Mkuu @Mkandara , hata sijui kwanini umehamaki.
Kwanza, ninapenda sana kumpongeza huyo mama kwasababu zifuatazo
1 Ametambua mapungufu yaliyotokea iwe kama yeye au mazingira yaliyomzunguka
2 Ametambua tatizo na wapi suluhu inapatikana. Ameongozwa na weledi
3 Mama huyo amekuwa mkweli wa nafsi yake na kwa wengine kwakusema ukweli
4 Anakuwa role model ya watoto wake yeye mwenyewe bilakumtegemea ma miss Tz
5 Anakuwa role model kwa jamii yetu yote kwa kujitoa,kufumbua macho wanaojitia upofu, wanaopotosha jamii na wengine waliojaa au kujazwa upuuzi
Pili, nimetaja makundi ya akina mama kwa sababu nilidhan itayari wameshamfikia kumkomboa mwanamke mwenzao.
Hatuwezi kuwa na umoja wa wabunge wanawake wenye kazi ya kutafuta mgombea mwanamke kwa Urais.
Hatuwezikuwa na wabunge wa kuteuliwa kwasababu uanawake wao wasiojua wanawake wanaishi wapi.
Hatuwezi kuwa na utitiri wa NGO za kutetea wanawake ambao kwahakika nikundi la wasomi na si kama mama huyu.
Hatuwezi kuwa na ma miss wenye kazi ya kugawa viroba vya Michele kwa mayatima kila sikuu huku wakishindwa kujua jamii yao ipo wapi.
Hatuwezi kuwa na kelele za uwiano sawa wa nafasi kati ya jinsia ikiwa wanawake hao hao hawajui wenzao wapo wapi wanaishije.
Nimemtaja Mohamed Said ilia one tatizo la jamii yetu kwa ukubwa wake.
Kuibuka na namba anazoita takwimu bila kujua tatizo la nchi na jamii kwa ujumla ni jambo la hatari, kupotosha na kusikitisha.
Tunamuonyesha mfano ili aachane na kukusanya namba mbili au tatu akaziita takwimu na kupotosha jamii.
Kwa upande wako, sijui kwanini umehamaki. Nashukuru unafahamu tatizo lililopo ni kama la omba omba.
Kwamba, kuna tatizo katika mfumo mzima, si tatizo la ‘mfumo' unless useme ndivyo ulivyomaanisha.
Kama wadau wengine nimekualika tu ili kupata mtazamo wako,huna sababu ya kuhamaki