Picha: Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Kikwete Akabidhi Wasanii Mashuhuri tuu Kadi za kujiunga na CCM

Na ninyi CCM kubalini kwamba kwisha kazi. Pamoja na maandalizi yote hayo bado uwanja mmeshindwa kuujaza? Nape usipokuwa lakini presha itakuua.
 
Kwahiyo wasanii wa bongo movie walikuwa ktk kutengeneza movies zao na JK??
JB atuambie lini anaachia movie la wasanii wakishirikisha CCM??
 
Mmmh njaa ni mbaya sana mtu yuko radhi kujizalilisha kwa sababu ya njaa. Ukimuuliza unaipendea nini CCM hana jibu la maana eti ''nimezaliwa CCM nimekulia CCM ndo mana tuko hapa''

wewe huna njaa m.
 
Sina cha kuongeza, A picture is worth a thousand words
2A.jpg
kwani nimekataa..nilitaka jua alitembea hadi wapi na na alipandia gari wapi?
 
Kuonekana kwa Irene kwenye news tena kumenikumbusa ile kesi yake dhidi ya Shigongo ya kuingilia privacy yake na mpenzi wake Diamond; je iliishia wapi?. Niliwahi sikia alikuwa akidai fidia ya Shs200,000,000 kutoka kwa Shigongo ama sivyo Shigongo angefilisiwa. Heunda sikufuatilia vya kutosha kujua hukumu yake, ila sidhani kama hukumu yake ilitoka hadharani. Inavyoonekana ni kuwa tangu afungue kesi hiyo sijawahi kusikia akiandikwa tena magazetini, hasa yale ya mtandano ninayosoma, kwa hiyo huenda alishinda.

Kesi za madai Tanzania hupamba moto kwa kasi na kufifia kimya kimya kiasi kuwa huwa inanipa wasi wasi na justice system ya civil cases nchini mwetu.

Kuna kesi nyingine ya madai iliyofunguliwa na Kinana dhidi Msigwa nayo niliisoma lakini sijui nayo iliishaje; vile vile kulikuwa na kesi ya madai ya Ridhiwani dhidi ya Slaa nayo iliyeyuka.
 
Ndio chama chenye serikali
Serikali iliyowafungulia milango na kuwafanya muwe mamilionea
Serikali inayolinda haki zenu za kisanii kwa watu kudurufu wanavyotaka
Serikali inayoruhusu kazi zenu zinauzwa kwa kumwagwa chini kama matunda tandale
Serikali inayowafanya muendeshe harambee ya kwenda kijitibu nje mkiumwa na si kwa mamilioni yenu
Serikali inayowatumia na kuwatema kama bazoka
Serikali inayowatumia kwa kujibu mapigo kwa chama fulani
 

Attachments

  • 1391380249370.jpg
    1391380249370.jpg
    132.1 KB · Views: 109
Hahahaaa. Huku Manzese wanamwaga kwenye meza ni Sh 1000 tu. Hawa jamaa ni Viazi sana Chama hakiwajali lakini bado wameenda kuchukua kadi.
 
Kama ilivyo ada kwa CCM kuwatumia wasanii wa muziki hasa wa kizazi kipya katika kukinadi chama na kuwashawishi wananchi ambao ni washabiki wa wasanii hao kuipenda. Mbinu hii hutumika hasahasa katika kipindi cha kampeni, na wasanii hawa huzunguka kutumbuiza mikutano na hivyo kuwavutia wananchi. Safari hii CCM imeanza kujiandaa mapema zaidi, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu (2015). Katika kilele cha kuadhimisha miaka 37 ya chama leo hii, tumeshuhudia pia hadi wasanii wa filamu za kitanzania wakiwa miongoni mwa waliopamba shereke za kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika mkoani Mbeya.

