Picha hii inakufanya ujiulize nini?

Picha hii inakufanya ujiulize nini?

Iamhonest

Member
Joined
Jun 27, 2018
Posts
14
Reaction score
22
main-qimg-3fbcf74adc6f3a65dd86f5e4a81bd8c7.jpeg
main-qimg-2e9545d680bf2ebfe44bb1d01cffc851.jpeg


Kwenye picha hizo hapo juu, utaona watu wawili wameketi kwenye pikipiki. Inaweza kuonekana kawaida kwa baadhi ya watu kwa muonekano wa haraka. lakini kiuhalisia, lakini hao waliokaa nyuma ya dereva siyo watu walio hai: ni miili ya watu waliokufa.

Nilidhani naujua uhalisia wa umasikini lakini nimeona jinsi miili ya watu waliokufa inavyochukuliwa kutoka vijiji vya mbali ndanindani D. R. Congo kupelekwa mochwari kwa kuwa hawana uwezo wa kukodisha magari maalum yakubeba miili ya waliofariki (mochwari inapokuwa mbali sana na kijiji),

Kwa hivyo watu wanaamua kuufunga mwili kwa nguo na kuukalisha nyuma ya pikipiki, hivyo dereva wa pikipiki anaupeleka mwili mochwari kwa ajili ya kuuhifadhi. Na safari hii huwa ndefu hadi masaa matano kwa vijiji ambavyo ni mbali sana na mochwari.

Na huu ni upande mwingine wa umasikini unaohuzunisha kwenye vijiji masikini duniani.
 
Back
Top Bottom