Moja ya nyumba za walimu katika shule ya msingi Ipyana wilayani Kyela mkoani MbeyaHali ya nyumba za walimu katika shule hiyo ni mbaya kama inavyoonekana hapa
Hili ni dirisha lenye kioo cha bati
Picha kwa hisani ya Gordon Kalulunga
kijijini utapata wapi nyumba za kupanga na shule zilivyo mbali kwanza kwa mshahara gani?
View attachment 72892
Ofisi ya CCM Chamakwaza, Chalinze: Kama ofisi ya hama tawala iko hivi, unatarajia nyumba ya walimu iweje? Tafakari!!
K
Moja ya nyumba za walimu katika shule ya msingi Ipyana wilayani Kyela mkoani MbeyaHali ya nyumba za walimu katika shule hiyo ni mbaya kama inavyoonekana hapa
Hili ni dirisha lenye kioo cha bati
Picha kwa hisani ya Gordon Kalulunga
Moja ya nyumba za walimu katika shule ya msingi Ipyana wilayani Kyela mkoani MbeyaHali ya nyumba za walimu katika shule hiyo ni mbaya kama inavyoonekana hapa
Hili ni dirisha lenye kioo cha bati
Picha kwa hisani ya Gordon Kalulunga
Aisee kuna watu wengine hawaishi Tz so wasamehe tu..!!Mwalimu aliyeanza kazi 2011 ana uwezo wa kujenga nyumba?
Nyumba za kupanga zinapatikana huko vijijini kama zinavyopatikana mijini?
ndio sababu kuna serikali za vijiji; viongozi wa vijiji kwa kushirikiana na wanavijiji husika wanaweza kabisa kutatua tatizo hili serikali kuu haiwezi kuwa kwenye kila kijiji hili ni tatizo ambalo wananchi wenyewe kwa kushirikiana na wabunge wao wanaweza kulifanyia kazi wanakijiji wanaweza kujitolea kufyatua matofali ya kuchoma mbunge akatoa mabati, hali kadhalika wananchi kutoka vijiji wenye vijinafasi hatukatazwi kuchangia maendeleo ya vijiji vyetu. Mkuu Nguruvi3 umeacha siasa na kuwa mwanaharakati turudi kwenye siasa tujenge nchi yetu
Chama
Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
ndio sababu kuna serikali za vijiji; viongozi wa vijiji kwa kushirikiana na wanavijiji husika wanaweza kabisa kutatua tatizo hili serikali kuu haiwezi kuwa kwenye kila kijiji hili ni tatizo ambalo wananchi wenyewe kwa kushirikiana na wabunge wao wanaweza kulifanyia kazi wanakijiji wanaweza kujitolea kufyatua matofali ya kuchoma mbunge akatoa mabati, hali kadhalika wananchi kutoka vijiji wenye vijinafasi hatukatazwi kuchangia maendeleo ya vijiji vyetu. Mkuu Nguruvi3 umeacha siasa na kuwa mwanaharakati turudi kwenye siasa tujenge nchi yetu
Chama
Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
My take: Bado tunashawishika kuwa serikali haina pesa za kujenga nyumba za walimu.KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya toleo lililopita la gazeti hili, tuliona jinsi Kampuni ya kifisadi iitwayo "Meremeta" ilivyoundwa bila kusajiliwa, mahsusi kwa ajili ya kukwapua mabilioni ya fedha kutoka nchini kupitia Benki Kuu (BoT) kwa ushirikiano wa watumishi wa ndani ya nchi na mafisadi wa nje, na kufanikiwa kukwapua zaidi ya shilingi bilioni 155. Tuendelee na sehemu hii ya leo.Kutokana na Kampuni ya Meremeta kujitangaza "mufilisi", lakini baada ya kukomba dhahabu zote za Buhemba, Buhemba Kusini, Nyamongo na Magunga, mbali na kukwapua bilioni 155/= kutoka Benki Kuu, iliundwa tume ya watu watano kuchunguza kampuni hiyo na kutoa mapendekezo serikalini.
Tume hiyo ilipendekeza kusitishwa shughuli za Meremeta, kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo, jukumu ambalo hata hivyo tayari ilikwishalitelekeza tangu mwaka 2003, na kujiingiza yenyewe katika uchimbaji na umiliki wa migodi niliyoitaja hapo juu.
