Mmmh njaa ni mbaya sana mtu yuko radhi kujizalilisha kwa sababu ya njaa. Ukimuuliza unaipendea nini CCM hana jibu la maana eti ''nimezaliwa CCM nimekulia CCM ndo mana tuko hapa''
Kama ilivyo ada kwa CCM kuwatumia wasanii wa muziki hasa wa kizazi kipya katika kukinadi chama na kuwashawishi wananchi ambao ni washabiki wa wasanii hao kuipenda. Mbinu hii hutumika hasahasa katika kipindi cha kampeni, na wasanii hawa huzunguka kutumbuiza mikutano na hivyo kuwavutia wananchi. Safari hii CCM imeanza kujiandaa mapema zaidi, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu (2015). Katika kilele cha kuadhimisha miaka 37 ya chama leo hii, tumeshuhudia pia hadi wasanii wa filamu za kitanzania wakiwa miongoni mwa waliopamba shereke za kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika mkoani Mbeya.
Hata hivyo, baadhi ya wasanii waliotumika 2010 wametoa malalamiko yao kwa kuporomoka kimapato na kazi zao kutopendwa tena na wananchi wengi. Nilidhani ingekuwa fursa nzuri kwa kutafuta mbinu mpya, ama wasanii hawa kusoma alama za nyakazi katika maendeleo/mapato yanayotokana na shughuli zao za usanii. Kwa kuangalia utumikaji wa wasanii vipindi vilivyopita, inaonekana wazi kuwa SIASA za Tanzania zinaathari kubwa katika kazi za wasanii nchini (Ref. Marlow, Nakaaya nk.). Je? ni kwanini CCM haiwasaidii wasanii hawa pindi wanapomaliza kuwatumia (hasa kipindi cha uchaguzi). Wasanii wengi wanafikiri wanaweza kunufaika kama ilivyo wasanii wa TOT (Ref. Capt. Komba et al.).
Nimejaribu kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, nimeshuhudia wananchi wengi wakuchukizwa na baadhi ya wasanii kutumika kisiasa na wengine kusema ndiyo itakuwa mara yao ya mwisho kununua kazi za wasanii hawa. Je, CCM inampango gani ya kuwasaidia wasanii hawa mara watakapoporomoka katika kazi zao baada ya kuwatumia kikamilifu?
View attachment 136742 View attachment 136743 View attachment 136790 View attachment 136788 View attachment 136789 View attachment 136745 View attachment 136746 View attachment 136787 View attachment 136747[idont know how much you earn from this but guy this is mess is 2going2cozt u most of ur life
Khaa!! Hivi nyie mna akili gani? Mwaka 1992 nchi iliingia kwenye mfumo wa vyama vingi hivyo kila mmoja ana haki ya kujiunga na chamachochote kwa utashi wake. Lakini kwa akili zenu mnaona ni haki kujiunga na CDM tu. Hivi huko upstairz kuna ubongo au kinyesi?? Mnakera banawiki 2 zilizopita richie alikua Arusha,tukajua mjanja kaja kwa wajanja kumbe bonge la jinga lisilojua kusoma alama za nyakati,sasa biashara yenu ya usanii ndo imeshakufa tizameni mauzo ndani ya mwaka huu mtaniambia.
Acha fikra za kichawi dogo... kila mtu ana haki na uhuru wa kufanya apendacho mradi avunji sheria. Kwani ni lazima watu wote wawe misukule kama wewe? ????
Hivi mbona sijasikia vijana wa CCM wakireact kwa kusema kuanzia leo hatusikilizi tena nyimbo za Prof J au kuanzia leo tusimsikilize Lady JD kwa kuwa kashirikiana na Prof J wa CHADEMA?
Ni chuki kiasi gani mliyo nayo kwa wasanii wakina Banana?Au hamkutaka wajiunge nacho..