PICHA na HABARI; Maalim seif ahutubia bububu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PICHA na HABARI; Maalim seif ahutubia bububu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 25, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Monday, September 24, 2012  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wafuasi na wapenzi wa Chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika kiwanja cha Kwa Geji, kijichi jimbo la Bububu.
  [​IMG]
  Wafuasi na wapenzi wa CUF wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad katika mkutano wa hadhara uliofanyika kiwanja cha Kwa Geji, kijichi jimbo la Bububu.
  [​IMG]
  Wafuasi na wapenzi wa CUF wakishangilia wakati Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kiwanja cha Kwa Geji, kijichi jimbo la Bububu.
  [​IMG]
  Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Ismail Jussa Ladhu akizungumza na wafuasi na wapenzi wa Chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika kiwanja cha Kwa Geji, kijichi jimbo la Bububu.
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Ismail Jussa Ladhu (kulia0, aliyekuwa mgombea wa uwakilishi jimbo hilo Issa Khamis Issa (kushoto), pamoja na wasomaji wa utenzi mara baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika kiwanja cha Kwa Geji, kijichi jimbo la Bububu.
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wafuasi na wapenzi wa Chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika kiwanja cha Kwa Geji, kijichi jimbo la Bububu.

  Na Salma Said

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif amesema watu wasioitakia mema Zanzibar wasipewe nafasi kuvuruga umoja wa Wazanzibari ulioimarika baada ya maridhiano ya kisiasa yaliyopelekea kuundwa kwa mfumo wa serikali yenye muundo wa umoja wa kitaifa.


  Amesema serikali inapaswa kuwa makini na watu hao, na kwamba iwapo viongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa wataendeleza nia njema ya kukuza umoja na mshikamano, watu hao hawatokuwa na nafasi wala njia ya kupita kupenyeza matakwa yao dhidi ya umoja wa Wazanzibari.

  Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ametoa kauli hiyo katika viwanja vyaKwa Geji Kijichi jimbo la Bububu, alipokuwa akizungumza na wafuasi na wapenzi wa Chama hicho kwenye mkutano wa hadhara, uliolenga kuzunguzia matukio na matokeo ya uchaguzi wa Bububu uliofanyika hivi karibuni.


  Amefahamisha kuwa Wazanzibari wanapaswa kuwa wamoja katika kutetea maslahi ya nchi yao, na kuweka wazi msimamo wake wa kutetea muundo wa Muungano wa Mkataba, ambao itaziwesha nchi mbili zilizoungana kuwa na mamlaka kamili kwa kila moja, huku zikikubaliana kwa mkataba juu ya mambo ya msingi ya kushirikiana.

  “Mimi binafsi ni muumini wa Muungano wa Mkataba”, alisisitiza Maalim Seif na kurejerejea kauli hiyo huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wafuasi na wapenzi wa Chama hicho waliojitokeza kwenye mkutano huo.


  Amesema vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi mdogo wa Bububu hivi karibuni huenda zilipangwa ili kuvuruga umoja wa kitaifa, lakini wenye nia hiyo hawatofanikiwa kwani wazanzibari walio wengi wameelewa juu ya umuhimu wa amani na umoja kwa maendeleo ya nchi yao.


  Maalim Seif amewanasihi wazanzibari wanaoitakia mema nchi yao kwa kuweka mbele maslahi ya nchi badala ya vyama, kutumia changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo wa Bububu kujipanga katika kutoa maoni kwenye tume ya mabadiliko ya katiba ili kupata katiba wanayoitaka ambayo itatoa mwelekeo wa kuwepo kwa mamlaka kamili ya Zanzibar.


  Katibu Mkuu huyo wa CUF alisema ni wajibu wa vyama vya siasa na viongozi kuelewa kuwa hakuna chama wala mtu mwenye hati miliki ya nchi, bali wenye mamlaka hiyo ni wananchi wenyewe na kutaka wananchi watendewe haki na usawa katika huduma zote ninazohusu maendeleo na mustakbali wao.


