PICHA: Nyumba ya Mwalimu Shule ya Msingi Ipyana, Kyela

kinyongo

Member
Oct 13, 2012
39
0

Moja ya nyumba za walimu katika shule ya msingi Ipyana wilayani Kyela mkoani MbeyaHali ya nyumba za walimu katika shule hiyo ni mbaya kama inavyoonekana hapa

Hili ni dirisha lenye kioo cha bati

Picha kwa hisani ya Gordon Kalulunga
 
kinyongo

Member
Oct 13, 2012
39
0
hii ndiyo inaitwa maisha bora kwa kila mtanzania,na nibora pia kwa watumishi wa sekta nyeti kama hiyo
:A S 11:
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,919
2,000
Mimi nadhani Walimu wameridhika na hali hiyo. La sivyo, tusingewaona kila mara wakisimama na ''status quo''
Kila inapotokea fursa ya mabadiliko walimu wamekwenda kinyume nayo!
Kama wanadhani bado ipo nafasi ya kuinua hali zao inabidi kila mara waangalie kalenda.
Ikifika 2015 waseme this is the moment!
 
Nov 14, 2012
13
0
kaka, mimi nadhani walimu hawana mshikamano na pia wanasalitiana wao kwa wao, mwishowe wanaumia wachache...... hapa chakufanya ni wao kuja na mbinu mpya.......yaani watuunge mkono ili katiba mpya iweze kutambua mchango wao na kuwalinda endapo mwajili wao anapokwenda kinyume.
 
CRN

Member
Oct 24, 2012
60
0
Hizo ni miongoni tu mwa nyumba bora kwa watumishi wa serikali,hongereni CCM lakini tunawaomba kila secta ijengewe nyumba za aina hii,kuna watumishi wengine mnawanyanyasa sana kwa mfano Rais,Waziri mkuu,Mawaziri na Manaibu wao,Wakuu wa Mikoa,wilaya nk..,hamtendi haki kabisa,kila mtumishi anataka mahali pazuri pa kuishi,natamani kuwa mwalimu ghafla kulingana na ubora wa nyumba zao jamani,kwa namna hii CCM hata 2015 kura za walimu zote za kwenu.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
78,046
2,000
Hebu pita Lupembe ,Ibungu, Kilasilo ,Mbako , nenda hadi Isaki kajionee uozo wa nyumba za walimu utashangaa ! Au njoo mbele kidogo ya Ipyana , hapa utakuta ile iliyokuwa shule nzuri zamani ya Mpanda, imechoka hadi upepo kidogo tu inayumba , Aibu !
 
chama

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
8,004
0
Mimi nadhani Walimu wameridhika na hali hiyo. La sivyo, tusingewaona kila mara wakisimama na ''status quo''
Kila inapotokea fursa ya mabadiliko walimu wamekwenda kinyume nayo!
Kama wanadhani bado ipo nafasi ya kuinua hali zao inabidi kila mara waangalie kalenda.
Ikifika 2015 waseme this is the moment!

Hakuna kipengele kinachomkataza mtumishi wa umma kupanga nyumba; au kujijengea kama haridhiki na nyumba aliyopewa na mwajiri wake.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
kizaizai

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
3,709
2,000
Hiyo nyumba mbona nzuri sana, ina madirisha, ukuta una plasta, bati, milango ya mbao, hujaona wewe, kuna nyumba za walimu hata mbuzi hakai. Tatizo la nyumba ni kada zote za serikali.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,919
2,000
Hakuna kipengele kinachomkataza mtumishi wa umma kupanga nyumba; au kujijengea kama haridhiki na nyumba aliyopewa na mwajiri wake.
Chama Gongo la mboto DSM
Mwalimu aliyeanza kazi 2011 ana uwezo wa kujenga nyumba?
Nyumba za kupanga zinapatikana huko vijijini kama zinavyopatikana mijini?
 
