PICHA: Matapeli wa kuuza viwanja, mashamba Bagamoyo watiwa mbaroni

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,393
24,968
MATAPELI WA VIWANJA BAGAMOYO.

Hawa ni matapeli wa kuuza viwanja Mapinga, Bagamoyo muwaogope.

Wamekamatwa muda mfupi uliopita, mwenye t-shirt ya mistari anajifanya mtoto wa huyo baba aliyevalia pajama ya michezo na huyo mweusi ni dalali.

Wengi wameshalizwa. Tuwe makini katika suala la kununua ardhi.

Sent as received!!
uploadfromtaptalk1461429519982.jpg

uploadfromtaptalk1461429535972.jpg
 
Asante kwa taarifa, ngoja sheria ichukue mkondo wake ukweli ujulikane
 
MATAPELI WA VIWANJA BAGAMOYO.

Hawa ni matapeli wa kuuza viwanja Mapinga, Bagamoyo muwaogope.

Wamekamatwa muda mfupi uliopita, mwenye t-shirt ya mistari anajifanya mtoto wa huyo baba aliyevalia pajama ya michezo na huyo mweusi ni dalali.

Wengi wameshalizwa. Tuwe makini katika suala la kununua ardhi.

Sent as received!!
View attachment 341873

View attachment 341874
Mkuu afu haya matangazo ya watu kuuza ardhi ni mengi sana hasa huku chanika, tena wengine wanasema wanakopesha, asa wengine tukiingia tamaa, binafsi natamani kununua ila naogopa kwa kweli mshahara wangu wa mwezi nisije kumpa mtu bureeee.
 
MATAPELI WA VIWANJA BAGAMOYO.

Hawa ni matapeli wa kuuza viwanja Mapinga, Bagamoyo muwaogope.

Wamekamatwa muda mfupi uliopita, mwenye t-shirt ya mistari anajifanya mtoto wa huyo baba aliyevalia pajama ya michezo na huyo mweusi ni dalali.

Wengi wameshalizwa. Tuwe makini katika suala la kununua ardhi.

Sent as received!!
View attachment 341873

View attachment 341874

Niliwahi kujumuika nao kwenye kinywaji Mrina Bar Mingoi kwenye kona ya kuelekea Kiharaka!
 
Kiukweli mapinga bagamoyo kumechafuka sana ukienda kiharaka kule ujambazi wa ardhi unatutesa sana nimefurahi kukwamatwa. Taarifa zote tumeshapeleka kwa mkuu wa wilaya mkuu wa mkoa na hata ocd bagamoyo wanazo kumbukumbuku
 
Aisee huyo mwenye zebra ni dalali kweli mie nilifanya nae biashara aliniunga kwa mwenye eneo lakini nilipitia taratibu zote kiserikali mpk hatua ya mwisho ndio nikalipia eneo.
Muwe makini sana kufanya uchunguzi manake kuna madalali wananunua mpaka ofisi ya mtendaji serikali ya mtaa mjumbe na yeyote yule ili utapeli ufanyike haswa wahindi ndio wamepigwa sana huko bagamoyo.
Msione ujinga kitumia wanasheria mnao wafahamu kwani inasaidia sana kukuweka salama japo kuna gharama unalipia lakini ni bora kuliko kujifanya bahili kisha unapigwa kote kote pesa na eneo unakosa.
 
wamekutana na mkono alhaji majid huko bagamoyo lazima wapoteane,wasambaa hadi kesho hawataki kumsikia huyo mtu mana kasi ya Magufuli alianza nayo tangu enzi za baba Riz
 
Aisee utapeli wa viwanja umezidi sana,mimi hadi naogopa sasa kununua viwanja,wakuu mwenye uelewa wa kipi cha kufanya na kufuata ili usitapeliwe atupe uzoefu hapa,maana nna washkaji zangu watatu washapigwa pesa na viwanja wameuziwa watu wengine,so inatia uwoga sana!
 
Aisee hamna watu nawachukia Kama hawa wakuitwa madalali..Ni chanzo cha kuongezeka kwa wezi na bei ya bidhaa husika. Serikali iliangalie hili swala katika jicho la tatu
Ungepata taaluma ya ujasiriamali ungetambua madalali hawaepukiki na kama wataepukwa changamoto itakua kubwa kuliko wakiwepo kwenye mfumo wa biashara kwani kwa kiasi kikubwa uwepo wao unafaida kuliko hasara itakanayo na kutokuwepo kwao
 
Hii siyo kweli
 
Back
Top Bottom