Tume ilipendekeza pia kuanzishwa kampuni mpya ya kusimamia na kuendesha Mgodi wa Buhemba itakayomilikiwa na serikali tu.
Na kwa uzito wa mapendekezo ya tume hiyo ya Balali na wenzake tuliowataja hapo mwanzo, Meremeta ilifilisiwa, mali na madeni yake yalichukuliwa na Kampuni mpya ya "Tangold," inayodaiwa kumilikiwa na serikali, pia asilimia kwa 100. Na ingawa Meremeta (halisi) ilifungwa rasmi mwaka 2006 nchini Uingereza, shughuli zake hazikukoma nchini Tanzania wakati huo, kama tutakavyoona baadaye katika makala haya.
Hapa kuna utata mwingine, kwamba kumbukumbu zinaonesha kuwa, Kampuni ya Tangold ilianzishwa katika Visiwa vya Mauritius, Aprili 4, 2005; na kupewa Leseni ya Biashara Aprili 8, 2005 kama Kampuni binafsi. Lakini kumbukumbu nyingine zinaonesha kuwa, Tangold ilifungua Akaunti ya Benki Namba 011103024852, Tawi la Corporate Drive la NBC, Dar es Salaam, Januari mosi, 2003; kabla hata Tume ya Balali na wenzake haijaundwa kutatua tatizo la Meremeta.
Taarifa nyingine zimeonesha zaidi kuwa, Kampuni hiyo ni ya kigeni iliyosajiliwa nchini Mauritius na kupewa leseni nchini Tanzania, Februari 20, 2005 kama tawi la Kampuni ya kigeni; na ilianza kupatiwa fedha na BoT Agosti mosi, 2005 kwa kazi isiyojulikana.
Je, hii ina maana Tangold ilikuwapo Tanzania kabla ya kuanzishwa nchini Mauritius mwaka 2005, au ni aina fulani tu ya usanii? Hata kama ilikuwapo, iliwezaje kufungua Akaunti Benki, Januari mosi, 2003 ambayo ilikuwa Sikukuu ya Kitaifa ya Mwaka mpya? Kama ilikuwapo, kwa nini Tume ilipendekeza kuundwa kwa kampuni ambayo tayari ilikuwapo? Nini tofauti kati ya Tangold iliyofungua Akaunti Januari 2003, na Tangold iliyosajiliwa Mauritius April 4, 2005 kurithi Meremeta?
Ingawa mapendekezo ya Tume na tamko la Serikali yalikuwa kwamba, Tangold imilikiwe asilimia kwa mia na Serikali, utekelezaji wake ulikuwa kinyume chake, inaelekea wajumbe wa Tume iliyochunguza matatizo ya Meremeta, ndio hao hao waliogeuzwa au kujigeuza kuwa wakurugenzi wa kampuni hiyo mpya. Hao wanatajwa kuwa ni Daudi Balali, Gray S. Mgonja, Andrew Chenge, Patrick J. W. Rutabanzibwa na Vicent F. Mrisho.
Inawezekana, kwa mtazamo wa enzi hizo na kwa kusudio hilo, kwamba hao watano ndio walikuwa serikali yenyewe. Lakini kifungu cha saba cha Katiba ya ya Tangold kinatibua dhana yote hiyo, kinaposema, "Wenye hisa ya kampuni wanaweza kurithisha hisa zao kwa ndugu zao".
Je, ni kweli Tangold ilimilikiwa na Serikali asilimia mia kama ilivyopendekeza Tume ya Balali na kwa mujibu wa tamko la Serikali? Ni ndugu wapi hao wa serikali [kama kweli serikali ina ndugu binafsi!) waliostahili kurithishwa hisa za Serikali?.
Haya ni maswali magumu, na tunashawishika kuamini kwamba, huenda Tangold haikumilikiwa na Serikali asilimia mia; bali ilikuwa kampuni binafsi iliyorithishwa mali za Kampuni ya Meremeta.
