wa Songea Mjini ambako ndiko kuliko hili soko kuu la Songea Mjini na papo hapo ni kiongozi mwandamizi serikalini, je ataendeshaje kofia hizo mbili kwa ufanisi huku zikikinzania na kusababisha maendeleo kudumaa?
 
Mod tupia hii kule inapohusika tafadhali,inatuongezea wingi bure hapa...
 
Mod tupia hii kule inapohusika tafadhali,inatuongezea wingi bure hapa...

Kule songea ambako kuna soko hili wana Mbunge na waziri Nchimbi ambaye wakati wa uchaguzi wa Meya wa Songea alikimbia na sanduku la kura. Ni mwepesi wa kukimbia na sanduku la kura lakini hajali soko kuu ambalo wananchi na walipakodi anaowawakilisha wafanye biashara katika mazingira mabaya na mabovu kama haya. Fikiria inaponyesha mvua nini kinaendelea hapa. Usiku hili si soko tena bali ni kambi ya vibaka.
 
Ndio anayetajwa kwenye mbio za keki kuu

Upendo na uwajibikaji huanzia huko anakowakilisha wananchi, kama hili tu limemshikda kuihimiza serikali kutengeneza mazingira mazuri ya biashara ya walipa kodi, atauweza mfupa wa pale magogoni?
 
Back
Top Bottom