Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Amebadili kinywaji! kaacha Safari Lager, Jamaa tulikua tunapiga naye kilagi sio mchezo!
Bila shaka huyu mzee ni mnene kiasili, binafsi nadhani moja ya sababu iliyokua inamfanya aonekane kipipa zaidi ni uvaaji wa jaketi la kuzuia risasi(Bullet Proof) enzi hizo akiwa Mkuu wa Kaya ambayo sasa atakua havalishwi.
Kutuletea picha zingine mnatutafutia ban maana hawa watu wengine tukiwaona tu tunajikuta maneno yanayotutoka ndo hayo ya ban, tuhurumieni jamani
Kutuletea picha zingine mnatutafutia ban maana hawa watu wengine tukiwaona tu tunajikuta maneno yanayotutoka ndo hayo ya ban, tuhurumieni jamani
Pamoja na unene, dalili zipo za kupungua, hasa tumbo limesinyaa kiasi chake, na sasa anaonekana kijana zaidi na mwenye nguvu akitembea bila egemezo la wenzo (fimbo).
Kampeni za ubunge kule mkoani Tabora - Igunga alikuwa anatembelea fimbo, na alikuwa tufe, leo ni ajabu anaonekana kifua mbele misuli ya tumbo imesinyaa, ni talili tosha amepata dawa ya kupunguza unene, na daktari wake anastahili pongezi, hali kadhalika yeye kuwa msikivu kwa maelekezo ya madaktari.
Alipungua tangu alivyopelekewa samansi ya kuitwa mahakamani, chezea mahakama nyieee????!!!Kwa vyo vyote mwonekano huu ni tofauti na alivyozoeleka. Samahani kwa kusema alikuwa kama tufe, lakini leo anavyoonekana na afya nzuri, anatembea kwa maringo kwa mtondo wa gwaride, na hata anaweza siku hizi kufanya zoezi la afya ile push up.