Wakati matatizo ya Meremeta yakiendelea, na wakati huo huo tayari mapendekezo ya Tume ya Balali ya watu watano yakiwa yameanza kufanyiwa kazi; Machi 18, 2004 iliundwa Kampuni nyingine iitwayo "Deep Green Finance" [DGF], ambayo madhumuni na shughuli zake hazijafahamika vizuri mpaka sasa. Wakurugenzi wa DGF walikuwa ni Mark Ross Weston wa New Zealand; Antón Taljaard wa Afrika Kusini na Rudolf Van Schalkwyk, pia wa Afrika Kusini.
Wanahisa wa DGF walitajwa kuwa ni Protase R. G. Ishengoma, Stella Ndikimi wa Kampuni ya uwakili ya IMMA, ya jijini Dar es Salaam; Benki ya Nedbank Africa Investment Ltd ya Afrika Kusini (ambayo Mshauri wake, Michael G. Garner, ndiye pia alikuwa Mshauri huru wa Tume ya Balali yenye watu watano, iliyochunguza matatizo ya Meremeta na kupendekeza kuundwa kwa Tangold), na Kampuni ya SBM Nedcor Holdings, ambayo haijafahamika bado, kama ina uhusiano wowote na Kampuni ya Nedcor Trade Service, iliyolipwa na BoT malipo tata ya zaidi ya Sh. 155 kwa niaba ya Meremeta.
Wakurugenzi hao watatu wa Deep Green Finance, ndio waliokuwa Ma-Afisa pia wa NedBank; na jina la Deep Green limetumiwa mara nyingi na NedBank katika miradi yake mingine ya kijamii. Haifahamiki pia ni kwa vipi na kwa njia ipi, Watanzania wawili pekee, Protase Ishengoma na Stella Ndikimi, walitembelewa na bahati ya kununua hisa za kampuni yenye kumilikiwa na wageni kama hii (DGF); na kama ni kweli inavyodaiwa, kwamba hatimaye walichukua hisa (kwa njia ya kuhamishia au kununua) katika Nedbank Ltd na Nedbank Africa Investments, hapo Aprili 15, 2004.
Kama ilivyokuwa kwa Kampuni ya Tangold, iliyofungua Akaunti siku ya Sikukuu ya mwaka mpya; ndivyo ilivyokuwa kwa Kampuni ya Deep Green Finance, iliyofungua Akaunti Benki ya NBC, Na. 011103024840, tawi hilo hilo la Corporate Drive; safari hii ilikuwa Sikukuu (ya mapunziko) ya Mei Mosi, 2004.
Kuna utata pia kuhusu utoaji wa namba za Akaunti za Benki hiyo kwamba, Akaunti ya Tangold, Namba 011103024852, iliyofunguliwa Januari mosi, 2003, ni kubwa (kwa Akaunti 12 zaidi,011103024852 – 011103024840), ikilinganishwa na Akaunti Namba 01110302840 ya Deep Green Finance, iliyofunguliwa zaidi ya mwaka mmoja baadaye, Mei mosi, 2004. Je, ni utaratibu wa NBC kutoa namba za Akaunti kuanzia na namba (kubwa) za juu, kushuka chini? Kama sivyo, basi kuna walakini mkubwa kutufanya tuamini kwamba kulikuwa na mchezo mchafu, ikizingatiwa pia kwamba akaunti zote mbili zilifunguliwa siku za mapumziko ya Sikukuu za kitaifa.
Tangu Mei mosi, 2004 akaunti ya Tangold ilipofunguliwa, hadi Julai 31, 2005 (zaidi ya mwaka mmoja), hapakuwa na shughuli za DGF zilizoingiza fedha katika akaunti hiyo; hadi Agosti mosi, 2005 ilipoanza kupokea mabilioni ya fedha kutoka ama BoT, Deep Green Finance au Tangold, kwenda ama Deep Green Finance, Tangold, Meremeta, IMMA Advocates ya Dar es Salaam, au kwingine kusikojulikana.