Hata hivyo, baadhi ya wasanii waliotumika 2010 wametoa malalamiko yao kwa kuporomoka kimapato na kazi zao kutopendwa tena na wananchi wengi. Nilidhani ingekuwa fursa nzuri kwa kutafuta mbinu mpya, ama wasanii hawa kusoma alama za nyakazi katika maendeleo/mapato yanayotokana na shughuli zao za usanii. Kwa kuangalia utumikaji wa wasanii vipindi vilivyopita, inaonekana wazi kuwa SIASA za Tanzania zinaathari kubwa katika kazi za wasanii nchini (Ref. Marlow, Nakaaya nk.). Je? ni kwanini CCM haiwasaidii wasanii hawa pindi wanapomaliza kuwatumia (hasa kipindi cha uchaguzi). Wasanii wengi wanafikiri wanaweza kunufaika kama ilivyo wasanii wa TOT (Ref. Capt. Komba et al.).

Nimejaribu kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, nimeshuhudia wananchi wengi wakuchukizwa na baadhi ya wasanii kutumika kisiasa na wengine kusema ndiyo itakuwa mara yao ya mwisho kununua kazi za wasanii hawa. Je, CCM inampango gani ya kuwasaidia wasanii hawa mara watakapoporomoka katika kazi zao baada ya kuwatumia kikamilifu?

View attachment 136742 View attachment 136743 View attachment 136790 View attachment 136788 View attachment 136789 View attachment 136745 View attachment 136746 View attachment 136787 View attachment 136747[idont know how much you earn from this but guy this is mess is 2going2cozt u most of ur life
 
Hivi mbona sijasikia vijana wa CCM wakireact kwa kusema kuanzia leo hatusikilizi tena nyimbo za Prof J au kuanzia leo tusimsikilize Lady JD kwa kuwa kashirikiana na Prof J wa CHADEMA?
Ni chuki kiasi gani mliyo nayo kwa wasanii wakina Banana?Au hamkutaka wajiunge nacho..
 
wiki 2 zilizopita richie alikua Arusha,tukajua mjanja kaja kwa wajanja kumbe bonge la jinga lisilojua kusoma alama za nyakati,sasa biashara yenu ya usanii ndo imeshakufa tizameni mauzo ndani ya mwaka huu mtaniambia.
Khaa!! Hivi nyie mna akili gani? Mwaka 1992 nchi iliingia kwenye mfumo wa vyama vingi hivyo kila mmoja ana haki ya kujiunga na chamachochote kwa utashi wake. Lakini kwa akili zenu mnaona ni haki kujiunga na CDM tu. Hivi huko upstairz kuna ubongo au kinyesi?? Mnakera bana
 
Kujiunga na chama cha watu ambao ni vibaraka,vibarua,madalali na mawakala ya rostam ni kujinyonga mwenyewe.R.I.P
 
Acha fikra za kichawi dogo... kila mtu ana haki na uhuru wa kufanya apendacho mradi avunji sheria. Kwani ni lazima watu wote wawe misukule kama wewe? ????

Wewe sio bure utakuwa umevurugwa...
 
Hivi mbona sijasikia vijana wa CCM wakireact kwa kusema kuanzia leo hatusikilizi tena nyimbo za Prof J au kuanzia leo tusimsikilize Lady JD kwa kuwa kashirikiana na Prof J wa CHADEMA?
Ni chuki kiasi gani mliyo nayo kwa wasanii wakina Banana?Au hamkutaka wajiunge nacho..

Mimi nlikua sina kazi yao hata moja sababu nlihisi mapema ni wasaliti.
 
kimsingi wamefanya uamuzi usio sahihi hasa ukizingatia mvuto katika jamii hawana na kazi zao hazijakubalika sana katika jamii na pia suala la wasanii kujihusisha na sembe sura hizo hazija sikika ama kukataa ama kuunga mkono nao ni mizigo tu
 
Yani wafanyakazi mmewasainisha mahudhurio lakini hata kuwarusha kwa picha moja hamjataka!! Badala yake mmewapa airtime yoote "wasanii", watu ambao wanaigiza uwepo wao hapo!!!.
Mna roho mbaya kama nini...
 
Back
Top Bottom