picha zinajieleza zenyewe waswahili husema kusoma hujui hata picha uoni? Sasa picha tumeona jinsi Kinana anavyonunua watu lakini mi nasema ukiangalia asilimia kubwa ya hawa watu wanaonunuliwa umri umeend kidogo, sasa ni jukumu letu sisi vijana wa sasa hivi tusikubali kurubuniwa wa kudanganywa kwa njia yeyote ile. kwani mabadiliko ya TANZANIA yataletwa na watanzania wenyewe hasa wazalendo vijana ambao ndio taifa la leo.Hebu fikira mfano mdogo tu tangu tupate uhuru mpaka hii leo kuna baadhi ya vijiji havina maji wala umeme, mashule hayana madawati, sehemu nyingine hakuna vituo vya afya watu wanatembea umbali mrefu kutafuata huduma za afya alafu leo hii mtu anasimama jukwaani anakwambia anakwambia Viongozi wa serikali ya CCM ni waadilifu wachapakazi.
Mimi nasema vijana tusipokuwa makini tutakuja kuulizwa maswali na watoto zetu ambayo majibu tutakosa'
Tusiogope kusema ukweli penye ukweli na tusiogope kuhoju maslahi ya nchi yetu.