PICHA: Mapokezi ya Prof Lipumba; Afande sele atumbuiza

na yale malori yaliyokuwa yanasomba washabiki gharama zake zimejumuishwa?

Inasema malori yalianza kuleta watu saa 12 asubuhi.Malori mengi yalileta watu kutoka Rufiji,Kisarawe,Bagamoyo na kuna waliosombwa kutoka Lindi.
 
Hakukuwa na haja ya kutumia fedha kiasi hicho kwa tukio kama hilo. Bora hata wangepewa wabunge wao kuchangia shughuli za maendeleo au wangetafuta kundi la vijana wakaanzisha miradi midogo midogo kupunguza tatizo la ajira naamini wangekitangaza chama chao maradufu kuliko hili tukio halina impact yeyote kwa uchumi wetu wala chama chao. mil 10 hadi 20 zinatosha tena nyingi.

Ni kweli mkuu wangu.Malori yamesharudisha watu kwao wamelipwa chao na bado chama kiko ICU
 
Habari kutoka makao makuu ya chama cha wananchi CUF ni kuwa kimetumia milioni 150 kwa ajili ya kumpokea mwenyekiti wao prof Lipumba,matumizi inahusisha posho kwa viongozi mbali mbali,usafiri wa ndege kwa wajumbe kutoka Zanzibar na maeneo mengine ya Tanzania bara,wametumia pia kulipia Star tv matangazo ya live,pia pesa zingine wamepewa vijana na wazee wa chama hicho kwa ajili ya kujitokeza kwa wingi kumlaki prof Lipumba ili watu waone kuwa bado CUF inapendwa wakati ipo icu.
Vyama vingi vya siasa, vina ujanja wa kuteka watu uwanjani na kuona kuwa wana watu wengi.

Hawajui sio kila akupigiae makofi ana kushangilia, Ingekuwa hivyo umati huo ccm isingeshi. Utaona uchaguzi wa Arusha.
 
Hii ni sawa na kuficha uchafu uvunguni ili baba asione,wanasahau utakuja nuka soon,Lipumba angeachana na siasa uchwara aanzishe hata taasisi ya consultancy za uchumi na mipamboo ili atunusuru na balaa la omba omba,biashara ya magogoni haimfai tena asije akapata kura za mrema.

Kuwemo kwenye siasa haina maana ya kwamba hawezi kuishauri nchi yetu juu ya masuala ya uchumi! Kwani hivi sasa anayoyafanya huko duniani hayupo kwenye siasa? Tatizo lake ni kuwa mtanzania! Watanzania hawabebeki!
 
CCM inawaamini maprofesa wachache saana sio kama Prof Lipumba!!! watu muhimu kwa ccm ni kama Prof Majimarefu and the like na ndio maana wamewaalika Arumeru Mashariki kutia nguvu ili kijana wao atoke kifua mbele!! wana maziongombwe ndio muhimu!!!:cool2:
 
CUF bwana kweli ni CCM tupu!
Hata tabia ya kubeba watu kwenye malori!

Na afande Sele kweli na akili zake amepewa nini hadi kwenda kwenye chama kichovu hivi!?

mnapenda kujifurahisha kweli mnajifariji sasa watu wanatambua chama gani kipo makini nyie endeleeni kujisemea kichovu huku uchovu wenu amuoni
 
Hukumbuki wangenga walisema palipo na miti mingi hakuna wajenzi? Kama umewahi kumwona Fundi uashi ana nyumba yake nzuri ujue sio fundi mzuri sana. Vile vile Mafundi seremala wengi hawana fernichers nzuri majumbani mwao. Umeshamwona fundi mshona nguo anavaa nguo bomba? Ukimwona basi huyo ni msimamizi tu sio fundi cherehani. Je, Umeona wapi Askofu watoto wake wakawa na tabia nzuri sana? Ulizia kama utakuta watoto wengi wa walimu wana akili sana. Only the exceptions which however, are very few!!!!