Wakati imeelezwa Tangold ilianzishwa Aprili 5, 2005 na kupewa leseni ya biashara Aprili 8, 2005 kuchukua nafasi ya Meremeta, na mali na madeni ya Meremeta kuhamishiwa au kuchukuliwa na kampuni mpya kwa maana kwamba Meremeta ilikuwa imefilisiwa na kufungwa; lakini kumbukumbu zinaonesha kwamba, Oktoba 12, 2005, jumla ya Shs. 1,690,500,000 zilihamishwa kutoka Tangold kwenda Kampuni (mfu?) ya Meremeta; na vivyo hivyo Novemba 23 (Tshs. 555,300,048), na Desemba 12 (Shs. 551,060,000). Iliwezekanaje Meremeta kulipwa fedha hizo wakati ilikwishafilisiwa? Nani aliifufua na kwa utaratibu gani?.
Kwa kifupi, kati ya Agosti mosi, 2005 na Desemba 21, 2006, jumla ya Sh. bilioni 32 zilihamishwa kutoka Benki Kuu kwenda Deep Green Finance na Tangold; mbali na zile zilizopelekwa kusikojulikana. Tunashawishika kuamini, Deep Green Finance iliundwa kurahisisha na kuhakikisha utoroshaji wa fedha za Meremeta na Tangold kwenda nje ya nchi, na si kwa sababu nyingine yoyote ile.
Baada ya purukushani hizo, na kuonekana kwamba Mradi wa Tangold hauwezi kuendelea; Serikali iliuza haki za Mgodi huo kwa Kampuni ya "Rand Gold" ya Afrika Kusini, kwa bei ya chini ya soko, na kusababisha kwa Serikali hasara ya dola za Marekani milioni 100; na pia Serikali kutakiwa kulipa dola miliono 132 (adhabu na riba), kutokana na Serikali kudhamini wakopaji/wawekezaji waliofilisika, na hivyo kuachiwa mzigo wa kulipa madeni hayo ya kitapeli.
Huku ikielewa fika juu ya uporaji wa madini na ukwapuaji wa zaidi ya Shs. 55 uliofanywa na kampuni hizo za kitapeli; Serikali ya awamu ya tatu ilikubali na kuridhia "hasara" ya dola milioni 232 (Sh. bilioni 232) kwa Kampuni hizo. Na kwa kasi ya kushangaza na ya kutisha, Serikali hiyo ililipa madai hayo Oktoba 2005, mwezi mmoja tu kabla ya kumaliza muda wake wa kuwa madarakani.
Kwa hiyo, wanaodai kwamba kashfa ya Meremeta haizungumziki, eti kwa sababu inagusa mambo ya Usalama wa Taifa, ni waongo. Tunawataka wajichunguze kwanza kabla ya kusema, kisha watueleze hayo wanayatoa wapi; vinginevyo tutawahesabu wasaliti wa Taifa letu.
Wakati huo huo, ni maoni sahihi kwamba hoja ya Zitto Kabwe, juu ya kukwapuliwa kwa Sh bilioni 155 (pia Sh. bilioni 232) na kutoroshewa kwenye benki za nje ya nchi, ina uzito na mantiki ya kutosha. Kujaribu kuzuia au kuteka nyara hoja hiyo, ni kujipambanua au kujitangaza "adui wa umma" wa Kitanzania
umeena vyema kakaElimu kwanza CCM baadaye, hata ofisi zao zikichakaa hakuna tatizo
Hakuna kipengele kinachomkataza mtumishi wa umma kupanga nyumba; au kujijengea kama haridhiki na nyumba aliyopewa na mwajiri wake.
Chama
Gongo la mboto DSM
Mkuu Nguruvi3, usishangae kuona hii post yako wakina chama wanaikwepa kama vile hawaioni...ndivyo walivyo! CCM inapofusha macho, inadumaza akili na kulemaza viungo. Hebu fikiria mtu na akili zake timamu leo hii anathubutu kuisifia CCM kwa kuzaliwa upya kwa kupata viongozi wapya! Akina nani hao? Mang'ula, Kinana, Meghji na wengineo, duh!Zakumi, sidhani kama kuna tatizo lolote kuifanya elimu yetu iwe ya ubora unaohitajika.
Na wala sidhani kuwa kuna umuhimu wa mwananchi anayelipa kodi sasa hivi kuchangia kwa kiasi hicho.
Tatizo letu kubwa ni kukosa nidhamu, kutowajibika, kutowawajibisha na kuogopa mabadiliko.
Miaka 50 baada ya uhuru bado tunahemea nje kwenye misaada hatujaweza ku-balance bajeti hata siku moja.