  “Hakuna Chama wala mtu mwenye hati miliki ya nchi hii, nchi hii ni ya Wazanzibari wote kabisa”, alisisitiza.


  Alieleza kusikitishwa kwake na vitendo vya vurugu ambavyo anadai kuwa vilisababishwa na vikosi vya ulinzi na usalama, na kwamba kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya kazi yao na kuijengea picha mbaya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.


  “Mimi nashangaa sana kwa sababu askari ni wale wale waliosimamia uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, mbona katika uchaguzi ule walikuwa na nidhamu na hawakumbumbudhi mtu, inakuwaje katika uchaguzi huu mdogo walete vurugu na kuwadhalilisha watu?” alihoji Katibu Mkuu huyo wa CUF.


  Kwa mujibu wa taarifa za Chama hicho, watu wapatao 22 walijeruhiwa na kudhalilishwa wakati wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu uliofanyika Septemba 16, 2012, akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mtoni Faki Haji Makame (CUF).


  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Mhe. Ismal Jussa Ladhu amewataka wafuasi wa Chama hicho Jimbo la Bububu kuwa wastahamilivu wakati chama kikifuatilia changamoto zilizojitokeza kwenye uchaguzi huo.


  Mkurugenzi wa haki za binadamu, habari, uenezi, mawasiliano na umma katika chama hicho Salim Bimani, alisema hawakuridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo, na kwamba waliotangazwa washindi wanaweza kulitema jimbo hilo, kufuatia nia yao ya kwenda mahakamani kupinga matokeo yaliyotangazwa.


  Katika risala ya wanachama wa CUF jimbo la Bububu iliyosomwa na bi Mgeni Ali Suleiman, waliishutumu tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi kuvuga uchaguzi huo uliompa ushindi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM, na kuonya kuwa hawamtambui na hawatompa ushirikiano mwakilishi huyo mteule.


  Katika uchaguzi huo, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM Hussein Ibrahim Makungu alitangazwa mshindi kwa kupata kura 3371 sawa na asilimia 50.7, dhidi ya mgombea wa Chama Cha Wananchi CUF Issa Khamis Issa aliyepata kura 3204 sawa na asilimia 48.2


  Huu ni mkutano wa kwanza wa hadhara kufanywa na chama hicho katika jimbo hilo tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu uliofanyika Septemba 16, 2012.


  at 3:13 PM

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Tume ya Uchaguzi Zanzibar nilidhani imekomaa zaidi ya kwetu Tanganyika... Lakini inaonekana ni Wale Wale

  Kutetea Serikali Tawala... Inaonyesha labda CUF wataweza kuwashitaki CCM na Vyombo vyake Vya Dola?

  Kwasababu hatusikii Chochote toka kwa Katimu Muenezi wa CCM - Nape Nnauye au Mweka Fedha wake

  Mwingulu Nchemba... Wamekaa KIMYA; Au Chama Cha UGOMVI sasa ni CHADEMA tu???
   
 3. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hivi kweli kuna watu wanamsikiliza huyu mchumia tumbo ambaye aliingiza CUF kwenye unyumba na CCM? Ana jipya gani la kuwaambia watu aliowasaliti akauza damu yao kwa cheo kisicho na hata kazi ya kufanya?

  Seif angeambiwa aendelee na ndoa yake kivyake na asiwapotezee muda wale aliowasaliti kwa ufisi na uroho wake wa madaraka. Kama wataingia mkenge mwingine basi hawana maana.

  Seif anatafuta ulaji mwingine baada ya kugundua kuwa muda unazidi kumtupa mkono huku salata yake ikizidi kufichuka.
   
 4. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwanini sisi em wasimshike masikio mpinzani aliyebaki yaani daktari na kumzima kwa kacheo?! Inawezekana sisiem, chukua hatua.
   
 5. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Fujo za BUBUBU ni kina nani walifanya? Nataka kujua kama CDM walianzisha na huko.
   
Loading...