Raimundo
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 13,415
- 12,622
Hii nchi bana, yaani mtu anaiba mchana kweupeee
Wanatafuta mtaji wasambaze mikeka!
Hii nchi bana, yaani mtu anaiba mchana kweupeee
hiko kijamaa chenye frana la njano kinakaa kitaa,kujishaua kote kule kumbe ni kijizi...!? aaah nina wanangu wako jera ngoja niwakawape taarifa kuna mademu wanakuja,kila mtu achukue wake....
haaa kumbe nikajambawazi....😱
Wizi wa kijinga...eti kadi ya ATM na password...hawajasoma hawa?
Wizi wa kijinga...eti kadi ya ATM na password...hawajasoma hawa?
Hakuna jambazi hapa hivi ni vibrazamen vya uswahilini, jambazi gani unapata muda wa kujiremba. Jambazi la ukweli na sugu sio kwamba anapenda kuwa na sura ngumu kwa makusudi ila ni makovu ya risasi pia utakuta ameshiba kikweli kweli kwa mazoezi makali. Hawa hata sehemu ya kupiga makofi hakuna ndiyo mana wamekalishwa hapo bila wasiwasi wowote, yangekuwa majambazi ya ukweli ungeskia risasi za unguruma dar na helikopta kibao kwenye anga la dar na huwakamatiMabrazameni kabisa hawa...
harafu hako kagari ni kababa yake,se.nge sana huyu dogo...
Wale makoti makubwa na sura nzito walikuwa majambazi wa zamani ila walikuwa na ubinadamu wanapokuvamia nyumbani pamoja na kwamba wanachokifanya hakikubaliki mbele ya jamii, ilikuwa ukikubali na kuonyesha ushirikiano kwa kuwaachia au hata kulala chini na kuwaacha wafanye yao kwa kuchukua vitu bila idhini yako hawakujeruhi lakini hawa mabarobaro ni shida yaani wanachukua mali zako na bado na kukukatakata pia kutahusika hata kama ulijisalimishaMasharobaro ,nilijua jambazi ni wale wanavaa makoti makubwa sura za kikauzu kumbe sio
Stress za maisha2_* kukimbilia utajiri , warudi kijij walime ~
Hawa wamekaa kitapeli kuliko kijambazi
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM JUU YA KUTIWA MBARONI KWA WATUHUMIWA SUGU WA KUPORA RAIA WA KIGENI NA AKINA MAMA
Watuhumiwa wanne wamekamatwa jijini Dar es Salaam katika makutano ya barabara ya Bibi Titi na Ohio karibu na Hotel ya Serena baada ya kumpora raia wa kigeni wakiwa na gari dogo rangi ya kijivu yenye nambari za usajili T787 DBU Toyota Cienta.
Hivi karibuni kumeibuka wimbi la wahalifu kuwapora pesa na vitu vya thamani kama mikufu, bangili, hereni pia pete na vitu mbalimbali vya thamani raia wa kigeni na akina mama ambao hupenda kutembea na pochi. Wahalifu hawa hutumia gari dogo ambalo mara kwa mara hubadilishwa namba zake za usajili na wakati mwingine gari hili wanalitumia kama Tax bubu.
Leo tarehe 21/04/2015 majira ya saa 09:00 asubuhi katika eneo la Posta Mpya watuhumiwa hawa walimdangavya bwana CEES S/O JAN CONIJN, Miaka 27, raia wa Uholanzi aliyetaka kufika Klabu ya Leaders kwamba wangempeleka eneo hilo kwa kutumia gari tajwa hapo juu. Baada ya kuondoka na dereva kila baada ya mita 200 dereva huyo alikuwa anasimamisha gari na kuongeza mtu mwingine kama abiria hadi walipotimia wote wane.
Walimpeleka hadi maeneo ya Kinondoni kwa Manyanya na walipofika eneo hilo walimweleza wazi kuwa wao ni wahalifu na walimtaka awapatie pesa vinginevyo wangemuua. Aliwapatia pesa zote alizokuwa nazo Tshs 75,000/= lakini hawakuridhika ndipo walipomtaka awapatie kadi ya benki (ATM CARD) na nambari za siri (Pass Word). Baada ya tukio hilo wakamtupa karibu na Hospitali ya Mwananyamala na wao wakageuza gari kurudi katikati ya -mji. Wakati tukio hilo linatokea raia wema walishuhudia na kutoa taarifa kwa Polisi. Polisi walifuatilia haraka na kuweka mtego uliowanasa watuhumiwa wote katika eneo la makutano ya barabara ya Bibi Titi na Ohio karibu na Hotel ya Serena.
Majina ya watuhumiwa waliokamatwa ni:
1. SALUM S/O SAID MTUMWA @ MARO, Miaka 25, Mkazi wa Changombe Bora.
2. ALEX S/O INNOCENT MANGUKA @ MAKA, Miaka 30, Mkazi wa Kimara Temboni.
3. MOHAMED S/O ALLY ABDALLA @ MEDY, Miaka 27, Mkazi wa Mwananyamala.
4. STEPHANO S/O ALBERT KIKINDI @ KING, Miaka 32, Mkazi wa Mwananyamala.
Usidharau ATM card kuwa na pin code sio salama sana kwa mtumiaji, kwenye nchi zenye organized crime , wahalifu wakikuteka wanakuweka chini ya himaya yao, wanakulazimisha kutoa namba za siri , then mmoja wao ankwenda kujaribu Kutoa pesa , akifanikiwa anaangalia na balance kabisa , akikuta kuna mzigo wa kutosha , ndio inakuwa mbaya zaidi kwako, wanaweza wakaamua wakuuwe , au wakuweke chini ya ulinzi wao mpaka watakapomaliza pesa yote bank, idea ni kuwa wakikuachia utaenda kutoa taarifa ya stollen card na kadi itafungwa..
Mwanzoni nilikuwa Kama we we nikidhani Niko Salama kwa kutembea na kadi ya ATM, lakini iliwahi kumtokea rafiki yangu wa karibu sana akiwa nje , ndo nikajua downside ya hizo ATM card , nadhani kiusalama akaunti zenye pesa nyingi ni busara zisiwe mobile ,