Picha hii inakukumbusha nini?

Inanikumbusha utawala wa huyu mzee, alikuwa anakandamiza sana watu.

Haya sasa hamkandamizwi mnafanya kitu gani zaidi ya kulalamika. Afadhali kukandamizwa kwenye kuleta tija kuliko kuwa huru na kukuukumbatia ufisadi na uholela. Uhuru usio na tija ni afadhali ukoloni.
 
206295_201872893167465_3289548_n.jpg

[h=2]Nukuu Sita za Nyerere ambazo CCM hawana budi kuzitafakari kwa makini sana leo hii [/h] 1. "Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?"
2. "Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii."
3. "Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi?"
4. "Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga."
5. "Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili."
6. "Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache katika nchi yao wenyewe...."


Na ya saba ambayo aliitoa siku nyingi sana;

7. “Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika" - Mwalimu Nyerere (Januari, 1966)

Na nyingine ya nane;

8. “Kwani fursa iko mbele yetu na inategemea kama tuna ujasiri wa kuichukua. Kwani uchaguzi uliopo siyo kati ya kubadilika au kutobadilika; uchaguzi kwa Afrika ni kati ya kujibadilisha au kubadilishwa – kubadilisha maisha yetu wenyewe kwa mwongozo wetu, au kubadilishwa na matokeo ya nguvu zilizo nje ya udhibiti wetu.. .Tunapendelea kushiriki katika kutengeneza hatima yetu sisi wenyewe” –MwalimuNyerere (Januari, 1966)

Nukuu hizi zimo katika kitabu kinachoitwa : Reflections on leadership in Africa: forty years after independence : essays in honour of Mwalimu Julius K. Nyerere, on the occasion of his 75th birthday ' , by Haroub Othman, VUB University Press, 01 Jul 2000.


SISIEMU ni chama hatari sana sana kinapandikiza udini,ukabila na mauaji Tanzania,Chama hiki 2005 kilikataliwa sana mijini,lakini kwa sasa mpaka vijijini ndani ndani huko Maswa,Meatu,Bukombe,Ukerewe n.k.,wote wazee kwa vijana wamekikataa hawakitaki tena,hawataki hata kukisikia wanasema 2015 lazima wakichinjie baharini.
 
Mungu ribariki kanisa langu katholiki la mitume,Mungu mbariki Dr.Slaa rais wetu mtarajiwa 2015,Mungu mbariki wetu Mhashamu Cardinali Pengo,Zaburi 23.
 
Mungu ribariki kanisa langu katholiki la mitume,Mungu mbariki Dr.Slaa rais wetu mtarajiwa 2015,Mungu mbariki wetu Mhashamu Cardinali Pengo,Zaburi 23.
 
Hii picha inanikumbusha jinsi Urais ulivyokuwa unaheshimiwa na kuogopwa. Hapo Mzee Malecela unaona alivyoweka mikono yake Kama anaomba dua huku akimsikiliza Mzee mzima. Pia inanikumbusha enzi ya Chon-li na Kaunda suti za vitambaa vya URAFIKI TEXTILE.
 
Nyerere ni "mdogo wangu" kimila na desturi. Yeye alikuwa mtani wetu mzuri sana. Uliza usimuliwe stori ya marehemu Batenga alivyosomba tofali za Nyerere pale kwake Msasani. Umenielewa?

Batenga ndo yule aliyemtapeli mwalimu kuhusu matofali?
 
Picha hii ianikumbusha ukweli kuwa paka akiondoka mipanya hujitawala. Unadhani mchonga angekuwapo angeacha kuwatolea uvivu vilaza wetu. John mwenyewe aliyemuita mhuni kweli amegeuka mhuni kwa kuwekwa mfukoni na hawa mafisadi vilaza wetu.
 
ckukuta utawala wake,najiona mwenye huzuni kwani sina cha kuadithia watoto wangu kuhusu mwl Nyerere
 
Nyerere ni "mdogo wangu" kimila na desturi. Yeye alikuwa mtani wetu mzuri sana. Uliza usimuliwe stori ya marehemu Batenga alivyosomba tofali za Nyerere pale kwake Msasani. Umenielewa?

Eeh kweeli ile ishu naikumbuka saanaaa!... Mh!. Ngoja nitoke ntarudi baadaye nikacheki usalama homu kabla hiri rijamaa HALIJATAPERI!
 
Inanikumbusha utawala wa huyu mzee, alikuwa anakandamiza sana watu.
Aliwakandamiza waliotaka tuuze madini na wanyama (vitalu vya kuwinda) na wale aliowaona wana tamaa, na watatupeleka kubaya. Siwajui, nahisi. Lakini ameatuachia mali zetu, ametuacha angalau na mwanga wa kielimu kidogo. Tuharibu sisi wenyewe. Mlaumuni, lakini angeuza madini yetu kama kina Mabotu tungelikuwa na nini. Watu wanampiga vita hasa wazungu na wenye damu ya ufisadi sababu aliwabania mali za nchi. Tumuenzi hata kwa mapungufu yake machache.
 
Mzee mwenye nchi!mzalendo wa kwanza wa kweli cijuikama katika nafasi yake atakuja mwingine!Rest in peace Mwalimu J.K. Nyerere
 
Back
Top Bottom