Miaka 50 baada ya uhuru bado serikali iliyopo inakusanya kodi kutoka katika vocha za simu, bia na sigara.
Haihitaji akili ya ziada kubaini kuwa ubunifu umefika mwisho na tunahitaji ubunifu mwingine.
Real? vocha ya simu ndiyo source of income kwa taifa lililojaa utajiri kama letu.
Mkuu Zakumi, pitia hesabu za CAG uone kiasi kilichopotea ndani ya miaka 10 kama si sawa na bajeti ya mwaka mzima ya nchi. Pitia matumizi ya serikali katika miaka 10 uone pesa za kufanya dhifa za kitaifa, makongamano ngurudoto na upuuzi mwingine halfu upate mahesabu.
Pitia wizi unaotokana na madini katika migodi kwa miaka 5 iliyopita.
Nenda bandarini kaangalie ukwepaji kodi kwa miaka 5 iliyopita.
Na mwisho pitia hazina uone pesa zinazopotea bila kujulikana, nenda BoT na kwingine ujionee miujiza.
Wakati hayo yakitokea bila majibu wala kuonyesha kushtuka tunaye Rais, Makamu na Waziri mkuu achilia majuha wengine. Wao afya zao zinachekiwa Uingereza na wana mafaili yao Appolo.
Si unajua ni kiasi gani kinatumika kutibu waheshimiwa kule India, South na UK.
Linapokuja suala la Walimu hilo tunaambiwa si tatizo la kitaifa. Piga mahesabu ya vitu nilivyokutajia hapo juu halafu uniambie ingechukua muda gani kujenga nyumba za Walimu.
Hatuhitaji kitu cha ziada, tunahitaji Viongozi wenye akili timamu ya kupanga na kusimamia nidhamu
Kuwaahidi walimu katika ilani ya uchaguzi halafu kuwaacha njia panda ndio theory ya kuwatumia kama toilet paper! nitty gritty.
Hatuwezi kuondoka hapa tulipo tukiendekeza hili genge la wahalifu lililopo.
Kama yupo mwendawazimu anayetaka kuongoza nchi hii mwenye mtizamo na fikra, hata kama nitaambiwa tatizo lake limetulizwa na dawa nitampa kura.
Hatuwezi kuwa na wahuni kwa miaka 50 halafu tusubiri matokeo tofauti.
Tumeambiwa kuwa kuna wizi umetokea, eti leo serikali inafanya kazi kwa kutumia tafiti za Zitto.Ni uhuni tu.
Sasa huyu anaweza kusimamia elimu kweli!
I know inauma sana lakini tuweni wakweli wa nafsi zetu. Tusidhulumu nafasi zetu kwa kujifanya hatusikii wala kuona. Tunajidanganya na kujifanya wapumbavu na wajinga bila sababu.
Huwezi kukamua kodi ya mkulima anyeishi kwa dola moja kwa siku ili iende kutibu watu Appolo, kusomesha watoto Cambridge na upuuzi mwingine, halafu tumshauri mkulima huyo huyo alipe kodi nyingine.
Tusijifanye wajinga huku tukielewa kuwa huwezi kumfunza mbwa mzee mbinu mpya.
Kufanya jambo lile lile kwa namna ile ile na watu wale wale kwa miaka 50 ni ujinga uliokithiri.
Ninarudia, hata kama mkoloni ataonyesha interest za kurudi, ili mradi kufanya hivyo kutaiondoa CCM madarakani nitakwenda uwanja wa ndege kumpokea nikiwa na matawi ya majani.
Endapo sitafanya hivyo, basi itabidi niwaombe walimu radhi kwasababu nami pia nitakuwa nimetumika kama toilet paper. Sipo tayari! Nimejifunza kutoka kwa walimu na ni kosa kurudia kosa.
Sitaidhukumu nafsi yangu wala kuidhalilisha akili yangu kwa kuamini kuwa baada ya miaka 50 kuna kipya kitatokea.
Tatizo kuna watu wamezaliwa upanga na wakakulia hapo maisha yao yote, kwa wao ni vigumu kujua hali zetu za vijijini zikoje ndiyo maana wanashauri walimu wapange nyumba