Kayabwe

JF-Expert Member
Jan 8, 2012
345
225
Walimu wote Serikali ya magamba inawaona kama makondo,wamedanganywa eti wameongezewa mshahara mwezi huu kumbe hakuna kitu,wamejiongezea vigogo tu.Walimu amka 2015 M4C iwe mfumbuzi wa matatizo yenu.
 
chama

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
8,004
0
Mwalimu aliyeanza kazi 2011 ana uwezo wa kujenga nyumba?
Nyumba za kupanga zinapatikana huko vijijini kama zinavyopatikana mijini?
ndio sababu kuna serikali za vijiji; viongozi wa vijiji kwa kushirikiana na wanavijiji husika wanaweza kabisa kutatua tatizo hili serikali kuu haiwezi kuwa kwenye kila kijiji hili ni tatizo ambalo wananchi wenyewe kwa kushirikiana na wabunge wao wanaweza kulifanyia kazi wanakijiji wanaweza kujitolea kufyatua matofali ya kuchoma mbunge akatoa mabati, hali kadhalika wananchi kutoka vijiji wenye vijinafasi hatukatazwi kuchangia maendeleo ya vijiji vyetu. Mkuu Nguruvi3 umeacha siasa na kuwa mwanaharakati turudi kwenye siasa tujenge nchi yetu

ChamaSent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

KASHOROBANA

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,244
1,500
Hakuna kipengele kinachomkataza mtumishi wa umma kupanga nyumba; au kujijengea kama haridhiki na nyumba aliyopewa na mwajiri wake.

Chama
Gongo la mboto DSM

MM WEWE UNA MANENO SANA, IVI ILALA BOMA, G.MBOTO, TUNGI, HAZINA P.SCHOOL N.k. KNA NYUMBA ZA WALIMU APO AU UNAWACHEKESHA WALONUNA? JUU YA KUJENGA NYUMBA IO NI NGUMU, AVERAGE MKOPO ANAOWEZA KUKOPA MWALIMU NOT MORE THAN 4Mn NYUMBA GANI ATAJENGA? IVO OPTN NI KUPANGA ATAJENGA ATAKAPO STAAFU
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,919
2,000
ndio sababu kuna serikali za vijiji; viongozi wa vijiji kwa kushirikiana na wanavijiji husika wanaweza kabisa kutatua tatizo hili serikali kuu haiwezi kuwa kwenye kila kijiji hili ni tatizo ambalo wananchi wenyewe kwa kushirikiana na wabunge wao wanaweza kulifanyia kazi wanakijiji wanaweza kujitolea kufyatua matofali ya kuchoma mbunge akatoa mabati, hali kadhalika wananchi kutoka vijiji wenye vijinafasi hatukatazwi kuchangia maendeleo ya vijiji vyetu. Mkuu Nguruvi3 umeacha siasa na kuwa mwanaharakati turudi kwenye siasa tujenge nchi yetu
Chama Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Kuumbe! hata mimi kwa kiasi fulani ninaelewa ulivyoelewa. Ninatatizika pale serikali iliyopo madarakani inapotoa ahadi za kuwajengea nyumba kila karibu na uchaguzi.
Mkuu Chama umeiwahi kuipitia pitia ilani ya uchaguzi ya CCM.

Kuna siku nilimsikia rais akisema ujenzi wa shule za kata uambatane na ujenzi wa nyumba za walimu. Hapo ndipo nikajua serikali kuu kumbe nayo ina mchango katika hili. Sijui kama ni sahihi au la, ninachojua ni kuwa walimu wanatumika sana kisiasa.

Halafu kuna ahadi ya rais ya kujenga nyumba 4000. Anyway tuhimize halmasahuri na vijiji pamoja na wananchi wajenge nyumba, halafu tukataze wanasiasa wasiwatumie Walimu kama vifaa vya maliwato mtu anavyovitupa na uchafu akishajisafisha.
 
chama

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
8,004
0
Mkuu Nguruvi3
politicians don't tell the truth, they don't lie either, kauli za wanasiasa inabidi wewe msikilizaji uzipime, politicians always find the way to meet in the middle to compromise! Turudi kwenye walimu wanajichezea wenyewe; wao wanakubali kutapeliwa na viongozi wao wa union; unakumbuka mgomo wa walimu? Ule ulikuwa utapeli mtupu wa viongozi wao nasikia walitumia zaidi ya milion 100 kuhamasisha mgomo hivi kweli unahitaji kutumia kiasi hicho cha pesa kuhamisha kudai haki hako? Raisi aliahidi kujenga hizo nyumba 4000 si lazima azimalize zote wakati wa muhula wake hiyo ipo kwenye mipango ya maendeleo ya serikali, nyumba za vijijini sisi wenyewe wazaliwa wa sehemu husika tunaweza kufanya mabadiliko bila kuihusisha serikali kuu.

Chama

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom