PICHA: Ndege mpya za Fastjet hizi

Naam, ndege imeenda shule hii. Kitu kimetulia. Ni jet engine. Yale mapanga shaaaa hata kwa bure sipandi.
Kwa kauli hizi inainekana ata ndege kupanda ni mpaka upate offer...kwani precision wanatumia ndege gani..mbona watu wanapanda ili hali nauli zao zipo juu...
 

Tatizo kubwa la ATCL, kama mashirika mengine ya umma, ni gharama za uendeshaji upande wa mishahara ya waajiriwa:
1) Ajira kutolewa nyingi na kiholela ili tu kuhakikisha ndugu wa mabosi wanaotoka vyuoni hawakosi ajira! Utakuta mtu ameishapangiwa kitengo kabla hata hajaenda chuoni kusomea taaluma husika!
2) Mishahara mikubwa, maradufu, kuzidi hali halisi kiasi hata cha kuweza kumvutia mmiliki wa ndege binafsi kuacha biashara ya ndege na kutafuta ajira ya ATCL, maana huko maisha ni rahisi zaidi!
3) Kuzifanya mpaka ajira za muda mfupi kuwa ajira za kudumu na kuzidi kulitwisha shirika mzigo!

.
.
.


Matokeo yake ni shirika kushindwa kujiendesha kiasi cha kuhitaji ruzuku ya serikali kulipa mishahara!
 
Hii serikali wangekua wasikivu wasingenunua ndege bali chanjo hospitali. Wamekosea vipaumbele sasa majanga yameanza.
 
Semeni msemavyo.... ndege ni zetu.Heri tisa kibindoni kuliko kumi nenda urudi.Tumeanza na hizo na tutafanikiwa tu..kwani penye nia pana njia.Inshaalah...
 
Wazo lako ni la msingi sana mkuu.Ubarikiwe kwa maoni yako ya kizalendo.
 
Asante sana
 
Kaka hata ziwe ndege 100,haziwezi kuwa mbadala wa Yutong,nauli itabaki kuwa expensive, umeona hee walete wataalam wenye weledi co kuchukua makada tu kama walivyofanya kwa TTCL.
 
Profesa Mbarawa ameitaka Bodi hiyo kuipa ATCL mifumo imara, makini na mahiri ili kuweza kutatua changamoto zinazoikabili Shirika hilo ikwemo wizi wa mafuta ya ndege na upotevu wa mapato.

Ili kupima ufanisi wa utendaji wa Shirika hilo Profesa Mbarawa ameitaka Bodi hiyo kuandaa mkataba kwa kila mfanyakazi kuanzia ngazi ya juu hadi chini.

Katika hatua nyingine Waziri Mbarawa amesema kuwa Serikali ina mpango wa kununua ndege mbili mpya aina ya Jet ifikapo mwaka 2017 kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji wa anga nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…