PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

akili hikaa kichwani kama kichwa kina ubongo. Kama hakina, basi akili hutafuta sehemu ya kujificha. Sijui akili yako wewe imekimbilia wapi baada ya kugundua kichwani hakuna ubongo.

Vichwa nazi, wamemuua ambaye katika matukio kama hayo wanatakiwa walindwe. Sasa watawaambiaje mabwana zao huko wanakoenda kuomba kila siku. Watageukwa muda si mrefu.
 
ahsante mie chizi na wengine watusaidie mie na uchizi wangu nimeiona jeans ya blue na anaepigwa kikatili ana suruali ya khaki.ngoja nikatibiwe nikirudi niione ya khaki.
Jeans ya blue umeiona wapi we chizi?tafadhali usijibu tena hii,potezea na blue yako.We si mwanachi wa kawaida,peleka ngozi yako kwingine **** wewe!
 
Kwa ukatili huu aliofanyiwa mwenzetu na hawa Policcm bila woga wanahabari wote nchini wanajukumu la kusaidia ukombozi wa nchi hii bila kurudi nyuma, Tumeshuhudia Channel 10 ikisaidia kupotosha ukweli juu ya mambo maovu yanayofanywa na serikali hii na leo Mwandishi wao ameuawa kikatili isivyoelezeka, tunaomba wanahabari mfanye maandamano ya amani nchi nzima kulaani mauaji haya na sisi wananchi tutawaunga mkono bila woga.
 
..Inasikitisha sana, huu ni upumbavu wa kiwango cha juu na kwa namna yoyote haukubaliki, RIP Mwangosi..
 
Siku yaja ambapo amani iliyotawara kwa miaka mingi itakua historia. Tutayakumbuka haya matukio yote kama vyanzo vya kupotea kwa amani yetu, tena wakati huo si mabli kama tutaendelea hivi.
 
Kwa kuanzia hizi picha zipelekwe balozi zote na wafadhili wao wote na vyombo vyote vya haki za binadamu.Na maandamano hadi haki ipatikane!Yani nimeshikwa na hasira basi tu.Ngoja niende nikatembee kidogo nipoteze haya mawazo kwasasa.
 
hv huyu Ubungoubungo ana akili kweli acha usenge wewe,huyo jamaa angekuwa ndg yako ungelisema bahati mbaya au unaongea kwasababu limdomo unalo?
n
mods naomba huyu msimpe ban,ila thread iliyosababisha akakereka ndio ipewe ban, thread nyingine zinaudhi wakati wa majonzi mpaka mtu unashindwa kujizuia.
 

Wewe bahati mbaya gani umemwelekezea mtu bunduki?????????? angalia vzr wewe wawezaje mnyooshea mtu mshale then useme huwa unafyatuka haiitaji akili nyingi kutambua
 
Kwa kuanzia hizi picha zipelekwe balozi zote na wafadhili wao wote na vyombo vyote vya haki za binadamu.Na maandamano hadi haki ipatikane!Yani nimeshikwa na hasira basi tu.Ngoja niende nikatembee kidogo nipoteze haya mawazo kwasasa.

mkuu ukombozi wa nchi haupo mikononi mwa mabalozi wala wahisani, ni sisi wenyewe kuamka, usitegee mabalozi waje wakukomboe, utangoja milele. ukombozi unaanza na wewe. tatizo wa TZ tuna threshold kubwa sana hata mnyanyaswe vipi mnasubiri malaika na miujiza!
 
Yaani hawa jamaa wameua kikatili hivyo halafu mwingine hana habari anajinywea maji, yaani hawa kwa sasa sio walinzi wa amani wala raia bali ni wavunjifu wa amani na wauaji wa raia
 

Sijategema,hiyo ni just one of the steps,ili wajuwe chanzo ni kitu gani endapo hali itachafuka na sisi kama wananchi kuomba msaada wa kujilinda dhidi ya serikali dhalimu,endapo wataendelea kutumia nguvu na silaha za moto kuzima nguvu ya umma,umeelewa?

Halafu wewe unadhani hizo silaha wanazozitumia dhidi ya wananchi wanazitengeneza wao?
 



Kana kwamba jambo lilikusudiwa, na mtazamo wao kwa tukio ni kama wanaashiria wamefanikiwa kumtoa adui wao mkubwa, macho yao yanatoa tafusiri ya wazi mno.
 
Jamani ebu tuangalie Haya mambo upya Kama vipi jeshi la Polisi liunde upya

polisi hawana mkataba wowote na raia. polisi wana mkataba na serikali. raia kugombana na polisi ni kupotea njia. 2010 hatukupiga kura kuchagua igp, rpc au ocd. tulichagua raisi, wabunge na madiwani. hao wakiwa upande wetu polisi hawatatuua tena. ccm wangeambiwa slaa au mbowe kapigwa risasi wangetoa machozi ya mamba na hata wangejifanya kuzimia kwa mshtuko na huzuni. kwa uzoba wetu tungewaunga mkono.
sipendi kusikia kauli za kijinga zikitolewa dhidi ya jeshi la polisi. wangefanya tofauti na maelekezo wanayopewa hatua kali zingekuwa zimechukuliwa...badala yake wanapongezwa kila siku.
 
Kana kwamba jambo lilikusudiwa, na mtazam wao kwa tukio ni kama wanaashiria wamefanikiwa kumtoa adui wao mkubwa, macho yao yanatoa tafusiri ya wazi mno.[/QUOTE]

Wanatia hasira hawa jamaa
 
nimekusoma kaka. tujiunge pamoja kukomboa nchi yetu mama tanzania
 
Hivi ni risasi ndio zimeharibu mwili kiasi hiki au ameripuliwa kwa bomu?

Kama ni risasi, mwili ungeharibika kiasi hiki? Kama ni risasi ndio zimeparaganya mwili, ni risasi ngapi zimetumika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…