Picha iliyonigusa

Picha iliyonigusa

Mpita Njia

Platinum Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
6,999
Reaction score
1,189
Nimeziona picha nyingi kuhusiana na ajali ya meli Zanzibar, lakini picha hii imenigusa kwa namna ya pekee kabisa. Nikiangalia sura zao zisizo na hatia, ninaona kuwa kama taifa, tumewaua malaika hawa bila sababu za msingi watoto.jpg
 
hii picha imenitoa machozi inasikitisha sana
 
Inauma kuona taifa linapotea kutokana na uzembe tu wa watu wachache ,Eee mola tuepushe na tamaa za wachache zinatuangamiza sana poleni wafiwa wote mola atwarehemu, am..........................................
 
...Ni msiba mkubwa sana..."malaika" wa Mungu wanapolazwa chini ya hema huku wazazi wao hawajulikani walipo; ni huzuni na simanzi hata kwa sisi tunaotazama watoto waliyekufa maji na wamelazwa kama wamelala! Inatia majonzi na huzuni pia kwa kuwa inawezekana sana wazazi wa watoto hawa wametoweka pia. MWENYEZI AZIPOKEE ROHO ZA WATOTO HAWA NA AWAZADIE NURU YA MAISHA YAO (BAADA YA KUFA) KWA KUWA NI WASAFI NA ROHO ZAO NI NYEUPE KAMA THELUJI. INNALILLAH WA INNA ILAYH RAJIUN (SISI NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWA MWENYEZI MUNGU TUTAREJEA).
 
nimeliaa baada ya kuimagine watoto walivoteseka wakinywa maji E Mungu
 
inasikitisha sana.....hasa ninapofikiri walipotumbukia baharini walifanyaje......hawakuweza kujiokoa wala kujua ni nini kinaendelea.....kweli inauma.....
 
inasikitisha zaid kuwa hakuna guarantee kuwa tukio hili halitajirudia. tume ya mv bukoba accident sijui ilishauri nini ambacho kilikuwa tofauti this time
 
Na anacheka cheka akihutubia taifa kwenye msiba?
Kimeo tunacho!
 
Back
Top Bottom