Pichani:
Elizabeth Michael ‘Lulu' akiwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni (lol), Dar es Salaam mwaka jana alipokuwa akituhumiwa kumshambulia kwa matusi ya nguoni, mlalamikaji Kilakhaba Aziz.
Msanii maarufu wa filamu hapa nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu' leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shitaka la mauaji.
Lulu alipandishwa kizimbani kwa usiri mkubwa akitokea Kituo cha Polisi cha Oysterbay alikokuwa akishikiliwa na kupandishwa kizimbani moja kwa moja bila kuwekwa mahabusu ya mahakama hiyo kama iwavyo kwa washitakiwa wengine wanaosubiri kusomewa kesi zao.
Baada ya kupandishwa kizambani alisomewa shitaka lake na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Elizabeth Kaganda ambapo alisema Mnamo Aprili 7 mwaka huu majira ya saa saba za usiku maeneo ya Sinza Vatican jijini Dar es Salaam Elizabeth Michael (18) alimuua Steven Kanumba. Katika kesi hiyo mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote isipokuwa alinyoosha kidole na kupinga umri uliotajwa kuwa ana miaka 18 na kusema umri wake ni miaka 17. Baada ya kusomewa shitaka hilo, Lulu alipelekwa gerezani Segerea na kesi yake itasikilizwa tena aprili 23 mwaka huu.
Source: News - Global Publishers
hii picha ya mwaka jana kamanda[/QUOTE
Ndugu,
Pamoja na kwamba sheria itachukua mkondo wake, tumuombe Mora aachiwe huru
Elizabeth Michael Lulu akiwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni (lol), Dar es Salaammwaka jana alipokuwa akituhumiwa kumshambulia kwa matusi ya nguoni, mlalamikaji Kilakhaba Aziz.
Mkuu umechanganya madesa
Hii picha ya mwaka jana mahakama ya Kinondoni
Unapotosha watu
Great Thinkers maelezo yaliyoko kwenye picha yanajitosheleza. Wala title haijasema ni Picha ya Mahakamani leo ingawa habari yake ny ya leo.
Sasa hasira za nini Wadau mnataka kuniua bure? Ngoja nivute Jack Daniels yangu hapa!