dah ukipata gundu la pimbi unaweza kujiua aisee.
kumbusha mimi long time kitambo
Enzi za kina zumo,obi,seba,linda na mayuku. Bila kumsahau mzee wa tungi sokomoko
Ehe Bwana nilikuwepo enzi hizo. Yes Chris Katembo alikuwa mchoraji mwenza na John Kaduma. John alifariki siku nyingi, zile bangi alikuwa anapuliza zisingemuweka hai muda mrefu. Lakini walikuwa wabunifu kweli kweli.
Tiba
Mie nimeyamisi majembe ya kwenye Jarida la Bongo akina Jua kali/kibaka, Ndumilakuwili/tapeli, Chepe/mzee wa fix, mapung'o/mchezaji na fidodido
hatari sana....Nimeona wiki iliyopita tu kwenye gazeti la Sani Pimbi kamtembelea mshikaji wake ulipofika mda wa kuoga Pimbi akapelekewa maji na shemeji yake alipofika bafuni wacha amvutie bafuni Shemeji baada ya mda mshikaji wake akashituka mbona wife harudi? ikabidi avizie kule bafuni kilichotokea hukoo!!! Labda tusubirie Part II
Dah kuna game tulicheza na Born Town huku Meko akiwa South Afrika, kipindi hicho Mandela ndio amekuwa rais wa nchi na kina Meko ni baadhi ya watu walioombwa kwenda kuhamasisha soka South Africa. Kumbe meneja wa timu alimtumia tiketi ya ndege mzee meko bana, mara half time mzee katia timu huku tulishapigwa goli 2 safi.
Kama kawaida ya mzee Meko, goli zote zilirudi na tukashinda mechi.
NB: Mimi nilikuwa mnazi wa Bush Stars.
Sokomoko mzee wa tungi,bila kumsahau mzee wa majibu ya kunya,LODI LOFA.
bila kumsahau mzee Ole mbabe
Mkuu! Nilikuwa nikitoka kijijini hadi Masasi mjini kuhemea hili jarida kila toleo jipya linapotoka. Wakati mwingine nilikumbana na karaha tele kulipata. Kipato kilikuwa duni nikitegemea ndg yangu aliyekuwa ananitumikisha kutwa 1 au 2 ktk Mgahawa wake kwa ujira wa hili Jarida. Lakini nikilitia mkononi inakuwa raha narudi kijijini mjanja mie.
Mkuu bila shaka ulikuwa ukirudi kijijini wewe ndo unakuwa Aluatani
Nafikiri umaarufu na upinzani wa Mapung'o kwenye Bongo vs mwenzake chepe ulikuwa kama Ronaldo na Messi, kuna game Chepe alichomoka kwa spidi na mpira Beki akamvuta shati ikaavuka, akamvuta bukta ikavuka, akamvuta chup ikavuka pia, ilibidi beki akamate ngozi ya mgongo, nayo ikavutika huku Chepe anakimbia tu.
Baada ya hapo aliachia bonge la shuti, likagonga mwamba na kurudi ndani, refa ndiye aliyemalizia kupiga golini huku mwenyewe anasema "Hii move huwezi kuiacha iende hivi hivi.
alicheza mpaka real Madrid yeye namwenzie Chepe