Polisi wengi wanaofanya kazi Arusha pamoja na Traffic wamesikitika sana na wanatengwa na jamii.
Wengi wa Polisi wemepanga mitaani, wanaenda bar za mitaani, wamejenga pia..
Sasa kitendo cha kutumika na Nyinyiem kulipua mkutano wa chadema na kesho yake kupiga mabomu kumewatenga na jamii, wanaonekana kama magaidi.
Polisi wanajieleza sana na kuomba msamaha na kusema wao hawahusika, Polisi walioletwa kutoka Morogoro na Kibaha ndo walitumika.
Huu mtindo wa serikali kuhamisha polisi kwenda kuua mikoa mingine ni cha kukemewa na watanzania wote wapenda amani. Mashirika ya Haki za binadamu na vyama vya wafanyakazi mbona wako kimyaaa??
Kwa mfano chama cha waaalimu, chama cha madaktari, TUCTA, chama cha wanasheria tanganyika, viongozi wa dini, kwa pamoja wakemee vitendo vya polisi kutumika na mafisadi na pia kauli ya PM.
Natoa wito kwa Polisi na JWTZ, wawe wazalendo kama baadhi ya usalama wa taifa, ambao wanasaidia kuvujisha siri za vikao vya kuihujumu CDM.
Mie nashangaa, Polisi akistaafu hapewi hata ukuu wa wilaya, ukuu wa Mkoa ama ujumbe wa board!!!!!.....