CCM tushawasema mpaka asymptote ya kikomo.
Sasa tuangalie "chama mbadala".
Nia ya kuanza kwa kusema hivi ni kutaka kueleweka kwamba naangalia mambo bila kujali vyama, bali kwa kuangalia mambo ya msingi zaidi.Mambo kama utaifa (kwa maana yake chanya), itikadi, miongozo, principles etc.
Kuna msemo wa Kiingereza kwamba picha moja ina thamani ya maneno elfu moja, shukurani kwa mdau aliyeleta picha.
Ona hii
https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=62414&d=1345383169
Naona kuna fulana nyekundu zilizoandikwa "Red Brigade". Soma zaidi kuhusu chanzo cha "Red Brigade" kwenye Wiki yake
http://en.wikipedia.org/wiki/Red_Brigades
Kwa sie tulioona "miezi kumi na nane ya kufunga mkanda" kwa macho na akili bila kuhadithiwa, kati ya hao tuliojitaabisha kidogo kufuatilia habari hata kwenye vitabu na vijarida tu tutakumbuka "Red Brigades" kama ma violent Marxist-Leninist up there with Carlos "The Jackal" na "Baaden Meinhof". Watu ambao waliamini katika assasinations kufikia political ends zao.
CHADEMA kinataka kutuaminishw kwamba ni chama mbadala.Kinaamini katika itikadi za "Red Brigades" hivi? Kiasi cha kuchapa fulana?
Au CHADEMA ni a bunch of people with no depth kiasi wanaweza kuchapa fulana "zikatokelezea" this prominently, bila kujua kwamba katika wasomi wastaarabu wa leo the entire "Red Brigade" chapter of history is an embarrasing episode?
Je, kiitikadi, CHADEMA kinaunga mkono "Marxism-Leninism" kiasi cha kujiranda na "Red Brigade" yake mpaka kuchapa fulana zinazokubalika hivi?