Tanzania imelaaniwa laana ambayo kina Mwakasege wanapigia kelele kila siku ili kuikemea ishindwe na kulegea ktk JINA KUBWA KABISA la YESU KRISTO, lakini laana hiyo haitoki kirahisi sababu wanaowazunguka katika maombi hayo nao wametingwa na dhambi kibao hata zinawasuta wakati wa maombi na hatimaye maombi yanazuiwa kufika JUU mbele ya Muumba, Kanchi katajiri sana lakini kananuka umaskini sababu wapo watu wanatambika sana kujilimbikizia utajiri kwa kuweka misukule kwenye ofisi zao, vitega uchumi vyao, uongozi wao......hata wengine huua watoto wao ili watajirike upesi lakini hawadumu sana, wenzao wanaobaki wala hawaoni hayo maana shetani anawasahaulisha. Hii ni vita ya kiroho. Bila kujali dini gani ni lazima watanzania wote tuamke, tutubu na kutakasika na ndipo tumwombe Mungu atuonee huruma. Hatupigani lakini nchi zinazopigana zinapaa kiuchumi. Sisi tunawaita wageni waje wale, wanye waondoke na kila wanachokitaka kutoka kwetu, nasi wanaturushia sumni kama vile makonda wanavyowafanyia wapigadebe, halafu tunafuraaaaaahi ajabu. Kama sio laana ni nini hiyo. Unaweza kuiona vizuri Tanzania ukitoka nje kidogo tu, itazame kutoka kule ndo utajua laaana hapa ndio amri ya kila siku tunaitumikia.

Aaghrrrr!!!

Message sent and delivered, I am not sure it is read. kila munu abena kwabo. Tusali sana sio mchezo, tena kwa kumaanisha.

tulilaaniwa tangia 1973 tulipo vunja uhusiano wa kibalozi na Israel. Mungu hatanii kwa taifa lolote lenye kuilaani Israel. Halafu tukaweka palestina day ili mtanznaia amchukie myahudi masaa 24! Leo Kenya anatutawala kiuchumi!
 
Ni kweli mkuu wangu.Malori yamesharudisha watu kwao wamelipwa chao na bado chama kiko ICU

unasapoti pumba tu ilavyama vingine vikitumia pesa zaidi ya hizo ndo sawa ila cuf ufujaji pesa. Endeleeni kusema icu 2015 tumeamua kumpa lipumba sasa kalieni na phd ya dini. Ndio kiwango chenu.
 
kafu oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

cuf 1.jpg cuf 1.jpg cuf 2.jpg cuf 3.jpg kafu i.jpg

kwa style hii ccm ni nambari wani na itaendelea kuwa nambari one
 
Inafurahisha sana kuona kiongozi aliyethaminiwa na dunia akipokewa na wafuasi wa chama chake kwa shangwe na furaha.

Inasikitisha sana kuona hii haikuwa Kitaifa.

Mnajidanganya kweli....mpelekeni Zanzibar apokelewe kimkoa....si mna ndoa kwenye baraza kule ..
 
Huyu jamaa ni mchumi mzuri lakini yupo kwenye chama ambacho kinaingozwa KISULTANI na hivyo kwa vyovyote vile hatuwezi kumpa jukumu la kujenga uchumi wetu.
 
Inafurahisha sana kuona kiongozi aliyethaminiwa na dunia akipokewa na wafuasi wa chama chake kwa shangwe na furaha.

Inasikitisha sana kuona hii haikuwa Kitaifa.

Kwani kaliingizia taifa mapato ya shilingi ngapi kwa kuwemo kwenye hilo jopo au katengeneza ajira au kaleta wawekezaji wa maana wa kusaidia tanzania kiasi gani hadi apokelewe kitaifa? Siku hizi ni diplomasia ni siasa uchumi siyo blabla.Umeleta kwa nchi nini siyo tu umeleta misifa uliyosifiwa kibinafsi isiyo na pesa wala mshiko kwa nchi.

CUF nadhani ndie profesa pekee waliyenaye tofauti na vyama vingine ambavyo vina maprofesa kibao wanachama wao.Wana haki kumpokea kimbwembwe profesa pekee ndani ya CUF.
 
Back
Top Bottom